Makanisa ya Kikristo ya Mungu
A_P2005
Mwandamano wa Matukio wakati wa Pasaka ya Mwaka 2005
(Toleo 1.020020112-20020112)
Yoshua Masihi au Yesu Kristo ni sadaka inayokubalika (1Wakorintho 5:7 Waefeso 5:2) inayotuwezesha sisi sote kupita-juu (Waebrania 7:27; 9:26; 10:12). Kila mahali imeamriwa kuadhimisha Ushirika wa Meza ya Bwana kama ni kitu cha lazima ili kuingia katika Ufalme wa Mungu (Yohana 6:52-58). Tunapaswa kuiandaa na kujitakasa sisi wenyewe kama Hekalu la Roho Mtakatifu (1 Wakorintho 12:27; Wakolosai 1:24). Sasa tutaadhimisha kiusahihi kabisa agizo hili kama dhabihu ya Roho iliyo hai (Warumi 12:11; 1Petro 2:5; Waebrania 13:16). Tutaanza miandamano ya matukio kuanzia siku ya 1 ya mwezi wa 1 (Abib), ambayo siku hii itakuwa ni mwandamo wa Mwezi Mpya wa Mwaka Mpya, pia ni Sikukuu ya Siku iliyo Kuu sana (Isaya 66:23; Zaburi 81:3; 2 Mambo ya Nyakati 29:17; Ezekieli 46:1-4; Amosi 8:5)
Christian Churches of God
PO Box 369, WODEN ACT 2606, AUSTRALIA
E-mail: secretary@ccg.org
(Copyright © 2005 James Dailley: Huu ni mwaka wa 28 wa Yubile ya 120)
Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana
Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org and http://www.ccg.org
Mwandamano wa Matukio wakati wa Pasaka ya Mwaka 2005
Mwanzo wa Mwaka Mpya katika siku ya 1 ya mwezi wa Abibu au Nisan unaanza kwa kutegemea na mwandamo wa Mwezi majira ya saa tano na dakika kumi (5:10) siku ya Alhamisi tarehe 10 Marchi, 2005 mjini Yerusalemu. Mwishoni mwa jioni ambayo kwa wanamaji hujulikana kama wakati wa zamu ya nne ya mabaharia, au mwanzo wa kipindi cha giza, ni saa 12: 36 kwa majira ya Yerusalemu.
Muda huu unaotuunganisha wa majira ya Yerusalemu ndio unaochukuliwa katika kuanza kwa siku mpya kama vile Sabato ambayo itakuwa katika siku ya kwanza ya mwaka mpya. Siku ya Jua kupita katikati ya Ikweta (equinox) itakuwa majira ya baridi (Vernal) tarehe 20 Marchi 2005 saa 8:34. Mwaka 2005 ni mwaka wa 28 wa Yubile ya 120 na ni Yubile ya 40 kuanzia ubatizo wa Masihi. Arobaini ni kipindi kilichowekwa kwa ajili ya toba. Sayari yetu ya dunia itatimza au kufikisha Yubile ya 40, ambayo itaadhimishwa katika miaka ya Kirumi ambayo ni ktikati ya 2027 wakati wa siku ya upatanisho, hadi siku ya upatanisho ya 2028.
Itafuatiwa na mwandamano wa mambo muhimu yanayojumlishwa kwaajili ya maandalizi yetu ambayo ni: Ushirika wa Meza ya Bwana, Mlo wa Pasaka, Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa na Siku za Mikate isiyotiwa Chachu. Sikukuu ya Pasaka huadhimishwa kwa jumla ya siku saba. Tutapaswa kuwa nje ya makazi yetu/ nyumba zetu/ mahema yetu kwa jumla ya masaa thelathini na sita kuanzia siku ya 14 ya Abibu, hadi asubuhi ya Siku Takatifu ya Kwanza ya 15 (kama isemavyo Kumbukumbu la Torati 16:4-8).
Kwa kweli mtu kama atarudi kambini kwake Siku ile Yakatifu ya Kwanza hakutamfanya aonekane kuwa amelinaji kutaniko hili linalodumu kuadhimisha sikukuu kama akirudi. Sikukuu itaadhimishwa kuanzia siku ya 14 Abibu hadi 21 Abibu. Iwapo mtu au baadhi wakiamua kuendelea kuishi katika hema zao au majumbani mwao kwa baadhi ya Siku za Mikate Isiyotiwa Chachu, basi kambi ya sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachuzaoyaya itatakiwa ipangiwe mahali ambapo kutawezekana watu kufika na kushiriki kila siku bila kukosa kwa siku saba zilizobakia.
Kristo na familia yake wakishika Sikukuu hizi kikamilifu kwa siku zake zote katika mahali palipowekwa (Luka 2:41-43). Sisi tunapaswa pia kuadhimisha kwa siku nane kamili kwa kuwemo mahali pale kambi ilipo, kama wanafunzi wa Yesu walivyofanya (Luka 24). Huu sio usumbufu (Zaburi 68:19; Isaya 43:21-25; 1Yohana 5:3). Maadhimisho yasiyozingatia umakini au kuzijali ama kuadhimisha kwa kulipua Sikukuu hizi za Baba yetu huwa ni chukizo mbele za Mungu (Isaya 1:8-16). Kunajiandaa na kushiriki Ushirika wa Meza ya Bwana kwa ishara ya tendo la kuoshwa miguu na kusafishwa likimaanisha kuwa tunapaswa kujiepusha na dhambi na maovu tuliyokuwa tunayafanya na kuyatumikia tulipokuwa katika maisha ya Umisri. Kila mwaka tutapaswa kuongeza uelewa wetu juu ya mpango wa kukuza hali ya upatanisho.
Kuanzia Siku ya Kwanza ya Mwezi, katika Sabato ya Mwezi Mpya, hadi siku ya 21 mfululizo, tutatakiwa kudumu katika maombi na wakati mwingine kufunga kuombea ndugu zetu ili waweze kuokolewa na sisi wenyewe tuzidi kudumu na kulindwa na maovu.
Siku ya kwanza ya Mwezi wa Kwanza [Abibu] ni Alhamisi Marchi 10.
Siku ya Kwanza ya Mwezi wa Kwanza, ni Sabato ya Mwezi Mpya (Isaya 66:23; Ezekieli 45:1-3; Hesabu 28:11-15; Kutoka 12:2) (Au angalia toleo linalosema Mwezi na Mwaka Mpya [213].
Mwaka wa Sabato uliopita, kwa mujibu wa (Mambo ya Walawi 25:1-5), ambao pia ni mwaka wa kwanza wa mzunguko wa Yubile ikuwa tarehe 21, Marchi 1999. Mwaka huu wa 28 wa Yubile ya 40 kuanzia ubatizo wa Masihi sasa unaangukia katika mwaka wa Kirumi wa 2005, ambao pia ni mwaka wa Sabato ambao unaadhimishwa kwa majumlisho ya siku za Usomaji wa Sheria za BWANA, sawa na isemavyo (Kumbukumbu la Torati 31:9-12).
Ardhi yetu au bustani na mashamba yetu tuvunayo kila mwaka yapaswa yabakie bila kupandwa mbegu yapumzike; tuwasamehe wote tunaowadai; na hatutatoa zaka lakini tutatoa sadaka ili kutimiza agizo hili.
Mwaka unaanza na shughuli ya kulisafisha Hekalu kuanzia siku ya kwanza kwa maandalizi ya Utakaso wa Wateule (2Nyakati 29:16-19; 30:1-6; Marko 11:11-18). Soma toleo linaloitwa Utakaso wa Hekalu la Mungu [241]. Kiti cha muhimu zaidi ni maandalizi ya kila mmoja wetu kukumbuka mwandamano wa mambo ya kufanya wakati wa Pasaka (1 Wakorintho 11:25-27), ambao inalazimu kufanyika katika kambi la muda (Kumbukumbu la Torati 16:5-7; Mathayo 26:17-19).
Siku ya saba Mwezi wa Kwanza ni siku ya mafungo kwa ajili ya Utakaso siku ya Jumatano, Marchi 16.
Siku ya saba ya mwezi wa kwanza tutakuwa na mfungo kwa ajili ya toba kwa makosa yote tuliyofanya ama kwa kutokujua yaani kwa ujinga (Ezekieli 45:18-20; Marko 11:12). Soma toleo la Utakaso wa Hekalu na Makosa [291]. Mafungo haya yataanzia baada ya jua kuchwa tarehe 15 Marchi na kuishia machweo ya tarehe 16 Marchi, kufuata machweo kama isemavyo (Mwanzo 1:5; Zaburi 104:19; Nehemia 13:19; Walawi 23:32 Matendo 27:27-33).
Majira ya machweo ya jua yaliyo katika maeneo yako au muda ujulikanao kama majira ya jioni ya mabaharia kubadilishana zamu zao yatapaswa kuheshimiwa. Lakini anuani ya tovuti tunayokupa hapa chini itakusaidia kujua muda sahihi unaotakiwa http://aa.usno.navy.mil/data/docs/RS_OneYear.html
Fungulia kwa ‘aina ya somo unalotafuta’ halafu isemapo nautical twilight; (yaani zamu ya machweo ya jua) kasha jaza kueleza mahali ulipo kasha bonyeza upate maelezo ya mwaka mzima kwa ajili ya maeneo yako, kasha Compyuta itakuonyesha.
Wakati huu tutatubu na kuomba Mungu atusamehe kwa dhambi tulizozifanya kila mmoja nafsi yake, na makosa tuliyomkosea Mungu kwa kutokujua katika Mwili wa Kristo, kwa Kanisa la Mungu, kwa familia zetu na kwa mataifa, na kuimbea sayari yote ya dunia ifunguliwa na kupatana na Mungu, Baba yetu.
Wale wote waiobatizwa wanapaswa hushiriki maombi haya ya kufunga (Yoeli 2:12-18). Huu ni wajibu wetu tulionao yaani kusaidia Bibi Arusi wetu katika kusafisha nyumba kwa ajili ya maandalizi ya Mlo wa Arusi ijayo (Ufunuo 19:7-8). Damu ya Kristo hutakasa (Waebrania 13:12), pale inaporuhusiwa kufundishwa Kweli (Yohana 17:17).
Tunafunga kama ni sehemu yetu muhimu katika hatua za upatanisho na ondoleo la dhambi (Yoeli 1:14). Hii pia ni kwa niaba ya makutaniko yanao potea kwa kuendeleza makosa au ujinga unaowapelekea kuyakataa mafundisho yenye uzima na kuendeleza kuyaandama mafundisho ya udanganyifu (Yoeli 2: 10-27) kwa ajili ya “Siku ya Bwana” inayokuja. Pia tunasisitiza kuhusu Bwana Arusi wetu ajaye na kujifunza njia sahihi ya kuzaa watoto watakaomiliki ufalme kipindi cha utawala wa Milenia kama watu waliowekwa wakfu na kutakaswa (Ufunuo 19:9).
Kasha tutaendelea na maandalizi ya kila mara ya kibinafsi ya Pasaka kwa kuupambanua mwili kwa njia ya kujihoji nafsini mwa kila mmoja (1Wakorintho 11:28-32; 2Wakorintho 13:5). Hii inafanyika ili kwamba ituwezeshe kukua na kwamba tusipatwe na hukumu ya Kristo (1Petro 4:17; 1Wakorintho 11:31-33).
Siku ya kumi ya Mwezi wa Kwanza ni Jumamosi Marchi 19
Hii ni siku ambayo Mwana kondoo alitengwa (Walawi 12:3). Matoleo ya Sadaka maalumu kwa ajili ya Sikukuu inapaswa yafanyike mapema ili kwamba uchambuzi ufanyike kwa wakati huu. Kanuni ya kiroho ya “kutenga kando kwa maana maalumu” itafanyika wakati wa Sabati hii wakati wa maandalizi ya kibinafsi.
Siku ya kumi na nne ya Mwezi wa Kwanza ni Ushirika wa Meza ya Bwana. Itaadhimishwa siku ya Jumanne jioni baada ya machweo ya jua tarehe 22 Marchi
Baada ya siku ya kumi na tatu ya maandalizi, katika siku ya kumi na nne wakati wa machweo ya jua, ni Ushirika wa Meza ya Bwana (1Wakorintho 11:17-20) (soma toleo lisemalo Ushirika wa Meza ya Bwana [103]. Inatanguliwa na ibada ya kuosha miguu (Yohana Mt. 13:1-17; Yohana 12:1-8), ambayo ni ya muhimu kufanyika kila mwaka kama ishara ya marudio ya ungamo la ubatizo (1Petro 3:21). Hii hufanyika kabla ya kupokea mfano wa mwili na damu ya Kristo (Yohana 6:27-58). Ni Mkate usiotiwa Chachu tu unaoruhusiwa kutumiwa katika Ibada hii (Kutoka 23:18; 34:25). Hii ni amri ya kila mwaka iliyoamriwa kufanyika kwa ukumbusho, ambayo ni pekeyake huadhimishwa usiku, n ani kwa usiku ule tu ambao alisalitiwa (1Wakorintho 11:23-29). [soma toleo linalosema Ishara ya Kuoshwa miguu [099] na Ishara ya Mkate na Divai [100].
Hii ni muhimu kushiriki kama ishara ya nje inayowakilisha uhalisiwa ndani unaokiri kukubaliana na mafundisho yenye uzima yenye kufundisha kweli ya mneno ya Mungu wa Pekee wa Kweli (Kutoka 24:11; Kumbukumbu la Torati 8:3; Yeremia 15:16; Ezekieli 2:8-10, 3:1-3). Wanaostahili kushiriki ibada hii ni wale watuwazuma waliobatizwa tu. Kwa mujibu wa Biblia, watoto walio kwenye nyumba za wateule wametakaswa na wateule wametakaswa na Mungu Baba (1Wakorintho 6:11; Waebrania 10:29) na wanalindwa na Yesu Kristo (Yuda 1:1; Waebrania 10:10). Roho Mtakatifu ni Roho wa Mungu wet una kwa kupitia jina la Yesu Kristo; wateule wameoshwa dhambi zao kwa njia ya dhabihu ambayo inaendelea kwa njia ya imani kwa Mungu na Roho wake Mtakatifu (Matendo 26:18).
Ifikapo saa tisa kamili (9:00) jioni ya Jumatano, tarehe 23 Marchi, kutakuwa na ibada takatifu. Huu ni muda ambao Mwana Kondoo alitolewa kuwa dhabihu ya msamaha wa dhambi ( Kutoka 12:6; Kumbukumbu la Torati 16:5-6; Pia inathibitishwa na mwanazuoni maarufu wa Kiyahudi wa karne ya kwanza aitwaye Josephus; katika kitabu chake kiitwacho Josephus na Vita ya Wayahudi, sura ya 6, ukurasa wa 9, aya ya 3). Tutaadhimisha Pasaka au Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu na kutoa sadaka baada ya ibada hii, ambayo ni kukumbuka Kifo cha Mwana Kondoo (soma nakala ya toleo lisemalo Kifo cha Mwana Kondoo [242].
Hii ni ya kwanza kati ya Sikukuu tatu kuu za kila mwaka zinazotolewa sadaka (Kumbukumbu la Torati 16:16; Kutoka 23:17; 34:23). Sadaka hii inatakiwa ikabidhiwe mapema kabla ya asubuhi ya siku ya kwanza ya Mikate isiyotiwa Chachu (Kutoka 23:18; 34:25). Vyombo vyote vilivyokidiwa havitakiwi vionekane na aina yoyote ya kitu chenye chachu yaani hamira ndani yake (Kutoka 12:15, 19, 13:7; Kumbukumbu la Torati 13:6). Tendo la kuyaacha makazi yetu ya kudumu yafaa lifanyike mapema kabla ya siku ya Pasaka.
Iwapo kama kwa bahati mbaya mtu atashindwa kushiriki Ushirika wa Meza ya Bwana kwa siku ile iliyopangwa kwa sababu za muhimu kama vile alikuwa anaumwa au bahati mbaya yoyote ile ilimpata na asishiriki na wenzake jioni ile, basi marudio yatafanyika katika machweo ya tarehe 21 Aprili na atashiriki. Hii ni siku ya 14 ya Mwezi Unaofuata kama inavyoagiza Hesabu 9:9-11; 2 Nyakati 30:2-3, 12-15.
Siku ya Kumi ya Mwezi wa Kwanza ni Pasaka. Chakula kitaliwa siku ya Jumatano jioni Marchi 23
Huu ni Mlo wa Pasaka (Kutoka 12:6-11). Ni siku ya kwanza ya Mikate isiyotiwa Chachu, ni Siku Takatifu (Walawi 23:6; Hesabu 28:17) na maadhimisho ya usiku vilevile inaelezewa kama ni Usiku wa Kuuangalia Sana au ni Usiku Maalumu wa Kuwa Macho nao (Kutoka 12:42, 13:3). Neno hili linapaswa kusomeka [kama linavyoonekana katika toleo la chapisho lisemavyo ni Usiku wa Kuuangalia [101]].
Mwishoni mwa mlo huu watoto au wale ambao hawaja ongoka watauliza “Je, ni kwanini tunafanya hivi?” (Kutoka 12:26; 13:14). Maana ya Pasaka na mfano wake wa divai (Kutoka 29:40), Mwana kondoo (Kutoka 12:27), mikate isiyotiwa chachu (Kutoka 12:39; Kumbukumbu la Torati 16:3-6) mboga za uchungu (Kutoka 1:14, 12:8; Hesabu 9:11) na matumizi ya chumvi lazima tafsiri zake zielezewe na wote.
Unywaji wa divai ulionwkana kuambatana na aina nyingi ya sadaka (Kutoka 29:40; Walawi 23:13; Hesabu 15:5, 7, 10; 28:7 & 14). Katika siku zijazo za Utawala wa Milenia tunaona ibada hii ya kutoa dhabihu za asubuhi itarejeshwa na kuwepo tena (Ezekieli 46). Kwakuwa sadaka za vinywaji na divai kuwakilisha kama fumbo la damu, hii ilikamilishwa na iko nje ya idadi ya sadaka hizi zitakazotolewa katika siku za ufalme uliotabiriwa.
Divai: (Mwanzo 14:18; Kutoka 29:40; Walawi 23:13; Hesabu 15:1-10, 28:14).
Mwana Kondoo: (Kutoka 13:13 & 29:39 Walawi 4:32)
Mikate Isiyotiwa Chachu: (Kutoka 12, 13:4-10, 29:1-24; Kumbukumbu la Torati 16:3; 1Wakorintho 5:5-8)
Mboga zenye Uchungu: (Kumbukumbu la Torati 32:18-24; 2Wafalme 14:24-26; Amosi 8:7-12; Mika 2:1-7; Yakobo 3:8-14; Ufunuo 8:11)
Chumvi: (Walawi 2:13; Hesabu 18:19; 2Nyakati 13:5; Marko 9:49-50
Kwanini mifupa ya Mwana Kondoo haitakiwi ivunjwe? (Danieli 6:24). Sawa na (Kutoka 12:46; Hesabu 9:12; Yohana 19:32-36; Zaburi 34:15-20).
Ahadi ya kukombolewa kwao Israeli na kila wenye mwili katika Mpango wa Mungu unahitajika kufafanuliwa kwa usahihi sana kwa wasikilizaji wetu wote. Kila mmoja kibinafsi anatakiwa kujitafutia fursa kwa ajili ya kufanya upatanisho na Mungu.
Kila mmoja anatakiwa kuifahamu tofauti iliyopo kati ya utakaso wa kimwili wa Israeli ulio chini ya Agano na ukombozi wake kutoka utumwani na ukombozi wa kiroho wa Israeli kutoka na nguvu za mauti. Ruhusu watu wote washiriki na wajifunze kufafanua vifungo vya kiroho. Somo hili linafaa liendelee hadi kufikia baada ya usiku wa manane.
Sisi sote tutamla mwana kondoo au nyama kutoka hatika kundi la wanyama wetu, na kuindaa kwa kuioka bila kuwa na mfupa ndani. Kule Misri nyama yote iliyobakia na mifupa iliyovunjika zilichomwa moto (Kutoka 12:10). Hii ilifanyika hivyo ili kwamba sadaka hii, ambayo ilimtakasa mzaliwa wa kwanza wa Israeli, asiweze kuchukuliwa na kutolewa sadaka kwa miungu wa uwongo na Makuhani wa Misri. Mlo huu ni uwakilisho wa kimwili wa tangazo la kimwili ya kwamba Baba yetu atafanya upatanisho na kila mwenye mwili aliyewaumba.
Wakati wa kipindi cha kujikumbushia cha wiki, ibada za asubuhi lazima zifanyike. Masomo na majadiliano vitaendelea wakati huu wote wa mihimu sana.
Siku ya kumi na nane ya Mwezi wa Kwanza ni Jumapili ya Marchi 27. hii ni Siku ya Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa
Mganda wa Kutikiswa kama isemavyo (Walawi23:9-14) ni mfano wa malimbuko ya mavuno ya kwanza (Kutoka 34:26, 1Wakorintho 15:20). Mwana Kondoo alitakaswa majira ya saa tatu kamili (3:00) asubuhi na kutolewa kama kondoo wa Pasaka saa tisa kamili (9:00) alsiri. (Kutoka 29:19-29; Walawi 14:12-24; 23:11) kwa utakaso wa ukuhani mpya wa utaratibu wa Melkizedeki (Waebrania 5:1-10, 6:20, 7:11-16). Chakula kipya cha kiroho chaweza kuliwa, kwa maana ya kuwa neno lililofanyiwa tafsiriwa na lenye kueleweka vizuri kwa wakati huu (soma toleo lisemalo Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa Na.106b).
Ibada hii ni lazima ianzie saa tatu (3:00) asubuhi kwa kipindi chote cha Mikate Isiyotiwa Chachu sio Sabato. Siku hii na muda wake huandaa mwanzo wa hesabu ya siku hadi kufikia siku ya Pentekoste ambayo itafanyika katika siku ya Jumapili ya Mei 15, 2005.
Siku na saa imeelekezwa kwenye Kanisa la Mungu ambalo ni malimbuko ya mavuno ya pili (Kutoka 34:22; 1Wakorintho 15:22; Yakobo 1:18; Ufunuo 14:4).
Siku ya Ishirini na moja ya Mwezi wa Kwanza ni Jumatano Marchi 30
Siku ya Mwisho ya Mikate Isiyotiwa Chachu ni Siku Takatifu (Walawi 23:8; Hesabu 28:25; Kumbukumbu la Torati 16:8). Ibada ya Siku Takatifu itafanyika kuanzia saa tatu (3:00) asubuhi hadi saa nane (8:00) mchana.
Wapendwa, ni watu wachache sana wanaojitoa nafsi zao kikamilifu kuzitunza siku hizi ishirini na moja za kipindi cha utakaso (Danieli 10:7-14). Wengi watawadhihaki na kuwakebehi na hata kuwatesa wale wanaozitunza siku hizi kikamilifu na wanaojitoa nafsi zao kikamilifu kwa mioyo yao yote (2Nyakati 30:10).
Kwa kadiri siku zinavyoendelea, wengi wataweza kuelewa na kupambanua hadi kuona maana na umuhimu wake. Hata kwa kupitia makosa hivi, wengi wanaweza kuokolewa na hukumu kwa maombi ya watu binafsi wenye haki (2Nyakati 301820, pia soma toleo la Chachu ya Kale na Mpya, Na. 106a).
Fanya bidii kutimiliza mambo yaliyoelekezwa hapa na ondoa kila ain azote za ibada za sanamu katika maisha yako. Sanamu za mwanadamu zinachukua wajibu kwa ajili ya aina karibu zote za laana zinazotukabili na zitafikia mahali ambapo adhabu itatufikia (Ezekieli 14:12-23).
Ibada za sanamu itatuongezea ufinyu na ukosefu wa maarifa (Isaya 45:16) ya kumjua Baba yetu ambayo anataka tuwenayo (Ezekieli 14:1-11, 20:31-44, 37:23).
Kuna masharti makuu matatu ili kuurithi uzima wa milele katika Ufufuo wa Kwanza na inahitajika kufahamika vema. Yatupsa tuelewe Ninani, Linini a jinsi gani tunapaswa kumuabudu na ufahamu huu unahusiana na misimamo yetu ya kiimani, viwango vyetu vya imani na utii wetu.
1. Tunapaswa kuamini na kujua kuwa kuna Mungu Mmoja Tu wa peke na wa Kweli (Kumbukumbu la Torati 6:4; Malaki 2:10; Waefeso 4:6) na tunapaswa kumjua Yesu Kristo aliyemtuma (Yohana 17:3; 1Timotheo 2:5; 1Wakorintho 8:4-6).
2. Ttunapaswa tumwnini Yesu Kristo kwa kupitia katika ufahamu wa kwamba kuna Mungu wa Pekee wa Kweli (Yohana 17:3). Hii itamfikisha mtu kwenye toba hadi kwenye ubatizo na kupokea Roho Mtakatifu, kwa njia ya imani ambayo Mungu alimfufua kutoka kwa wafu (Warumi 10:9).
3. Yatupasa Kutii na kushiriki katika Ushirika wa Meza ya Bwana na miguu iliyooshwa na kula mwili na kuinywa damu ya Yesu Kristo (Yohana 6:53-58; 1Wakorintho 6:11).
Kuna haja kubwa ya kuwa na Roho Mtakatifu. Bila ya Roho wa Mungu hatutaweza kuuingia ufalme wa Mungu na kuwa na uzima wa milele na kuwa na sehemu katika Ufufuo wa Kwanza (Warumi 8:11) au na hata ule wa Pili (Ezekieli 37:12-14).
Roho ndiye kiini cha ibada zetu kwa Mungu (Yohana 4:23; Wafilipi 3:3). Kwa kumpokea Roho Mtakatifu wa Mungu, atatuwezesha kuzitii amri zote za Mungu (1Yohana 3:24) na tunafanyika wasafi wakati wote (1Wathesalonike 4:7-8) na tutakuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo (Ufunuo 12:17; 14:12).
Kama hutaweza kuwa ni miongoni mwa watakaoshiriki maadhimisho ya sherehe hizi katika siku ya 14 ya mwezi kwa makusudi kabisa, ujue ukweli huu wa kwamba wewe hutakuwa na sehemu na Yesu Kristo (Yohana 13:8), Yatunapasa sote tushiriki na kuupambanua mwili wa Kristo, kwa mafano Kanisa la Mungu, na maandalizi yake kuchukua mfano wa mwili na damu kama inavyopasa kwa ajili ya uzima wetu wa milele (Yohana 6:54).
Lazima tuwe na hakika kuwa tunamuabudu Mungu wa pekee wa Kweli na kwa zile siku tu alizozitenga mwenyewe na sio kwa kujiwekea siku zetu nyingine tulizoziona zinafaa kwa kufuata matakwa au hekima zetu wenyewe. Tunapaswa kumuabudu kwa kufuata utaratibu ambao yeye mwenyewe aliuweka na sio kwa kufuata taratibu zetu wenyewe tuzipendazo.
Ukombozi wa mwanadamu unategemea kwa maeneo yote mawili, yaani maisha ya kiroho na utaratibu wa kijamii. Uumbaji wote, uumbaji wa kimwili wa uzao wa Adamu na utu unaofanyakazi katika ulimwengu wa roho au uumbaji hatimaye vyote vitapata ukombozi (Warumi 8:19-39).
Uwezo wetu wa kuelewa mambo utaongezeka, “mawazo yatahuishwa” na Mungu, iwapo tutazitii kwa bidii na kikamilifu amri zake,
Mithali 16:3 inasema: Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika.
Kwa kuwa tunampenda Mungu wetu wapekee na Wakweli na Baba yetu, basi tutashika maelekezo yake yote, haitajalisha eti nini ninatokea.
Kumbukumbu la Torati 6:1-25, inasema: Na ndiyo sheria, na amri, na hukumu, alizoziamuru BWANA, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki; 2 upate kumcha BWANA, Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, siku zote za maisha yako; tena siku zako ziongezeke. 3 Sikiza basi, Ee Israeli, ukaangalie kuzitenda; upate kufanikiwa, mpate kuongezeka sna, kama BWANA, Mungu wa baba zako, alivyokuahidi, katika nchi ijaayo maziwa na asali. 4 Sikiza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja. 5 Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, pia kwa nguvu zako zote. 6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; 7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena, uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. 8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. 9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako. 10 Tena itakuwa atakapokwisha BWANA, Mungu wako, kukuleta katika nchi aliyowaapia baba zako, Ibrahimu na Isaka na Yakobo, yakuwa atakupa; miji mikubwa mizuri usiyoijenga wewe, 11 na nyumba zimejaa vitu vyema vyote isizojaza wewe, na visima vimefukuliwa isivyofukua wewe, mashamba na mizeituni usiyoipanda wewe, nawe utakula na kushiba; 12 ndipo ujitunze, usije ukamsahau BWANA aliyekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa. 13 Mche BWANA, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake. 14 Msifuate miungu mingine katika miungu wa mataiafa wawazungukao; 15 kwani BWANA, Mungu wako, aliye katikati yako ni Mungu mwenye wivu; isije ikawaka juu yako hasira ya BWANA, Mungu wako, akakuangamiza kutoka juu ya uso wa chi. 16 Msimjaribu BWANA, Mungu wenu, kama mlivyomjaribu huko Masa. 17 Zishikeni kwa bidii sheria za BWANA, Mungu wenu, na mashuhudizo yake, na amri zake alizokuagiza. 18 Nawe yaliyo sawa, na mema, machoni pa BWANA; ili mate kufanikiwa, nawe upate kuingia na kuimiliki nchi nzuri BWANA aliyowaapia baba zako, 19 ya kuwa atawasukumia nje adui zako wote mbele zako, kama alivyonesema BWANA. 20 Na zamani zijazo atakapokuuliza mwanao, akikuambia, N’nini mashuhudizo, na amri, na hukumu, alizowaagiza BWANA, Mungu wetu? 21 ndipo umwaambie mwanao, Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri; BWANA akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu; 22 BWANA akaonya na maajabu, makubwa mazito, juu ya Misri, na juu ya Farao, na juu ya nyumba yake yote, mbele ya macho yetu; 23 akatutoa huko ilikututia huku, apate kutupa nchi aliyowaapia baba zetu. 24 BWANA akatuamuru kuzifanya amri hizi zote, tumche BWANA, Mungu wetu, tuone mema siku zote, ili atuhifadhi hai kama hivi leo. 25 Tena itakuwa haki ketu, tukitunza kufanya maagizo haya yote mbele ya BWANA, mungu wetu, kama alivyotuagiza.
AMINA, ELOH.
Mwandamano wa Matukio wakati wa Pasaka ya Mwaka 2005 [A_P2005]
q