Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[157]

Utaratibu wa Kufuata Wakati wa Ibada ya Meza ya  Bwana

Jinsi ya kushiriki Meza ya Bwana mahali ambapo wazee hawapo

(Toleo la  1.1 19960323-19991008)

Inatoa taarifa kwa ajili ya wale ambao hawawezi kushiriki na kundi.

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

E-mail: secretary@ccg.org

(Copyright © 1996, 1998, 1999  Wade Cox)

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

.

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org and http://www.ccg.org


Utaratibu wa kufuata wakati wa Ibada ya Meza ya Bwana

Kama unastahili na unazo sifa za kushiriki kula Meza ya Bwana, lakini huwezi kufika mahali mahali lilipo mojawapo ya kutaniko la Makanisa ya Mungu kwa wakati muafaka vile uko mbali nayo, unaweza kushiriki peke yako au pamoja na kundi la wenzako wenye sifa hizo za kustahili kushiriki kama ulivyo wewe.

Andaa meza ya Bwana kwa kununua aina yoyote ya mkate ambao hauchanganywi na chachu au hamira, kwa Wayahudi hutumia mkate unaoitwa Matzoth au Matzos kutoka kwenye stoo ama glosari yoyote au jitengenezee mkate usiotiwa chachu. Huu unatengenezwa bila kutiwa aina yoyote ya hamira, aina yoyote ya soda, unga wa kuumuka au aina yoyote inayohusiana na chachu. Re-vita au kila kilicho katika jamii isiyo na chachu kama vile Biscuit zaweza kutumika.

Jinunulie chupa ya mvinyo mwekundu, unaokubalika kuwa unafaa, wenye kiwango kizuri cha ubora. Vinywaji kama vile Cabernet Sauvignon au Shiraz ni baadhi ya zinazofaa. Usitumie divai yenye kileo ndani kama vile divai za Kihispania zinazoitwa Sherry au zinazo vundikwa kwenye kibuyu.

Juisi za zabibu zilikuwa hazitumiki kabisa wakati wa kipindi cha Pasaka kwa Myahudi yeyote au Mwuisraeli, akiwemo Kristo mwenyewe, mitume au na Kanisa la Agano Jipya. Mafundisho ya madhehebu potofu ya karne zilizopita hivi karibuni yamo katika juhudi zao tu za kupotosha ukweli. Juisi ya zabibu haiwezi kutumika katika mazingira kama haya. Imekufa, wakati ambapo divai inao uzima na inakuwa ni mfano wa damu iliyohai ya Yesu Kristo kama mwanadamu.

Fanya maandalizi ya Chakula cha Meza ya Bwana, kwakutenga mbali balasi lillyo safi na taulo kwa ajili ya kuoshea miguu, na kuanza ibada wakati wa majira baada ya machweo ya jua kumekuwa giza, muda muafaka usiwe ni usiku sana. Andaa chumba kiweke tayari kwa ibada na kisafishe na maridadi. Jifanyizie kiasi kidogo cha mikate na divai pembeni mwake, kwenye sinia, chini ya kitambaa cha mezani au cha mkononi. Tumia kipimo sawa cha bilauri kwa kila mmoja kwa kipimo kidogo kwa kila bilauri.

Isiliwe ndani ya malango ya nyumba yako. Inapaswa ichukuliwe na kuliwa mbali na malango ya nyumba yako, kama ilivyo kwa jioni ya siku inayofuatia, wakati wa Pasaka (au kama iitwavyo; Usiku wa Kuangaliwa Sana) sawa na isemavyo Kumbukumbu la Torati 16:6-7 (soma toleo lisemalo Usiku Wa Kuangaliwa sana [101]. Asubuhi ya Siku ya Kwanza ya Siku Takatifu waweza kurejea kwenye malango ya nyumba yako. Wale ambao ni wagonjwa na wadhaifu wa afya ambao hawawezi kutembea wanaweza kubakia majumbani mwao.

Ibada hii inatakiwa ifanyike katika hali ya heshima na utukufu wa kisherehe. Hata hivyo hii haiwi ni ibada yenye kufanywa ikitawaliwa na ukimya watu wanaruhusiwa kufanya maongezi. Wakuu wa familia, au mtu aliyechaguliwa kwa kutaniko lile kubwa, anaweza kuongoza ibada hii. Kanda ya tepu inayofundisha kuhusu Ibada ya Ushirika wa Meza ya Bwana inapatikana na kwa ajili ya ibada imechapishwa (angalia toleo lisemalo    Ushika wa Meza ya Bwana, [103]. Karatasi ya mwongozo inapaswa ufuatwe kwa kuisoma ukiitikiwa na washiriki wa ibada hii. Wale wote wasiobatizwa hawaruhusiwi kushiriki kula chakula cha ushirika ingawa tu wanaweza kuruhusiwa kuwepo mahali hapo na kufuata maongozi mengine ya ibada. Hii ni ibada muhimu sana ya ukumbusho wa Karamu ya Mwisho ya Bwana wetu Yesu Kristo kabla hajatolewa kama Mwana Kondoo wa Pasaka katika jioni iliyofuatia, ambayo ni Usiku wa Kuuangalia Sana ambao ni usiku wa pili wa majira ya Pasaka (Kut. 12:8-11; Kum. 16:6-7). Hii ni Pasaka yenye maana sawa tu na ile iliyo katika Kutoka na usiku ule ambao Israeli walilindwa na Mwana Kondoo wa Pasaka.           

Kwa kweli hakuna mkate wala divai iliyotumika katika jioni ile ya kwanza wala katika mlo wa siku ya pili ulioruhusiwa kusalia hadi subuhi ya Siku Takatifu ya kwanza. Ni lazima kiharibiwe.

Ikitokea kwa bahati mbaya kuwa hii karatasi ya toleo letu la Ushirika wa Meza ya Bwana [103] haipo ili isomwe, basi viongozi wa ibada watatakiwa maandiko yaliyo sawa na hayo kutoka katika Biblia. Mtu huyo atatakiwa asome mbele za kutaniko hili Luka 22:7-8 na 14-15; kasha Mathayo 26:17, 26-30; kasha aendee kusoma 1Wakorintho 11:23-30 na kasha Yohana 13:1-17. Uoshaji wa miguu utatakiwa ufanyike iwapo kama kuna watu waliobatizwa wanaoanzia idadi ya wawili au zaidi yake. Mahali penye watu wengi watatakiwa wajipange kwa kujigawa kufuatana na jinsia na wakae mahali muafaka. Watu binafsi kwa kweli hawawajibiki na suala hili. Baada ya kumalizika kwa shughuli hii basi kirudishe chumba katika hali yake ya kawaida.

Kisha kutatakiwa kuelezea maana ya kushiriki kwa mkate na divai na kasha mwongozaji wa ibada atamshukuru Mungu na kuombea baraka ule mkate kama ishara ya mwili wa Yesu Kristo, kasha atauvunja vipande vipande na kuugawa kwa waliohudhuria. Kila mmoja atashiriki kuula mkate huu katika mazingira ya ukimwa na tafakari kuu.

Kisha baada ya hapo, kiongozi wa ibada ataombea divai na kumshukuru Mungu na kuiombea baraka ili kama ishara takatifu ya damu ya Yesu Kristo iliyo mwagika kwa ajili ya ondoleo ya dhambi zetu. Kasha kikombe cha divai kitapitishwa na kumimina divai kwenye vikombe vya kila mmoja na kunywewa kama ishara ya marudio ya ukiri ya kuwa damu ni kweli damu ya Yesu Kristo ilimwagika kwa ajili ya ondoleo la dhambi zandu.

Kisha baada ya hapo, bilauri zote na mikate ambayo haijatumika yote itarudishwa kwenye sinia na ile meza itafunikwa kwa kitambaa kikubwa au hata kidogo kilichopo.

Kisha kiongozi wa ibada atasoma angalau sehemu ya maandiko matakatifu kutoka katika Injili ya Yohana 13:18 hadi Yohana 17:26. Baada ya maneno haya kutamkwa na Kristo, kasha aliondoka kwenda bustanini ambako hatimaye alikamatwa na kusulibiwa. Kiongozi wa ibada atasoma sehemu ya maelezo ya ziada kuhusu ibada ile kama itakuwa imewekwa kwenye ratiba. Kama kuna wahudhuriaji wengi, basi nyimbo kutoka kwenye vitabu zinaweza kuimbwa kama nafasi itakuwepo au kama inawezekana kufanya hivyo.

Kisha kutaniko laweza kutawanyika na kurudi kwenye vyumba vyao walivyopangisha kwa muda.

                                                                                                                                             MWISHO!           

q