Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[255]

 

 

Torati na Amri ya Tatu ya Mungu

 (Toleo Na 4.0 19981006-20050810-20120520)

 

Imeandikwa: Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.. Amri hii ya Tatu inahusika na dhana nzima ya mamlaka na uweza wa Mungu kwenye mfumo wake wa Utaratibu wa Torati. Amri hii sio tu kwamba inahusu tu kukufuru na kunajisi matumizi ya jina lake kwanye maongezi bali pia inahusika na sheria yote ya kijamii na kidini na Kalenda imewekwa kwa ajili ya kutumiwa kwenye mfumo huu. Katika kutilia maanani kumfanyia Mungu kwenye utaratibu mwingine ambao pia ni kuvunja amri hii.

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 1998, 1999, 2005, 2012 Wade Cox et al, ed. Wade Cox)

(tr. 2012)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org


Torati na Amri ya Tatu ya Mungu

 


Imeandikwa:

Kutoka 20:7 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure

 

Kumbukumbu la Torati 5:11 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure

 

Jina la Mungu liko kwenye tarakimu ya umoja kama jina kale lilivyo la Eloah. Yeye ndiye kiini cha nguvu na mamlaka yote na ndiye anayestahili kuwa kiini au mlengwa wa ibada kenye Hekalu (Ezra 4:17-7:26).

 

Malaika wa mbinguni wanapewa uweza wa kiungu, yaani kuwa elohim wakishirikiana na Eloah, katika maumbile yao kama sisi tunavyofanyika kuwa na uweza wa kimungu yaani elohim. Hata hivyo Eloah au Mungu ni mmoja tu.

Kumbukumbu la Torati 6:4-5 4 Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. 5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

 

Kutoka 3:14 inatuonyesha jinsi Mungu anavyofanyika kuwa kitu fulani. Hapa anasema, Mimi niko ambaye niko, yaani “Nitakuwa kama Nitakavyokuwa”( kwa mujibu wa Tafsiri ya Biblia ya Oxford Annotated RSV na ya Bullinger, na Comanion Bible kwenye aya zake, neno lililotumika ni ‘eyeh ‘asher ‘eyeh). Tunaona jinsi Mungu anavyojieneza mwenyewe na kuwa ni “yote ndani ya yote”.

 

Sheria za Mungu-Mfumo wa Utaratibu

Ni tengo ka uvunjajis wa Sheria za Mungu na amri ya tatu ya Mungu kuuweka mfumo wa sheria au imani iliyokinyume na isemavyo Biblia na maelekezo au kanuni zake. Mfumo mzima unaoonekana kugeuza Amri za Mungu. Hairuhusiwi kuweka aina yoyote ya utaratibu wa sheria na kuzichagua nyingine.

 

Hairuhusiwi kudai kuwa tunamwabudu Mungu Aliyehai kwa jina la Yesu Kristo na wakati huo huo tukizidharau au kutozitunza Sabato na Sikukuu zake, na kuupa nafasi mbadala mfumo wa wa imani zinazotokana na upagani na ibada za kuabudu Jua. Ndivyo ilivyo kwamba ibada za siku ya Jumapili na maadhimisho ya sikukuu za Krismas na Easter sio tu kuwa yanapingana na kuivunja amri ya hii ya Tatu, bali ni kuzivunja amri zote. Mungu anasema kwamba anazichukia Sikukuu na Sabato zao. (Isa. 1:11-20) kwa ajili ya unafiki huu mkubwa.

 

Sabato ya uwongo haina maana tu ya lile tendo la kufanya ibada siku nyingine asiyoiamuru Mungu tu, kama ilivyo Jumapili, bali ni tendo la kumuabudu Bwana Mungu bure au kumfanyia ibada isiyo na maana, kwa kutojali haki na kutenda uovu na machukizo na unafiki. Kungu anawachukia makuhani hawa wa uwongo na waabudu sanamu. Ni watu waliovaa mavazi meusi na wanaomtumikia Baali na mungu Jua (kama ilivyoandikwa kwenye 2Fal. 23:5; Hos. 10:5; Sef. 1:4).

 

Mamlaka yote imetakiwa itumike kwa ajili ya kuyafanya mambo yote yaihusuyo Torati ya Mungu. Aina yoyote ya imani ya kidini inayopingana na maudhui ya Biblia na maana zake au inayoathiri au yanayobadili maana iliyo kwenye torati au utaratibu wake ni yana maana sawa tu na hii ya kulitaja jina la Mungu huyu wa Pekee na Wakweli bure; na ni kuivunja Amri ya Torati yake iliyoko kwenye amri ya tatu. Na ni kwamba wanafundisha kinyume na neno la Mungu na wanalichukua jina lake pasipo na maana ya kimungu na pasipo mamlaka yake na kwa hiyo kulifanya lisiwe na maana au heshima yoyote.

 

Jina la Mungu

Mambo yote yahusuyo kutumia mamlaka yaliyo kwenye mambo ya Mungu yanafanywa kwa jina lake akiwa ni Yahova na wanayatumia mamlaka yake kwa namna iliyo sawa tu na kama anavyofanya mfalme aitumiapo pete yake itumiwe kama muhuru wa kuidhinisha jambo (sawa na ilivyoandikwa kwenye jarida la Malaika wa YHVH [The Angel of YHVH (No. 24)]; katika kitabu cha Mwanzo sura za 18 na 19).

 

Mungu anatuonya na kutufundisha sisi. Upole wake hutufanya tuwe wakamilifu na tuna ngao ya wokovu wake. Yeye ni ngome yetu na mkombozi wetu (soma 2Sam. 22:32-35; Zab. 18:34; 144:1). Mamlaka na uweza vyote ni vya Mungu na mamlaka yaliyoko yote ni ya Mungu (Rum. 13:1,2,7).

 

Kwa hiyo tuapaswa kumtii Mungu kuliko wanadamu (Mdo 5:29). Kisasi ni juu yake yeye na ni yeye awezaye kufidia na kulipiza kwa haki (Kum. 32:35; Zab. 94:1; Ebr. 10:30; Rum. 12:19).

Kumbukumbu la Torati 10:20-22 Mche Bwana, Mungu wako, umtumikie yeye; ambatana naye, na kuapa kwa jina lake. 21 Yeye ndiye fahari yako, na yeye ndiye Mungu wako, aliyekutendea mambo haya makubwa, ya kutisha, uliyoyaona kwa macho yako. 22 Baba zako walishukia Misri na watu sabini; na sasa Bwana, Mungu wako, amekufanya kama nyota za mbinguni kwa wingi.

 

Kwa hiyo, tumekatazwa kulitumia jina la Mungu bure, au kufanya viapo vya uwongo kwa jina lake. Yeye ni mtakatifu, na jina lake ni kuu na linatisha (soma Kutoka 20:7).

 

Mambo ya Walawi 19:12 Msiape uongo kwa jina langu, hata ukalinajisi jina la Mungu wako; Mimi ndimi Bwana..

 

Zaburi 99:2-3 Bwana katika Sayuni ni mkuu, Naye ametukuka juu ya mataifa yote. Na walishukuru jina lake kuu la kuhofiwa; Ndiye mtakatifu.

 

Zaburi 111:9 Amewapelekea watu wake ukombozi, Ameamuru agano lake liwe la milele, Jina lake ni takatifu la kuogopwa.

 

Yeremia 14:9b Lakini wewe, Bwana, u katikati yetu, nasi tunaitwa kwa jina lako; usituache.

 

Mungu asiye onekana

Maandiko matakatifu yanatueleza kuwa Mungu hajawahi kuonekana kamwe kabisa na kwamba hakuna aliyewahi kuisikia sauti yake. Je, Mungu huyu ni yupi basi na ambaye anajulikana kwa jina lake tu?

Yohana 1:18a Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote;

 

Kutoka 33:20 inasema: Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi.

 

Yohana 5:37 Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona.

Hapa Kristo anamwelezea baba yake kuwa ni kumbe ambaye hajawahi kuonekana—na wala sura yake wala umbo lake—na wala sauti yake haijawahi kusikiwa.

 

Maandiko ya Mtume Paulo kwenye Agano Jipya anamwelezea kama ni Mungu “asiyeonekana”.

Wakolosai 1:15 naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.

 

1Timotheo 1:17 Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.

 

Waebrania 11:27 Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.

 

Mungu huyu ambaye hakuna mtu aliyewahi kumuona analo jina. Jina la Mungu huashiria tabia yake au jinsi alivyo. Jina la Mungu ni Eloa, au Yahova wa Majeshi. Wakati mwingine jina hili la Mungu hukosewa kuitwa, kwa jinsi watu wanavyomuita kuwa ni Yehova au Yahwe.

 

Je, ni kwa namna gani basi jina hili la Mungu linaweza kutumika au kutajwa bure au visivyo? Kitabu cha fasiri cha Young’s Analytical Concordance kinaelezea jinsi linavyoweza kutumiwa visivyo kama ifuatavyo:

·      Ubatili: Neno hili linatokana na lugha ya Kiebrania la hebel (Yer.10:3)

·      Bure, kwa kutangua-kutoka kwenye neno la Kiebrania  chinnam (Eze. 6:10)

·      Tupu, linalotokana na neno la Kiebrania la nabab (Ayubu11:11,12)

·      Pasipo Kitu, bure linalotokana na neno la Kiebrania rig (Zaburi 2:1; Yeremia 51:58)

·      Uwongo au Udanganyifu kutokana na neno sheqer (Kutoka 5:9)

·      Kuharibika au uharibifu, kutoka kwenye neno tohu (Isaya 45:18; sawa na Mwanzo 1:2; Yeremia 4:23)

·      Hasara au kisichofaa kutoka kwenye neno la Kiyunani mataios

 

Maneno haya yote yametafsiriwa kama kitu bure kwenye lugha ya Kiingereza, ila sisi tunajionea kutoka kwenye mtazamo wa kiroho kwamba kila moja ya maneno haya lina mwelekeo wenye maana na matendo. Neno linalochukua maana ya bure kwenye amri hii ya tatu, na kwa vyovyote vile, linatokana na neno tofauti la Kiebrania la shav au shawv, ambalo pia lilikuwa na maana ya udanganyifu na ambao ni ubatili. Kwenye kitabu cha fasiri cha Strong’s Hebrew Dictionary, neno hili limeandika shawv (SHD) 7723 ambayo maana yake ni uharibifu au maganjo, uovu, uharibifu, ibada ya sanamu, kutfaa, bure, uwongo mkubwa. Kama tulivyoona kwenye amri hii ya tatu tuntaona namna nyingi ambazo kwazo neno hili lina maanisha.

 

Jina la Mungu limeandikwa na sio kutajwa

Jina la Mungu lilikuwa na maana sana kwa Kiebrania. Baada ya kipindi cha utumwa wa Babeli kabila la Yuda na sehemu ya kabila la Lawi na Benyamin kwao walilichukulia jina la Mungu kuwa ni takatifu sana, ingawaje lilionekana limeandikwa mara kwa mara, bali halikutamkwa kabisa. Wakati msomaji wa Torati kwenye sinagogi alipofika kwenye jina hili “YHVH” alijinyenyekesha kwenye matamshi ya neno hili na kuliita “Adonai” ambayo maana yake ni Bwana (sawa na kutamka Yahova SHD 3068 na Yahovih SHD 3069 hapo chini).

 

Maandiko ya Kiebrania kama yalivyo mengineyo ya uandishi wa mkono yalitungwa kwa mtindo wa sarufi konsonati peke yake. Sarufi za vokali ziliwekwa kipindi kilichofuatia baadae na watu waliokuwa huenda wasioyajua mapokeo ya uandishi wa Kiebrania ambao walifanya mlolongongano wa alama ndogondgo zilizojulikana kama vokali ambazo ziliwekwa pande za juu, kuzungushia na chini ya uandishi wao wa konsonati, lakini haikuweza kabisa kuingiliana nazo. Kwa hiyo, vokali za neno Adonai (SHD 136) zilitolewa kutokana na maneno yaliyotokana na jina la Mungu, na vokali hizi zilisomwa. Na matokeo ya kufanya kwake hivyo, neno rutubisho la Yahovah limefanyika na kutokea (kwa vipindi vilivyo sawa na sahihi kwa zama mpya) na ambalo ndilo limewezesha kuwepo na kuandikwa jina la YHVH linalotokana na vokali zinazounda jina la Adonai. Jina hili limebadilishwa kwa takriban mara 134 na wanazuoni wa kundi lijulikanalo kama Sopherim (waandishi waliokuweko siku za marabi) na tunajua kipindi ambacho mabadiliko haya yalifanyika kwa kulizingatia jina lake la kale asilia. Pia tunajua kwamba kutokana na ugunduzi uliofanywa na wataalamu wa mambo kale kwamba jina la Mungu hapo kabla kwa ufupi liliitwa Yaho (sawa na iliyoandikwa kwenye kitabu cha J.B. Pritchard, kiitwacho The Ancient Near East (Mashariki ya Karibu ya Zama za Kale), Princeton, 1958, Toleo la 1, ukurasa wa 278-282). Kwa hiyo, sio sahihi jina hili kuandikwa au kuitwa Jah. Katika lugha ya Kiebrania hakuna herufi ya J na vokali yake imeachwa kwa makusudi na kimakosa kabisa kwenye uandishi wake, kama tunavyoona kutoka kwenye maandiko ya kale ya Hekaluni kwa herufi kubwa yaani Elephantine (soma Zaburi 68:4). Waomi wa siku hizi wanaandika Jahveh au Yahweh na haya ni makosa kabisa.

 

Wakati jina hili lilipoandikwa Yahovah (SHD 3068) basi kila lilipoandikwa hivyo lilitamkwa kama “Adonai,” na wakati Mungu alipotajwa kama Yahovih (SHD 3069) kuliandikwa hivyo. Wakati wote lilitamkwa “elohim” na waandishi waliokuja siku za baadae, na walifanya hivyo ili kuepukana na hisia au mabishano ya wanateolojia ya kutofautisha na sio kwa sababu nyingine yoyote. Mengi ya mapokeo haya yaliyokuja baadae yaliingizwa kwenye itikadi za imani ya kiyahudi zilizochukuliwa kutoka kwenye imani zenye asili ya Wababeloni, kipindi walichokuwa utumwani huko pamoja na dhana au imani za wapagani wa kale ambazo zilikataza kuyataja majina ya miungu yao kwa kuogopa kuichokoza au kuikasirisha, jambo lingalilowafanya kumpatiliza mtu atakayefanya tendo hilo la kulitaja jina lake (soma jarida la Ibrahimu: Maana ya Majina (Na. 240) [Abracadabra: The Meaning of Names (No. 240)].

 

Hata walipokuwa wanaliandika jina hili la Mungu walipokuwa wanazinukuu sheria za Mungu kwenye maandiko mbalimbali, waandishi walilazimika kuadhimsha au kuzishika shera na taratibu fulani fulani

 

·                  Alipaswa kuwa ameoga vizuri na awe msafi.

·                  Ni lazima awe amezaa mavazi yote yaliyochukuliwa kuwa matakatifu kwa Wayahudi.

·                  Alipaswa kujihadhari kuwa asiingize peni yake na kutumbukia hadi katikati wakati anapiliandika jina hili la Mungu.

·                  Ni lazima Mfalme amuelekeze anapokuwa analiandika jina hili la Mungu, na asichukue maneno yoyote mengine anayoyasikia au kuwaza moyoni mwake.

 

Inadaiwa kuwa taratibu hizi ziliingizwa au kuwekwa kwa kuwa walidhania kwamba zingezuia watu kulitaja jina la Mungu bure. Ni jambo lililodhahiri sana kwamba, kwa namna yeyote zingeathiri umuhimu uleule kama tunavyojionea kwanye dhana ya Majina ya kipagani, ambayo kwamba, iwapo kama utalijua jina utaweza kulihubiri au kulitetea na kulidhibiti. Mtazamo huu ni tofauti na kinyume kabisa na maana halisi ya amri hii iliyo kwenye Torati ya Mungu.

 

Biblia maarufu ya wwandishi maarufu Bullinger inayoitwa Bullinga’s Companion Bible (Nyongeza yake ya 32) ina orodha ya nyongeza hizi yanayolitaja jina la Adonai katika kumtaja Yahova na pia utendaji kazi wa elohim. Mtazamo wa jinsi ya kulitamka jina la Mungu sio kitu ambacho amri hii ya tatu inaliongelea au kinachomaanisha.

 

Mwandishi mwingine aitwaye R.J. Rushdoony [kwenye kitabu chake cha Chuo cha Torati au Sheria ya Biblia (The Institutes of Biblical Law)], ambacho kilichapishwa kwenye machapisho yaliyoitwa kama  Presbyterian  and Reformed Publishing Company, 1973, ukurasa wa (126) ambayo ilikuwa na maswali yafuatayo:

“Swali la112. Je, ninini kinachotakiwa kufanyika kwenye amri za tatu?”

“Jibu: Amri ya tatu inataka kwamba, jina la Mungu, wadhifa wake, haiba yake, amri zake, neno lake, sakramenti zake, kwenye maombi, viapo vyake, katika kupiga kura, katika kuapa, kazi zake, na mambo mengineyo yote na ambavyo kwavyo vinamfanya ajulikane kuwa ni mtakatifu na atumike kwa heshima yake kubwa na kutumika mawazoni, kwenye mawazoni, neno au uandishi, kwa taaluma takatifu ya kikuhani, na malumbano yasiyojibika, kwenye utukufu wa Mungu, na kwa faida zetu na za wengine.”

 

“Swali la 113. Je, kuna dhambi gani imekatazwa kwenye amri hii ya tatu?”

“Jibu: Dhambi zilizokatazwa kwenye amri hii ya tatu ni, kutolitumia jina la Mungu kinyume na inavyotakiwa, na tendo la kulidhalilisha kwa kulitumia kinyume na kijinga, au kulitumia bila maana au sababu ya maana, kulitumia visivyopasa, kulikufuru, kulitumia kwenye mambo ya ushirikina, au kulitumia kwenye mambo ya ulozi au kwa matendo yote ya kutumia cheo chake, wadhiwa wake, kuyatumia maandiko yake au aya na kazi zake kwa matumizi ya kukufuru, au kufanya maapizo, au katika kuweka nadhiri, viapo, utiifu au uadilifu, na kutimiliza kama kuna vitu vingine visivyo kwenye uadilifu, kwenye manung’uniko na migogoro, kwenye udadisi au nasaha, au kushindwa kutendea kazi, au kwa namna nyingine yoyote inayoligeuza au kupingana na neno lake, au sehemu nyingine iwayo yote, katika namna ya kukufuru, mabishano au kwenye maswali yasiyo na faida, kulitumia kinyume na kwa mambo yasiyo ya lazima au katika kuyatetea mafundisho ya uwongo, kulidharau,, kiumbe au kitu chochote kilichochini ya jina la Mungu, kulitumia kwa matumizi ya kiuchawi au kwa dhambi zozote zinazotokana na tama ya mwili na utendaji wake, au kwa matendo yoyote maovu, udanganyifu, kwa mpindisho au kwa namna nyingine yoyote inayopingana na kweli ya Mungu, neema na nyinginezo. Kuweka dhana ya nyadhifa kwenye mambo ya dini ni unafiki au ni kwa kwa namna nyingine twaweza kusema kwamba hatimayake ni kupelekea kwenye jambo la aibu au ni aibu kubwa”.

 

Huenda watu wengi hawajatilia maanani jambo au utendaji huu mkuu wa amri hii ya tatu ya Mungu. Tunajua kwamba Mungu anataka kushirikiana na mwanadamu. Na jinsi pekee ya uhusiano huu anaweza kusababisha mchanganyo ni kwa mtu kuwa na hali ya kujisalimisha kikamilifu kwa Mungu na kwa mapenzi yake, kwa kuwa na unyenyekevu kamilifu kwenye Amri zake. Mungu anapendezwa na unyenyekevu na sio sadaka. Na zaidi sana ni kwamba sheria hizi tulipewa kwa fainda yetu na kamwe sio mzigo zinapoadhimishwa kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

 

Tendo la kuyabadili matumizi ya jina la Mungu na kulitumia pasipo sababu na kimakosa yalianza nyakati za mjukuu wa Adamu aliyeitwa Enoshi, kwa mujibu wa ilivyoandikwa na kuonekana kwenye kitabu cha Mwanzo 4:26.

Mwanzo 4:26 inasema: Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la Bwana.

 

Uandishi wa neno hili kwenye tafsiri ya Kiingereza ya KJV inaficha kile ambacho kwakweli kinachoendelea, wakati kwenye tafsiri ya Biblia iitwayo Bullinger’s Companion Bible, Appendix 21 inatupa maana kusudiwa ya aya hii. Kwa mujibu wa fafanuzi za kale za Kiyahudi, zonaonyesha kwamba watu waliacha kuomba kwa kulitumia jina la Bwana (kwa mujibu wa kitabu cha Targum Onkelos) na pia walijifanyia vinyago na sanamu za kuchonga na kuziitia kwa jina la Neno la Bwana (kwa mujibu wa Targum Jonathan). Rashi anasema kulikuwa na aina ya kufuru katika kuliitia jina la Bwana. Kwa hiyo, Dabar Yahovah au Neno la Bwana lilikuwa ni jina linalomaanisha Mungu; na hii ndiyo kazi ya Yesu Kristo, akiwa ni Neno.

 

Ilijulikana vema kwamba katika siku za Enoshi (aliyekuwa miongoni mwa uzao wa Adamu) ndipo watu walianzisha aina ptotfu ya ibada kwa kulihusianisha jina la Mungu na viumbe vingine vya mbinguni. Inaaminika kuwa walianza kuiitia miungu yao kwa jina la Yahova. Ni tendo linalilinganishwa na mwanzo wa ibada ya sanamu tangu kipindi hiki. Jina Enoshi maana yake ni mtu goigoi, dhaifu, mgonjwa au asiyeweza kutibika na kupona. Kitabu cha Mwanzo ni kitabu kinachoelezea mwanzo au chanzo cha mambo yote. Katika siku hizi za Enoshi ndipo watu walipoanza kulitumia jina la Mungu vibaya. Inaaminika kuwa Henoko, ambaye alikuwa ni mtu wa saba katika uzao wa Adamu, alisimama kidete kuwakemea na kutoa unabii dhidi yao na dhidi ya matendo yao machafu na yenye kuchukiza (Yuda 14, 15). Kilamara Ibada za sanamu hupelekea kuligeuza jina la Mungu. Ni Shetani ndiye anayewavuvia watu wabadilishe namna ya ibada zisiendane na anavyotaka Mungu na badala yake zimlenge yeye.

 

Jinsi ya Kulitamka Jina la Mungu kwa Lugha ya Kiebrania

Kuna makundi fulani miongoni mwa ndugu wa Makanisa ya Mungu yanayotunza Sabato, ambao wanashikilia kuamini dhana ya kuwa ni muhimu sana unapolitaja jina la Mungu utumie lugha ya Kiebrania peyake na sio vinginevyo. Wanaamini hivyo kwa hoja yao kuijenga kwa kutoielewa au kuielewa kimakosa aya iliyoko kwenye kitabu cha Matendo ya 4:12.

Matendo 4:12 inasema: 12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo

 

Baadhi ya majina yaliyoaminika kutumiwa na jinsi ya kuyatamka na makanisa haya ni kama tunavyoyaorodheshwa hapa:

Ili kutamka jina, Mungu Aliye Juu Sana, wanatumia: YaHVah, Yahu Wey, Yahaweway, Yhwh.

Kwa Masihi, wanatumia: YaHVaHoshea, Yahushua, Yahshua, Yeshua.

 

Kulitaja “Jin takatifu zaidi), makundi haya kwanza wanatumia Yahweh na kwa Yeye Aliye Juu Sana, na hutumia jina Yahshua ili kumtaja Masihi.

 

Dhana iliyoko kwenye “majina matakatifu” inadai kwamba tunapaswa kulijua jina sahihi la Mungu na pia tuweze kulitamka vizuri—pamoja na kujua jinsi linavyoandikwa—ili tupate kuokolewa. Wazo hili linamdhalilisha Mwenyezi Mungu na kumfanyia dhihaka, na kumfanya aonekane kuwa hawezi kuwasiliana na wanadamu kwa lugha nyingine yoyote ila ni kwa Kiebrania tu, na wanasahau kabisa kuwa ni yeye Mungu ndiye aliyezigawanya lugha za wanadamu kwenye mnara wa Babeli. Dhana hii pia inapuuzia kilichoelezwa kwenye Isaya 28:11.

Isaya 28:11 inasema: La, bali kwa midomo ya watu wageni, na kwa lugha nyingine atasema na watu hawa;

 

Wazo na dhana hii ya kutumia “majina matakatifu” pia inashindwa kujua majina na vyeo mbalimbali yanayomwakilisha mtu ambaye hatimaye alijulikana kama Yesu Kristo, kama tunavyojionea kwenye Isaya 9:6.

Isaya 9:6 inasema: Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.  

 

Dhana halisi ya kifungu hiki inaweza kusomwa na kueleweka kwa namna mbalimbali. Kwenye tafsiri maarufu ya Septuagint (LXX), aya hii ya Isaya 9:6-8 inasomeka hivi:

Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mjumbe wa Shauri Kuu [Malaika wa Shauri Kuu] kwakuwa nitaleta amani kwa wafalme na afya kwake. 7 Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo.
8 Bwana alimpelekea Yakobo neno, likamfikilia Israeli. 

 

Andiko hili linasomeka moja kwa moja kama, Mshauri wa Mungu [el] Mkuu, wakati kwenye tafsiri ya LXX inasema Malaika wa Shauri Kuu, jambo ambalo linaeleweka vyema.

 

Jina Baba wa Milele haliwezi kueleweka na waamini Utatu au kwa walio kwenye dini ya Kiyahudi na limeandikwa kikamilifu sana kwenye tafsiri hii ya LXX. Maandiko ya Kiebrania yanahusisha kuwa Baba huyu wa Milele kuwa ni Masihi. Kwa mujibu wa Mtume Paulo, Tunajua kwamba inawezekana kuwa na mababa wengi sana mbinguni na duniani (Waefeso 3:14). Mtu anaweza kujitahidi kusoma kwa Kiebrania kuwa ni Baba wa Milele kwa kulipa mashiko jina hili, ila kwa kawaida halisomwi kwenye utendaji wa aya hizi. Mtaalamu wa fasiri maarufu aitwaye Soncino anaitafsiri aya hii kama ifuatavyo:

Mtoto amezaliwa kwa ajili yaetu,

Tumepewa mtoto,

Na uweza wa kifalme u mabegani mwake,

Na jina lake aianitwa

Pele-joez-el-gibbor-

Abdi-ad-sar-shalom

 

Kwa hiyo, mfumo mzima unaonekana kama ni jina lenye uweza lililotolewa na Mungu. Tafsiri hii ya Septuagint LXX, na ambayo imeandikwa kipindi cha karne kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, inaelewa kuwa mtu huyu angekuwa ni Malaika wa Agano la Kale aliyempa Musa Torati. Imani ya sasa ya Kiyahudi inajaribu kuupuuzia ukweli huu, na ndiyo maana kuona kwamba imani ya Kiyahudi ya marabi waliokuja baada ya kipindi cha Kikristo waliipuuza tafsiri hii ya Septuagint LXX. Tunajua kwamba majukumu haya mbalimbali yako na yanawakilisha yale yaliyoko kwenye aya ya 7b (aya ya 8 ya Septuagint LXX), inayosema: “Kwa kuwa wivu wa Bwana wa Majeshi ndiyo utakaofanya hivi.”

 

Dhana hii inayoupa ulazima wa kutumia “majina matakatifu” inaonyesha kupuuzia kile kilichoandikwa kwenye Maandiko Matakatifu kwenye Mathayo 1:21 (pia kwenye aya ya 23).

Mathayo 1:21 inasema: Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

 

Yesu alifanyika Mwokozi kwa uteule wake, baada ya kuishi maisha yasiyo na dhambi na kisha kuyatoa maisha yake yawe sadaka. Kuna Maandiko Matakatifu yanayoonyesha vizuri kwamba Mungu Baba yetu ni Mwokozi wetu halisi (Zaburi 106.21; na Isaya 60:16).

Yuda 25 inasema: Yeye aliye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu; utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo, na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina.

 

 (sawa na tulivyoandika kwenye jarida la Mungu Mwokozi Wetu (Na. 198) [God Our Saviour (No. 198)].

 

Mathayo 1:23 inasema: Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.

 

Mwna huyu wa Mungu, ambaye pia ni Masihi na Mwokozi aliyeruzukiwa na Mungu, alifanya pia kuwa ni Kuhani Mkuu mwenye Cheo sawa na kile cha Melkizedeki, na alifanika kuwa kuhani wetu Mkuu alipokuja kwa mara yake ya kwanza na atafanyika kuwa Mfalme wetu kipindi atakapokuja mara ya pili. Kumfanya Masihi awe na jina moja tu kwa Kiebrania kunavunja amri ya tatu, na ni sawa na kulitaja jina la Mungu bila sababu ya maana. Kunazuia makusudi ya Mungu na kuuzuia Mpango wa Mungu uliowekwa kwa kusudi la kuwaokoa watu wote.

 

Wakati Yesu alipoombwa na wanafunzi wake awafundishe jinsi ya kuomba (Luka 11:1-4), aliwafundisha kuyawakilisha au kuyapeleka maombi yao moja kwa moja kwa Baba. Mungu anatajwa hapa kama “Baba Yetu uliye Mbinguni.” Tunaon kwamba kamwe kristo hakuwaambia au kuwafundisha wanafunzi wake wafanye maombi yao kwa lugha ya Kienrania peke yake.

 

Tunaona pia kwamba maombi aliyoyafanya Yesu Kristo katika Yohana 17:1-26 aliyafanya kwa kumtaja Mungu kuwa ni “Baba.” Na kwenye Mathayo 27:46 tunaona kuwa Yeeu Kristo alipokuwa anasulibiwa mtini alimlilia Baba kwa lugha ya Kiaramu, ambayo ilikuwa ni ya kawaida na iliyozoeleka na wengi kwa kipindi kile akisema “Eloi, Eloi, Lama Sabakthani?” [(Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?) (alinukuu Maandiko Matakatifu ya Kiebrania)]. Tunaona kwamba wala hakuitumia lugha ya Kiebrania ili kumtaja Baba. Mtume Mathayo aliandika hivyo kwa kuwa alikuwepo pale wakati alipokuwa anasulibiwa na alimsikia akitamka hivyo. Yohana pia alikuwepo pale, na aliandika kwa kunukuu maneno aliyoyasema Kristo ya kuwa “Imekwisha.”

 

Kwa hiyo, Mungu ana majina mengi na majina haya yote yanapaswa kutukuzwa. Tendo la kuyataja au kuyatamka majina haya kwa lugha ya Kiebrania peke yake halifanikishi dhana ya Kulitukuza jina la Mungu. Majina wenyewe tu kama yalivyo yanafanya taswira au ashirio fulani. Majina haya yenyewe tu yanafanya uwakilisho wa mwana na Baba kuwa na cheo chenye mamlaka, ambayo inafanya sababu iliyowafanya Malaika walofanya mambo mbalimbali ya Mungu kipindi cha Agano la Kale walipewa majina ya Yahova. Lakini ni Mungu tu peke yake ndiye aliyekuwa na sifa na jina hili ya Yehova, Bwana wa Majeshi.

 

Kukufuru na kuyatumia vibaya Majina ya Mungu

Mwandishi wa Zaburi alielezea jinsi wajinga na maadui wa Israeli walivyolikufuru na kulitumia vibaya jina la Mungu (Zaburi 74:10-18). Ni watu waliochukuliwa mateka na kupelekwa mbali pasipokuwa na makosa na hatimaye wakakombolewa, ndiyo wanaosema. Watu wa Mungu walipelekwa utumwani na kulikufuru jina la Mungu. Kwa hiyo watu hawa watalijua jina lake na ya kwamba yeye ananena (Isaya 52:5; sawa na Warumi 2:24). Katika siku za Mwisho watu watalikufuru jina lake Mungu na watakataa kutubu na kumpa utukufu (Ufunuo 16:9, 11, 21).

 

Mfano wa dhairi katika kulitumia vibaya jina na mamlaka ya Mungu kwa kufanya viapo visivyomuhimu na kulikufu, unapatikana kwenye kitabu cha 1Wafalme 21:10-13 na Matendo 6:11. tunona kwamba Stefano hakuuliza haki waliyopewa baraza la kidini ya kumhukumu yeye kifo. Bali tunaona kwamba waliwaombea wote wasamehewe, kwakuwa walichukua hatua hiyo kwa ushahidi wa uwongo, kwamba alikuwa ameivunja amri hii ya tatu na ile ya tisa.

 

Tunaona pia kwamba Kristo alishitakiwa kwa makosa ya uwongo ya kukufuru (Mathayo 9:3; 26:65,66; Yohana 10:36). Tunaona pia kwamba aliitaja dhambi nyingine asiyoweza kuwsamehewa mtu ambayo ni ile ya kumkufuru Roho Mtakatifu (Mathayo 12:22-32; Marko 3:22-30). Hili ni jambo linalotatanisha kwa namna fulani. Roho Mtakatifu ni wa muhimu sana kwa wokovu wetu kwa mamlaka ya Mungu. Tendo la kushinwa kuujua umuhimu wa ukombozi na kushindwa kuzijua dhambi zake mtu ni kujidanganya kwa kiasi kikubwa sana na ndiko kumkufuru Roho Mtakatifu kunakoongelewa.

 

Kuwaheshimu wengine wanaolichukua Majina ya Mungu 

Mamlaka ya Mungu yanatuama kote kuwili, yaani ni kwa watawala wa kada zote mbili yaani wa kimwili na kiroho kama ilivyoagizwa au kuelekezwa.

Kutoka 22:28 inasema: Usimtukane Mungu, wala usimlaani mkuu wa watu wako.

 

Tendo la kutomtii na kumuasi elohim na watawala wa nchi fulani ni sawa na kukufuru huku kunakoelezwa hapa kwenye jina la Mungu. Tunajionea jambo hili zaidi hapo mbeleni. Kukufuru na kulikufuru jina la Mungu ni matendo yanayofanyika kwa namna nyingi kwenye Maandiko Matakatifu.

Zaburi 74:10 inasema:  Ee Mungu, mtesi atalaumu hata lini? Adui alidharau jina lako hata milele.

 

Zaburi 74:18 Ee Bwana, uyakumbuke hayo, adui amelaumu, Na watu wapumbavu wamelidharau jina lako.

 

Isaya 52:5-6 Basi sasa, nafanya nini hapa, asema Bwana, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema Bwana, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa. 6 Kwa hiyo watu wangu watalijua jina langu kwa hiyo watajua siku ile ya kuwa mimi ndimi ninenaye; tazama ni mimi.

 

Mfano wa ushahidi wa uwongo uliotolewa kwa faida ya udhalimu unaonekana kwenye tukio la Nabothi. Tukio hili linapingana ama linazivunja amri zote mbili, yaani ya tatu na ya tisa, kwa kuwa ni uvunjifu wa amri ya tisa kwa pale unapotokea ushahidi wa uwongo, na hivyo, kuikinzana na ya tatu ambayo hukumu ile ilitolewa kidhalimu sana.

1Wafalme 21:10-13 inasema: mkainue watu wawili, watu wasiofaa, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe. 11 Wale wazee wa mji wake, na walio wenye nguvu waliokaa mjini mwake, wakafanya kama Yezebeli alivyowaagiza, kama ilivyoandikwa katika nyaraka alizowapelekea. 12 Wakapiga mbiu ya watu kufunga, wakamweka Nabothi juu mbele ya watu. 13 Na hao watu wawili, watu wasiofaa, wakaingia, wakaketi mbele yake; wale watu wasiofaa wakamshuhudia Nabothi mbele ya watu, wakasema, Nabothi amemtukana Mungu na mfalme. Ndipo wakamchukua nje ya mji, wakampiga kwa mawe hata akafa.

Kwenye andiko hili tunaona jinsi Yezebeli alivyowaleta walalamikaji wa uwongo ili Mfalme Ahabu afanikishe jama yake ya kulichukua shamba la mizabibu la Nabothi.

Mfano ulio kwenye Agano la Jipya wa mashitaka ya uwongo unaonekana kwenye kitabu cha Matendo sura ya 6.

Matendo 6:8-13 inasema: Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu. 9 Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano; 10 lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye. 11 Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu. 12 Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza. 13 Wakasimamisha mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati.

Hapa waliwekwa mashahidi wa uwingo ili wamshitaki Stefano kwa kumsingizia kuwa walimsikia akikufuru. Mamlaka iliyokuwepo ilimhukumu auawe lakini walifanya hivyo kinakosa na waliyatumia vibaya mamlaka yao.

 

Na kama ultvyoona, kuwa walijaribu kumtia hatiani Kristo kwa namna hiyohiyo. Kwenye matukio karibu mengi yaliyoandikwa kwenye maandiko mbalimbali ya kale tunaona pia kwamba manabii waliotumwa kwa Israeli waliuawa na makuhani au manabii wa uwongo au na jamii iliyokuwepo katika kipindi kile. Na katika matukio mengi taifa limeenenda kweny kipindi cha utendadhambi kwa kuwa dini iliyokuweko kwenye jamii yenyewe ilikuwa na makosa ma kwa ujumla tunaweza kusema kwamba ilikuwa kwenya mazingira ya kuabudu sanamu.

Mathayo 9:1-7 inasema: Akapanda chomboni, akavuka, akafika mjini kwao. 2 Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako. 3 Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. 4 Naye Yesu, hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu? 5 Kwa maana rahisi ni lipi, ni kusema, Umesamehewa dhambi zako, au ni kusema, Ondoka, uende? 6 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako. 7 Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake.

 

Iwapo kama Jesu alikuwa ndiye Kristo, kwa hiyo asingeweza kusema neno la kufuru. Kuhani Mkuu alitabiri mwaka ule kwamba inampasa mmoja afe kwa ajili ya wengi. Alitegemea mtu huyo kuwa ni Kristo, nah ii ndiyo maana hasa ya kurarua vazi lake. Kuhani Mkuu hapaswi kamwe kulirarua vazi lake, lakini kile alichokifanya kilikuwa ni mfano unaoasihiria sawa na kulirarua vazi lake kwa jinsi alivyofanya hivyo, ilikuwa ni mfano pia wa kuuondoa ukuhani kutoka kwenye kabila la Lawi katika Yudea na kuupeleka kwa Melikizedeki katika Israeli.

Mathayo 26:63-66 inasema: Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu. 64 Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni. 65 Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake; 66 mwaonaje ninyi? Wakajibu, wakasema, Imempasa kuuawa.

 

Yesu Kristo alishitakiwa mashitaka ya uwongo kwamba amekufuru kwa kulikotokana na hali ya wasikilizaji wake ya kutoyajua Maandiko Matakatifu jinsi yanavyosema. Na wengi wa Wakristo wa leo wangeweza pia kumuua Kristo kwa kama angekuja kwao leo, angetoa mahubiri yanayotofautiana na vile wanavyotaka aseme kwa jinsi walivyoongozwa na kufanywa waamini. Kipindi zama kijulikanacho kama cha Zama za Kati angeweza hata kuchomwa kwenye kifaa maalumu cha mateso na wale waliokuwa wakiitwa Waariani washika Sabato, kutokana na jumbe zake za kwenye maandiko ya Agano jipya ya zama kale.

Yohana 10:34-36 inasema: Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe? 33 Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu. 34 Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? 35 Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka); 36 je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?

 

Ujumbe uliko kwenye maneno haya peke yake ungeweza kumfanya ahukumiwe kifo. Alikuwa anashutumiwa kuwa anafanya kazi na miujiza yake kwa kutumia nguvu za Belzebuli, aliyekuwa ni Bwana wa Warukao na Mungu wa Ekroni.

Mathayo 12:22-32 inasema:  Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona. 23 Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi? 24 Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo. 25 Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama. 26 Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje? 27 Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu. 28 Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. 29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake. 30 Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya. 31 Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa. 32 Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.

 

Yesu Kristo alifundisha kwamba tendo la kukufuriana mtu na mwenzake ni machukizo yanayoweza kusameheka lakini tendo la kumkufuru Roho Mtakatifu wa Mungu ni uovu sioweza kusameheka na unampelekea mtu kwenye hukumu ya mauti. Toba ndicho kitu kinachohitajika ili mtu aupate wokovu, na tendo la kuikiri dhambi na kujua umuhimu wa neema iletayo wokovu iliyo kwa Mungu kupitia kwa Roho wake Mtakatifu ndiyo kiini pekee cha wokovu. Adhabu ya mtu anayekufuru na asiyetubu ni kali kwa kweli.

Ufunuo 16:9,11,21 inasema:  Wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu. 11 wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao. 21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.

 

Tendo la kumkufuru Mungu kikwazo kikubwa cha toba. Dunia imeendesha mambo yake kwa kadiri ya zinavyosema sheria zake na mfumo wake kwa takriban kipindi cha miaka elfu sita na zaidi sasa. Wangeweza kuipunguza dunia hali isiyoweza kukalika na kumilikiwa na kubakia kuwa jangwa, lakini kamwe hawaoni umuhimu wa kufanya toba na kumpa Mungu utukufu na kuzishika amri zake. Wanalitumia jina lake pasipo maana kwa kujiwekea mfumo au utaratibu mbovu wa utawala (cf. Walawi 24:16).

 

Mungu hafanyi mchezo au masihara, bali anamaanisha kile anachokisema. Dunia na jumuia zake patakuwa ni mahala salama iwapo tu kama sheria hizi zitatendwa kikamilifu. Kanuni za Sheria zake Mungu haziwezi kutumika kwa mtindo bandia au kwa kuzifanya zifuatane na hali ya kimtondo ya kidunia. Mfumo na utaratibu wote wa Sheria za Mungu ni mfumo mkamilifu ambao umetuama kwenye mahusiano halisi ya kiroho na ambayo yametanguliza hali ya asili yake Mungu. Chanzo asili sio mfumo wa mahusiani adhimisho yanayoitwa matukio ya baadae, ni neno lililo kwenye hali ya wingi iliyoonekana kwenye hali asilia ya Mungu. Kanuni ya Sheria zake ni takatifu, za haki, njema, kamiilifu, na za kweli kwa kuwa ni mwenye sifa hizi zote. Tendo la kuzipindisha Sheria na ushuhuda wake ni sawa na kulitumia jina lake bure.

 

Maasi ya Kora kwenye kitabu cha Hesabu 16 kunatuonyesha jinsi ambavyo Mungu hataendela tu kuwa mvumilivu milele kwa wale wanaompinga na kumkufuru.

Hesabu 16:31-33 inasema:  Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka;32 nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote. 33Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni.

 

Tunaona hapa kwamba jina la Mungu na la mtikwa mafuta wake walikuwa wananenewa maneno mabaya. Mungu aliutumia mfano wake kuwafutilia mbali wale waasi ili iwe ni mfano wa wengine wote watakaokuwa wanamkufuru Mungu. Kukufuru ni zaidi ya kulitumia jina la Mungu na kulitumia kwa mambo yasiyopaswa, au kulidhalilisha au kulitumia kama kitu dhaifu kwa lugha za kiuasi zinazosemwa kinyume na Mungu na kanuni zake na wale wote wanaolifanyia kazi jina lake.

 

Nabii Yeremia alichukiwa na manabii wa Anathothi ambao walikuwa ni watu wanaotoka mahali alipotoka yeye pia. Kwa ujumla twaweza kusema kwamba ghasia zilifanyika kwenye nchi chini ya mfumo wake wa kimaongozi. Na katika siku za mwisho mfumo wa kikahaba wa kidini utakuwa imejiharibia wadhifa wake, na mahala pake na mfumo wa kidunia wa mnyama utamgeukia mwanamke huyu kahaba na kumuangamiza. Kwa kuwa mwanamke huyu kahaba amelitumia jina la Mungu Aliye Hai vibaya na kuliondolea heshima yake lililokuwa nayo (sawa na inavyosema Ufunuo 17:16).

 

Mtume Paulo na Torati

Mtume Paulo aliletwa mbele ya Kuhani Mkuu. Tendo hili linatupa fundisho la muhimu.

Matendo 23:1-5 inasema: Paulo akawakazia macho watu wa baraza, akasema, Ndugu zangu, mimi kwa dhamiri safi kabisa nimeishi mbele za Mungu hata leo hivi. 2 Kuhani Mkuu Anania akawaamuru wale waliosimama karibu naye wampige kinywa chake. 3 Ndipo Paulo akamwambia, Mungu atakupiga wewe, ukuta uliopakwa chokaa. Wewe umeketi kunihukumu sawasawa na sheria, nawe unaamuru nipigwe kinyume cha sheria? 4 Wale waliosimama karibu wakasema, Je! Unamtukana Kuhani Mkuu wa Mungu? 5 Paulo akasema, Sikujua, ndugu zangu, ya kuwa yeye ni Kuhani Mkuu; maana imeandikwa, Usimnenee mabaya mkuu wa watu wako.

 

Je, ni Shera gani hiyo iliyoandikwa kutomnenea mabaya liwali au mkuu wa watu ama kiongozi? (Ni kwenye Kutoka 22:28).

 

Mtume Paulo aliijua sheria hii. Alifundishwa torati akiwa Farisayo na Gemalieli (soma Matendo 5:34).

Matendo 22:3 Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi;

 

Mtume Paulo hakuwa Myahudi, kwa kweli yeye alikuwa ni Mbenyamini (Warumi 11:1) wa kabila la Benyamini na sio Yuda, lakini neno Myahudi linalotumika hapa lina maana ya kijeneriki zaidi ya kabila. Musa pia hakuwa Myahudi, bali anakuwa na uhusiano na kabila la Lawi. Kuhani Mkuu pia alikuwa ni Mlawi na pia hakuwa Myahudi, na wala hakuwa kiongozi wa kabila la Yuda na Benyamini, na pia kwa kabila ya Lawi, na hata hivyo, maongozi ya Kuhani Mkuu aliyekuwa wa kabila la Lawi hayakuweza kabisa kufanywa baada ya kuangamizwa ka Hekalu na kutawanyika kwao.

 

Mtume Paulo alijua kile alichokuwa amekifanya na mara tu baada ya kuligundua kuwa amemnenea mabaya Kuhani Mkuu Anasi, na kwamba amemnenea vibaya mkuu wa watu au mtu aliyepewa mamlaka na Mungu, tendo ambalo limekatazwa kwenye torati (Kutoka 22:28).

 

Hatimaye Mtume Paulo analiandikia Kanisa la Rumi, kwenye Warumi 13:1a akisema: “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu” au kama inavyosema fasiri ya Agano Jipya ya toleo la the Concordant Literal New Testament) ambayo inasema hivi:

Warumi 13:1-2 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. 2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.

 

Makatazo ya Mungu ni Amri za Mungu zilizoandikwa kwenye kitabu cha Kutoka 22:28. Amri hii ni ngumu sana kwa mtu kuiishia kwa sababu ya matumizi mabaya ya mamlaka yaliyoko, ni kama alivyosema mtume Paulo hapa. Vi jambo lililo dhahiri kwamba katika siku zijazo watu wote watajaribiwa kwa namna ya sheria hii kwa jinsi tunavyoelekea kwenye hali hii ya matumizi mabaya ya mamlaka na nguvu za utawala.

 

Kujifunga kwa kiapo

Mithali 19:28 inasema: Shahidi asiyefaa kitu hudhihaki hukumu, Na vinywa vya wasio haki humeza uovu.

 

“Msingi wa kile kinachoitwa utaratibu wa kisheria unahusisha kile kinachoitwa mabishano ya kienyeji ni kitu kilicho wazi sana kwenye amri hii ya tatu na ingeweza kuchukuliwa kama mjadala kuhusu uhalifu.

 

[Hii ni kwa mujubu wa Ingram, kwenye kitabu chake cha Ulimwengu Chini ya Torati ya Mungu, ukurasa wa 46 (World Under God’s Law, page 46)].

 

Kiapo cha kuingia kwenye wadhifa, kiitwacho kama ushuhuda wa uaminifu, au ithibitisho katika jamii ni neno lililozoeleka kwenye jamii likijulikana kama kiapo cha uaminifu na utii na ukweli, na mfumo wake mzima uliotuama kwenye aina yoyote ya maneno na sio matendo ya maelekezo yaliyo kwenye dhana ya usafi au ukweli unaotokana na viapo (au uthibitisho ambao kiapo kinapo kinaonekana kama tendo hili la kula kiapo linapingana na maelekezo ya Kristo). Mahali pasipo na kikomo au kanuni za ukweli mahali ambapo mtu anaweza kuiona kama kiapo ambacho hakikusudii kutuama kwenye maneno yao, na ambako viongozi na watawala wanaoiwakilisha jamii wanaifuata. Mahala pasipo na hofu ya Mungu ndipo utakatifu wa kiapo hutoweka na misingi ya jamii huyumba kutoka kwenye ukweli na kuw auwongo.

 

Kwenye miaka ya mwanzoni, kiapo cha Ufalme au cha ofisi ya Urais (na kila kiapo cha kuchukua wadhifa ofisini) vilichukuliwa kabisa kwamba vilikuwa vinatokana na amri hii ya tatu na kwa kweli ilikuwa inaivunja. Kwa kula kiapo mtu aliahidi kuiheshimu kwa neno lake na maelekezo yake hasa kwa kuwa Mungu ni mwaminifu kwenye neno lake. Kwa mujibu wa kiapo cha kuwekwa kwenye ofisi, kama maofisa wa jamii wameshindwa walichukuliwa kama wamezitengua hukumu za Mungu na laana ya torati juu yao. Kwenye jamii zetu za leo kuna hali ya kutotilia maanani masuala ya viapo kwa kiasi kikubwa sana. Na imechukuliwa kwamba tendo hili la ulaji wa kiapo ni kama suala la sherehe tu, au ni jambo la kawaida na la mazoea na ambalo kwamba linaweza kuvumilika. Watu wanakula kiapo wakitumia Biblia ambayo hawajaisoma na kuelewa vema au wanakuwa hawaielewi, na la kusikitisha zaidi ni kwamba wengi wao wanakuwa hawaiamini pia wala hawaamini matokeo mabaya ya kufanya hivyo.

 

Tendo la kudharau kiapo lilichukuliwa kama machukizo makuu sana katika siku za kale. Na ili mtu ashuhudie kiapo kile kwa sababu njema au mbaya mahali popote na ili kusichukuliwe hatua, kulihtajika itilewa sadaka ya upatanisho (Walawi 5:4-7). Kiapo cha uwongo kilikuwa ni kosa na machukizo (assault) kwa maisha ya jamii nzima husika. Umuhimu wa kuchukia kiapo cha uwongo umeelezwa kwenye Zaburi 109.

 Zaburi 109:17-18 inasema: Naye alipenda kulaani, nako kukampata. Hakupendezwa na kubariki, kukawa mbali naye, 18 Alijivika laana kana kwamba ni vazi lake. Ikamwingilia moyoni kama maji, Na kama mafuta mifupani mwake.

Kutoka 23:1 inasema: Usivumishe habari za uongo; usitie mkono wako pamoja na mwovu, kuwa shahidi wa udhalimu.

Namna sahihi ya kula kiapo imeelekezwa kwenye kitabu chaKutoka 22

Kutoka 22:10-11 inasema: Mtu akimpa mwenziwe punda, au ng'ombe, au kondoo, au mnyama ye yote, ili amtunzie; yule mnyama akafa, au akaumia, au akachukuliwa mtu asione; 11 patakuwa na kiapo cha Bwana katikati ya watu hao wawili, kwamba alipeleka mkono wake kutwaa mali ya mwenziwe, na mwenyewe atakubali hayo, wala hatalipa.

Maana ya neno kukitunza iliyoandikwa kwenye aya ya 10 ni kule kinakojulikana kama kukitunza kiusalama wakati jirani anapokuwa ameondoka. Mchakato mzima wa kula kiapo unatakiwa kuandaliwa ili kiapo kifanyike ili kufikia ufumuzi kwa jamo linalobishaniwa kati ya watwawili, wakati kwamba neno linalobishaniwa hakuna aliyeliona.  

Zekaria 8:16-17 inasema: Haya ndiyo mtakayoyatenda; kila mtu na aseme kweli na jirani yake; hukumuni kweli na hukumu ya amani malangoni mwenu; 17 wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema Bwana.

 

Kutokula kiapo kabisa

Je, Yesu Kristo alikuwa na maana gani kwenye mahubiri yake ya Mlimani alipowaambia wanafunzi wake, “Swear not at all”? na kwa vile alikuwa ndio kwanza tu anawaambia kuwa yeye hakuja kuitangua torati. Je, kwa kusema hivi alikuwa anabadili sehemu ya torati hii hapa?

Mathayo 5:34-37 inasema: lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; 35 wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. 36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu

Maneno yaliyotumika kwenye tafsiri ya Mfalme Yakobo (KJV) yanasema “Usiape kabisa” sio tafsiri nzuri kutoka kwenye tafsiri halisi ya kiyunani.

Tafsiri ya Agano Jipya iitwayo The Concordant Literal New Testament inaelezea kile alichokikusudia Yesu Kristo, na kuelezea kwa uwazi zaidi kwa kuandika kama ifuatavyo:

Mathayo 5:33-37 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako; 34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; 35 wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. 36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.

Kuna aina mbili katika aya hizi, sehemu ya kwanza inaithibitishba sheria ya kiapo, na sehemu ya pili inakataza kuapa kwa sababu zisizo na umuhimu (a frivolous manner) au kula kiapo kwa hali ya mzaha. Sisi sote tumewasikia watu wakisema kwamba “Waseme kweli.” Je, hii inamaana kuwa walikuwa hawasemi kweli hapo kabla? Au wanajaribu kutilia mkazo kwa kusema “Mama yangu na awe kipofu iwapo kama ninalolisema sio neno la kweli!”

Jamii katika siku za Kristo walikuwa wanatumia ardhi, Yerusalemu au vichwa vyao ili kujaribu kutilia mkazo kwenye maneno yao. Na ndivyo ilivyo hata watu wengi leo, wanatumia maneno ya laana ili kutilia mkazo mambo yao fulani lakini Kristo alituambia ifuatavyo: “Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo;

Viongozi haohao wa kanisa wamewafundisha watu kuwa wasiape wanapokuwa mahakamani wakiyachukulia maneno haya, “msiape kabisa” all”. Hii ni tafsiri potofu ya maneno haya. Hata hivyo, mtume Paulo alipopelekwa mahakamani aliapa na ilikuwa sahihi kufanya hivyo.

 

Ruthu alilitumia jina la Mungu katika kujitangaza wakati alipojitoa kwa Naomi.

Ruthu 1:16-17 Naye Ruthu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu; 17 Pale utakapokufa nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami.

 

Sahihi, na kwa mfano hii tunapaswa hata sisi kufanya vivyohivyo.

 

Mambo saba anayoyachukia Mungu

Mithali 6:16-19 inasema: Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. 17 Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; 18 Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; 19 Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.

 

Mambo ya Walawi 5:1 inasema: Na mtu awaye yote akifanya dhambi, kwa kuwa ameisikia sauti yenye kuapisha, naye akawa ni shahidi, kwamba aliona au kujua, asipolifunua neno lile, ndipo atakapochukua uovu wake mwenyewe;

 

Mambo ya Walawi 5:4-5 inasema: au, kama mtu akijiapisha, kwa kutamka haraka kwa midomo yake, kutenda uovu, au kutenda mema, neno lo lote mtu atakalolitamka kwa kiapo pasipo kufikiri, na neno hilo likamfichamania; hapo atakapolijua, ndipo atakapokuwa na hatia katika mambo hayo mojawapo; 5 kisha itakuwa, hapo atakapokuwa na hatia katika mambo hayo mojawapo, ndipo utakapoliungama jambo hilo alilolikosa;

 

Jambo jema la kulifanya

Mambo ya Walawi 5:6-13 inasema: naye atamletea Bwana sadaka yake ya hatia kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, mwana-kondoo wa kike, au mbuzi mke, kutoka katika kundi lake, kuwa ni sadaka ya dhambi; kisha kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake. 7 Lakini asipomweza mwana-kondoo, ndipo atakapomletea Bwana hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kuwa ni sadaka yake ya hatia ya jambo hilo alilolikosa; mmoja wa hao ndege kwa sadaka ya dhambi, na wa pili kwa sadaka ya kuteketezwa. 8 Naye atawaleta kwa kuhani, atakayemsongeza kwanza yule wa sadaka ya dhambi, naye atamkongonyoa kichwa shingoni mwake, lakini asimpasue vipande viwili; 9 kisha baadhi ya damu ya hiyo sadaka ya dhambi atainyunyiza katika ubavu wa madhabahu; na damu iliyosalia itachuruzishwa hapo chini ya madhabahu; ni sadaka ya dhambi. 10 Kisha huyo ndege wa pili atamsongeza kuwa sadaka ya kuteketezwa, sawasawa na sheria; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, naye atasamehewa. 11 Lakini asipowaweza hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, ndipo hapo atakapoleta matoleo yake kwa ajili ya neno hilo alilolikosa, sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba, kuwa sadaka yake ya dhambi; asitie mafuta juu yake, wala ubani usitiwe juu yake; maana, ni sadaka ya dhambi. 12 Naye atamletea kuhani, na kuhani atatwaa konzi yake ya huo unga kuwa ukumbusho wake, na kuuteketeza juu ya madhabahu, juu ya sadaka zilizosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto; ni sadaka ya dhambi. 13 Na huyo kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake ambayo katika mambo hayo mojawapo amefanya dhambi, naye atasamehewa; na unga uliosalia utakuwa wa kuhani, kama hiyo sadaka ya unga ilivyokuwa.

 

Tendo la kuvunja amri zilizo kwenye Torati na huku ukizijua sio jambo linaloweza kusamaheka, sawa na tendo la kutomtimizia Bwana nyapo zako ulizoziweka kwa Mungu, pia hakuna udhuru utakaokubalika kumsamehe mtu wa namna hii.

Kumbukumbu la Torati 23:21-23 inasema: Utakapoweka nadhiri kwa Bwana, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako. 22 Lakini ukijizuia usiweke nadhiri, haitakuwa dhambi kwako. 23 Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri Bwana, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako.

 

Kuna sheria na maelekezo yaliyowekwa kuhusu familia na mkuu wa familia kuhusu ulaji wa kiapo kama ifuayavyo hapa chini.

Hesabu 30:1-16 inasema: Kisha Musa akanena na wale vichwa vya kabila za wana wa Israeli, na kuwaambia, Neno hili ndilo aliloliagiza Bwana. 2 Mtu atakapomwekea Bwana nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake. 3 Tena mtu mke atakapomwekea Bwana nadhiri, na kufunga nafsi yake kwa kifungo, naye aketi katika nyumba ya babaye, katika ujana wake; 4 babaye naye akasikia nadhiri yake, na kile kifungo chake alichofungia nafsi yake, na babaye akamnyamazia; ndipo nadhiri zake zote zitathibitika, na kila kifungo alichofungia nafsi yake kitathibitika. 5 Lakini kama huyo babaye akimkataza siku hiyo aliyosikia; nadhiri zake ziwazo zote, wala vifungo vyake alivyoifungia nafsi yake havitathibitika; na Bwana atamsamehe, kwa kuwa babaye alimkataza. 6 Tena kama amekwisha kuolewa na mume, wakati huo wa nadhiri zake, au wa neno hilo alilolitamka kwa midomo yake pasipo kufikiri, alilojifungia; 7 na mumewe akasikia, naye akamnyamazia siku hiyo aliyosikia neno hilo; ndipo nadhiri zake zitathibitika, na vile vifungo ambavyo ameifunga nafsi yake vitathibitika. 8 Lakini kama mumewe akimkataza siku hiyo aliyolisikia; ndipo ataitangua nadhiri yake iliyo juu yake na neno alilolitamka kwa midomo yake pasipo kufikiri, alilojifungia; na Bwana atamsamehe 9 Lakini nadhiri ya mjane, au ya mwanamke aliyeachishwa mume, kila neno ambalo ameifunga nafsi yake kwalo, litathibitika juu yake. 10 Tena kama aliweka nadhiri nyumbani mwa mumewe, au kama aliifunga nafsi yake kwa kifungo pamoja na kiapo, 11 na mumewe alisikia akamnyamazia, wala hakumkataza; ndipo nadhiri zake zote zitathibitika, na kila kifungo alichojifungia kitathibitika. 12 Lakini kama mumewe alizibatilisha na kuzitangua siku hiyo aliyozisikia, ndipo kila neno lililotoka midomoni mwake katika hizo nadhiri zake, au katika kile kifungo cha nafsi yake, halitathibitika; huyo mumewe amezitangua; na Bwana atamsamehe. 13 Kila nadhiri, na kila kiapo kifungacho, ili kuitaabisha nafsi ya mwanamke mumewe aweza kuthibitisha, au mumewe aweza kutangua. 14 Lakini mumewe akimnyamazia mkewe kabisa siku hata siku ndipo azithibitisha nadhiri zote za mkewe, au vifungo vyake vyote vilivyo juu yake; yeye amezithibitisha, kwa kuwa alimnyamazia mkewe siku hiyo aliyozisikia nadhiri zake. 15 Lakini akizibatilisha na kuzitangua baada ya kuzisikia; ndipo yeye atachukua uovu wa mkewe. 16 Hizi ndizo amri, ambazo Bwana alimwagiza Musa, kati ya mtu mume na mkewe, kati ya baba na binti yake, katika ujana wake, ali nyumbani mwa babaye.

 

Utakatifu wa Sadaka au Dhabihu

Mambo ya Walawi 22:1-33 inasema: Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Nena na Haruni na wanawe, ili wajitenge wenyewe na vitu vitakatifu vya wana wa Israeli ambavyo wanitakasia mimi, tena kwamba wasilinajisi jina langu takatifu; mimi ndimi Bwana. 3 Waambie, Mtu ye yote wa kizazi chenu chote katika vizazi vyenu, atakayevikaribia vile vitu vitakatifu, ambavyo wana wa Israeli wamtakasia Bwana, naye ana unajisi, mtu huyo atakatiliwa mbali asiwe mbele zangu; mimi ndimi Bwana. 4 Mtu ye yote wa kizazi cha Haruni aliye mwenye ukoma, au mwenye kisonono; yeye asile katika vitu vitakatifu, hata atakapokuwa safi. Tena mtu awaye yote atakayekinusa kitu kilicho na unajisi kwa sababu ya wafu, au mtu ambaye shahawa humtoka; 5 au mtu amgusaye mnyama atambaaye, wa kumpatia unajisi, au kwamba amgusa mtu wa kumpatia unajisi, kwa unajisi wo wote alio nao; 6 huyo mtu atakayegusa kitu cho chote namna hiyo atakuwa najisi hata jioni, naye hatakula katika vitu vitakatifu, asipooga mwili wake majini. 7 Jua likiisha kuchwa atakuwa safi; kisha baadaye atakula katika vitu vitakatifu, maana ni chakula chake. 8 Nyamafu au mnyama aliyeraruliwa na wanyama asile, asijitie unajisi kwa hiyo nyama; mimi ndimi Bwana. 9 Basi kwa hiyo watayashika mausia yangu, wasije wakachukua dhambi kwa hayo, nao wakafa humo, wakiyanajisi; mimi ndimi Bwana niwatakasaye. 10 Mgeni awaye yote asile katika kitu kitakatifu; mgeni wa kuhani akaaye kwake, au mtumishi aliyeajiriwa, asile katika kitu kitakatifu. 11 Lakini kwamba kuhani akinunua mtu ye yote, kwa kumnunua kwa fedha zake, yeye atakula katika hicho; na hao waliozaliwa nyumbani mwake watakula katika chakula chake. 12 Na binti ya kuhani kwamba ameolewa na mgeni, asile katika sadaka ya kuinuliwa katika vitu vile vitakatifu. 13 Lakini kwamba binti ya kuhani ni mjane, au kwamba ameachwa na mumewe, wala hana mtoto, kisha amerudi na kuketi katika nyumba ya baba yake, kama vile katika ujana wake, yeye atakula katika chakula cha baba yake; lakini mgeni awaye yote asile katika chakula hicho. 14 Tena kama mtu ye yote akila katika kitu kilicho kitakatifu pasipo kukijua, ndipo ataongeza sehemu ya tano juu ya kitu hicho, na kumpa kuhani kitu hicho kitakatifu. 15 Wala wasivinajisi vitu vitakatifu vya wana wa Israeli, wavisongezavyo kwa Bwana; 16 hata wakawatwika ule uovu uletao hatia, hapo walapo vitu vyao vitakatifu; kwa kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye. 17 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 18 Nena na Haruni na wanawe, na wana wa israeli wote, uwaambie, Mtu ye yote wa nyumba ya Israeli, au wa wageni walio katika Israeli, atakayetoa matoleo yake, kama ni nadhiri zao mojawapo, au kama ni sadaka yo yote ya hiari, watakayomtolea Bwana kuwa sadaka ya kuteketezwa; 19 ili mpate kukubaliwa, mtaleta mume mkamilifu, katika ng'ombe, au katika kondoo, au katika mbuzi. 20 Lakini mnyama ye yote aliye na kilema msimtoe; kwa kuwa hatakubaliwa kwa ajili yenu. 21 Na mtu awaye yote atakayemtolea Bwana dhabihu katika sadaka za amani, ili kuondoa nadhiri, au sadaka ya moyo wa kupenda, katika ng'ombe, au katika kondoo, atakuwa mkamilifu, apate kukubaliwa; pasiwe na kilema ndani yake cho chote. 22 Kipofu, au aliyevunjika mahali, au kiwete au aliye na vidonda, au aliye na upele, au aliye na kikoko, hamtamtolea Bwana wanyama hao, wala msiwasongeze kwa Bwana kwa njia ya moto juu ya madhabahu. 23 Ng'ombe, au mwana-kondoo aliye na kitu kilichozidi, au aliyepungukiwa na kitu katika vitu vya mwilini mwake, mna ruhusa kutoa kuwa sadaka ya moyo wa kupenda; lakini kwa ajili ya nadhiri hatakubaliwa. 24 Mnyama aliyeumia mapumbu yake, au kusetwa, au kuvunjwa, au kukatwa, msimtolee Bwana; wala msifanye hivi katika nchi yenu. 25 Wala msisongeze chakula cha Mungu wenu katika wanyama hao mmojawapo kitokacho mkononi mwa mgeni; kwa sababu uharibifu wao u ndani yao, wana kilema ndani yao; hawatakubaliwa kwa ajili yenu. 26 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 27 Hapo ng'ombe, au kondoo, au mbuzi, akizaliwa, atakuwa pamoja na mamaye muda wa siku saba; na siku ya nane na baadaye atakubaliwa kuwa ni sadaka ya kutolewa kwa Bwana kwa njia ya moto. 28 Tena kama ni ng'ombe, au kama ni kondoo, msimchinje huyo na mwanawe wote wawili kwa siku moja. 29 Tena mtakapomchinjia Bwana dhabihu ya shukrani, mtamchinja ili mpate kukubaliwa. 30 Italiwa siku iyo hiyo; msisaze kitu chake hata asubuhi; mimi ndimi Bwana. 31 Kwa hiyo mtayashika maagizo yangu, na kuyafanya; mimi ndimi Bwana. 32 Wala msilinajisi jina langu takatifu; lakini nitatakaswa mimi katika wana wa Israeli; mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi, 33 niliyewaleta mtoke nchi ya Misri, ili niwe Mungu wenu; mimi ndimi Bwana.

 

Sadaka zote ni takatifu kwa Bwana, na sadaka kuinajisi sadaka ni tendo lile la kulitaja jina la Mungu bure. Na hiki ndicha hasa chanzo zha malalamiko: Mungu anawaambia watu wake kwamba wanadai kuwa meza yake imenajisika, kwa kuwa sisi tu wenyedhambi na ni watu tuliokombolewa na Mungu tukiwa kama sadaka iliyohai.

 

Matumizi ya Ulimi

Mtazamo wa amri hii ya tatu unatuama kwenye kile tunachokisema. Maneno yetu yanadhihirisha kile tunachokifikiria au tunachowaza, wakati kwamba mawazo yetu huongoza matendo yetu. Kanuni hii imetolewa na Kristo kwenye Injili ya Luka 6:43-45.

Luka 6:43-45 inasema: Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; 44 kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. 45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.

 

Mtume Paulo anauelezea moyo mbaya uli ndani ya mwanadamu kwa wapagani waliokuwa huko Rumi. Anaionyesha matendo yatokanayo na asili ya mwili wa mwanadamu aliyeamua kujitenga na kuwa kinyume na Mungu.

Warumi 3:10-18 inasema: Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. 11 Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. 12 Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja. 13 Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao. 14 Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. 15 Miguu yao ina mbio kumwaga damu. 16 Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao. 17 Wala njia ya amani hawakuijua. 18 Kumcha Mungu hakupo machoni pao.

 

Aya hizi zinawaelezea wale wasiozitii na kuzipenda Amri na Sheria za Mungu.

 

Ndugu wa karibu sana wa Kristo aliyeitwa Yakobo na mchungaji wa Kanisa la Yerusalemu na ambaye ndiye alikuwa msemaji wa makao makuu ya kanisa kama alivyoandikwa kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume 15, alikuwa pia na mengi sana ya kuongea kuhusu matumizi ya ulimi.

Yakobo 1:26 inasema: Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai

 

Yakobo 2:5-7 inasema: Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao? 6 Bali ninyi mmemvunjia heshima maskini. Je! Matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya viti vya hukumu? 7 Hawalitukani jina lile zuri mliloitwa?

 

Yakobo 3:5-9 inasema: Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana. 6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum. 7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu. 8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti. 9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.

 

Yakobo 4:11-12 inasema: Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu. 12 Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine?

 

1Petro 3:10 inasema: Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila.

 

Tunayaona Maandiko haya Matakatifu yakisema kwamba Mungu anawataka watumishi wake wa kweli wawe na ulimi safi (sawa na ilivyoandikwa pia kwenye Tito 2:7-8). Tunahukumiwa kwa maneno tunayoyassema. “Kutokana na yaliyoujaza moyo wa mtu, ndyo yatakayomtoka mtu ulimini mwake”  

 

Maombi

Kumuomba Mungu kwa namna iliyo sahihi kulijulikana tangia siku za kale za kwanza. Hata hivyo maombi yalitumika pia kama namna ya kumshawishi Mungu. Hali hii ya kushawishi kiulaghai kulikofanywa ni tendo la kupoteza muda na kunapingana na amri hii ya tatu. Viongozi wa kanisa wamekuwa wanatoa wito kufunga saumu na kuomba wakati mashirika yao yanapokumbwa na matatizo ya kiuchumi au kifedha; na maombi yamekuwa wakifanywa ili kuwaombea viongozi wa Kanisa ambao wanawaongoza waumini wao kwenye upotevu na ukengeufu.

Isaya 1:15 inasema: Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia;

 

Unabii wa Uwongo

Mungu alitumia unabii na manabii ili kuwaonya watu kwa ajili ya matukio yanayokuja mbele yao, na anapowataka watu waliomuasi watubu, na kuwaonyesha yanayotaka kutokea au kuwapata Israeli kwa ajili ya kuzivunja kwao amri na Torati yake.

 

Unabii wa uwongo umekuwa ni mtego wa kila mara kwa watu wa Mungu. Tukio la Mfalme Balaki wa Moabu la kumuomba Balaamu awalaani kwa laana Israeli kwenye kitabu cha Hesabu sura ya 22 linaonyesha jinsi Mungu anavyowaona hawa manabii wa uwongo. Ilimlazimu Mungu amtumie punda ili aongee na Balaamu kama njia iliyoonekana ingemshangaza na kukamata hisia zake. Kutoai mabashiri ya uwongo kwa kulitumia jina la Mwenyezi Mungu ni machukizo makuu na ni ubatili mkuu pia. Tendo la kujikinai kwa kutoa mawazo ya uwongo au kuyatafsiri vibaya Maandiko Matakatifu kumekuwa ni tanzi kubwa kwa Kanisa la Mungu katika kipindi zama cha karne ya ishirini.

 

Ulimwengu wa Wakristo wanaojiita wenye Itikadi Kali au ya Kiorthodoxi umegubikwa na mafundisho waliyotungwa na wanadamu na ambayo yanapingana na kuivunja mari hii ya tatu na kuzipinga Sheria na Torati ya Mungu. Tendo lao la kumuomba mtu aliyebandikwa jina la Mariamu mama wa Mungu na kumfanyiza Kristo bandia na wa uwongo ni jambo lenye ibatili mkubwa—na mtindi wao wa maombi ya kurudia rudia ni ubatili mkubwa. Matumizi ya vishada vya shanga vyenye mzunguko-duara kufanyia maombi yote ni ubatili mkubwa pia na imekatazwa na Biblia (Mathayo 6:7). Tendo la kukusanyika maelfu ya watu mahali pamoja kwenye viwanja vya mpira na kuwahubiria ili eti wamkubali na kumpokea Kristo ni ubatili mkubwa pia—hii ni kulitumia jina la Mungu Aliye hai bure.

 

Kuna jambo moja pia ambalo tunapaswa kulijua nalo ni kwamba; nyimbo nyingi zilizotungwa hivi karibuni na ambazo zinaonekana au kujulikana kuwa ni za kisasa.na kutumika kanisani wakati wa ibada, na hususani zile za mtindo wa “Mimi kama nilivyo” au “Mniache kama nilivyo” zinaivunja amri hii ya tatu. Zinaonyesha kutojua umuhimu au kutotilia maanani na kuonyesha kuwa hakuna haja ya kufanya toba, bali ni kutimiliza dhana ya makutaniko ya waovu (Amosi 8:3), ambao walikuwa wanatabiri ili kujaliza mahala wapapofanyia ibada. .

 

Mahubiri yanayofanywa siku za Jumapili asubuhi nayayoitwa “mahubiri ya kumhubiri Yesu” yanalenga jambo hilihili moja la kulitumia jina la Bwana bure. Yesu Kristo wa ukweli wa Agano Jipya anasema kwenye Mathayo 15:9 na Marko 7:7 hivi:

Nao waniabudu (Kwa Kiyunani-adore) bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu,

 

Namna yote ya kile wanachokiita Muziki wa Injili pamoja na ujumbe wake wanaokazia kuutoa wa “Yatoe maisha na moyo wako kwa Bwana” na mafundisho yao ya uwongo ya kwenda mbinguni, au mafundisho wanayowaambia watu kuwa “utakwenda motoni na kuungua milele” vyote hivi havinamsingi na wala hayatoki kwenye Maandiko Matakatifu ya Mungu Aliye hai. Mawazo yaliyopekelea kuanza kwa mafundisho haya hayatokani na Biblia kabisa na hayapatikani humo. Bali yote haya yametokana na mawazo tu ya wanadamu. Hayana mashiko yatokanayo na Maandiko Matakatifu bali yote haya ni ubatili mtupu, au hayana maana yoyote kabisa na yahatimizi makusudi yoyote bali zaidi sana ni kwamba yanaleta hofu ya kidini na huku yakilificha kusudi na mpango mzima wa Mungu wa Pekee na wa Kweli. Na mpango wenyewe ni wa kuwaleta watu wote kwenye ushirika nay eye, unaofanyika kwa njia ya toba na utii (sawa na ilivyoandika kwenye Matendo ya Mitume 2:38 na Mathayo 7:21).

 

Kusimama Kinyume na Torati

Kuna watu ambao wamediriki hata kulaumu wakiwema kwamba utaratibu wa Amri Kumi zilizoandikwa kwenye Torati unajipinga wenyewe na maneno yanayosema (Usifanye hivi na vile…” Usemi huu umetumika mara kumi kwenye Kutoka 20 na mara kumi tena kwenye Kumbukumbu la Tirati 5. Lakini vipengele vya amri hizi kumi zinaendana pamoja kwenye utekelezaji wake. Amri hizi Kumi zinapaswa kuheshimiwa, na zina umuhimu wake fulani kwenye jamii kwa mtazamo wa watu wengi au kwa kila mmoja binafsi yake.

 

Sheria hizi za Torati zinapokuwa zinatunwa hunfanya mtu awe mtii na mnyenyekevu na mwenye kujitoa kwa Mungu. Zinamfanya mtu aendeleze tabia yake ya utii kutoka ndani, na zinamfundisha mtu namna ya kujitawala na kuyatii mamlaka. Mwanadamu anapokuwa anamudu kujifunza kuitawala roho au moyo wake, ndipo ile hali ya kutojali na kuzivunja sheria na amri zake Mungu hutoweka. Moyo wa mwanadamu unapaswa uongoke na ubadilike, vinginevyo matendo yote ya mwanadamu huwa ni ujinga mtupu.

Zaburi 14:1; 53:1a inasema: Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu;  

 

Mithali 14:7 inasema: Toka mbele ya uso wa mpumbavu, Maana hutaona kwake midomo ya maarifa.

 

Mithali 17:12 inasema: Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang'anywa watoto wake, Kuliko na mpumbavu katika upumbavu wake.

 

Mithali 18:6 inasema: Midomo ya mpumbavu huingia katika fitina, Na kinywa chake huita mapigo.

 

Mithali 13:20 inasema: Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.

 

Sheria na Torati ya Mungu imejaa hekima na mtu akiitii inampa mtu uelewa. Mtu anapoitendea kazi inaleta majibu mema na mtu anapoiasi kutoa matokeo mabaya.

 

Sheria ya Mungu hutoa majibu na suluhu ya hali ya mwanadamu kushindwa kujitawala mwenyewe na kuitawala sayari hii, na amri hii ya tatu ni sehemu kuu na muhimu ya kutawla huko. Mungu kwa hekima yake ametufunulia Sheria yake. Mwanadamu anapaswa kujifunza mumcha Mungu na kuzitii Amri zake. (Pia soma Kutoka 20:10; Kumbukumbu la Torati 5:14; Mithali 1:32; 14:7; 17:12; 10:23; 18:6; 29:11; 13:20; 26:6.)

 

Haki na hukumu ya haki

Mfano wa maamuzi ya hukumu ya kifo kwa mwenye kukufuru unapatikana kwenye kitabu cha Mambo ya Walawi 24:10-16.

Mambo ya Walawi 24:10-16 inasema: Ikawa mwana wa mwanamke wa Kiisraeli, ambaye babaye alikuwa Mmisri, akatokea kati ya wana wa Israeli; na huyo mwana wa mwanamke wa Kiisraeli, na Mwisraeli mmoja, wakapigana pamoja ndani ya marago; 11 kisha huyo mwana wa mwanamke wa Kiisraeli akalikufuru hilo Jina, na kuapiza; nao wakamleta kwa Musa. Na jina la mamaye alikuwa akiitwa Shelomithi, binti ya Dibri, wa kabila ya Dani. 12 Nao wakamtia kifungoni, ili wapate kuambiwa neno litakalotoka kinywani pa Bwana. 13 Na Bwana akasema na Musa, na kumwambia, 14 Mtoe huyo aliyeapiza nje ya marago; na wale wote waliomsikia na waweke mikono yao kichwani mwake, kisha mkutano wote na wamwue kwa kumpiga kwa mawe. 15 Nawe nena na wana wa Israeli na kuwaambia, Mtu awaye yote atakayemlaani Mungu wake atachukua dhambi yake. 16 Na yeye atakayelikufuru jina la Bwana hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzalia, hapo atakapolikufuru jina la Bwana atauawa.

 

Kitu cha msingi kuhusu aya hii ni kwamba ni Yesu Kristo ndiye alikuwa na hawa Israeli kule Jangwani. Kristo mwenyewe amesema kwamba wala hakuna mtu aliyewahi kumuona Mungu, wala aliyewahi kuisikia sauti yake. Kwa hiyo, ni Kristo ndiye aliyeiweka hukumu hii kupitia kwa Musa, nah ii inaonyesha jinsi Kristo alivyofikiri jinsi ilivyopaswa kusimamiwa.

 

Musa aliichukulia hukumu hii kama alivyoelekezwa kule jangwani na mtu tunayemdhania au kumjua kuwa ni Masihi, akiwa kama Elohim wa Israeli. “Wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.(1Wakorintho 10:4).

Mambo ya Walawi 24:23 inasema: Musa akanena na wana wa Israeli, nao wakamtoa huyo aliyeapiza nje ya marago, wakamwua kwa kumpiga kwa mawe. Wana wa Israeli wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Musa.

 

Iwapo kama huyu Malaika wa Kuwepo kwake alikuwa ni Yesu Kristo, kwa hiyo amri hii ilisimama imara bila kuzibadilishwa au kuzivunjwa na kuziathiri zile kumi nyingine zote, ikiwemo nah ii ya Sabato nay a Sikukuu Takatifu zilizoamriwa, zote zimebakia imara na pasipo kuathiriwa. Kwa ajili hii ndipo makanisa ya Waamini Imani ya Utatu wa nyakati za Zama za Kati walifanya kuwa ni tendo la kukufuru kama mtu atasema kuwa Kristo ndiye aliyekuwa na wana wa Israeli pale jangwani, akiwa kama Malaika wa Yahova au Mjumbe wa Mshauri Mkuu wa Ajabu aliyetajwa kwenye Isaya 9:6 (LXX). Na ndipo Waamini Utatu hawa wakayatumia mamlaka ya Mungu na kulitumia jina lake bure, na wakawaua mashahidi wafia dini na wakafanyika kuwa ni wanywaji wa damu za watakatifu.

 

Kulaani na kuabudu

Kutoka 21:17 inaonyesha hukumu itokanayo na mtu anayediriki kumlaani baba yake au mama yake. Umuhimu wa kumlaani mtu aliyefanya matendo ya kuliasi taifa umetokana na maandiko ya torati. Hakuna namna yoyote ya kulaani au mashitaka yanayoweza kufanywa pasipofuatwa utaratibu ulioko kwenye torati. Aina nyingine yoyote itakayofanyika itakiuka na kuivunja amri hii ya tatu, na nyingine nyingi ambazo zinaangukia kwenye mambo ya kisheria.

 

Tendo la Kumtangaza Mungu na Ibada

Mungu anapoapa kwa nafsi yake mwenyewe, kiapo kile ni lazima kibakia kama hivyo kilivyo. Isaya 45:23 ni unabii.

Isaya 45:23 inasema: Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.

 

Hapa Mungu anatangaza kwamba historia ndiyo itakayohitimisha na kuweka kikomo cha kumuabudu yeye, na kiapo cha kimungu kitakuwa ni msingi wa kila jamii na kila kabila.

Mika 6:8 inasema:  Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!

 

Yakobo 5:12 inasema: Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.

 

Neno la Mungu halitarudi bure, na wala jina lake halitatumika bure (sawa na Warumi 14:11).

 

Kwenye kila kizazi Mungu amewalinda na kuwatunza wale wote wasioupigia magoti mfumo huu, na wakiwa wamemkubali na kubakia waminifu kwake (1Wafalme 19:18).

1Wafalme 19:18 inasema: Pamoja na hayo nitajisazia katika Israeli watu elfu saba, kila goti lisilomwinamia Baali, na kila kinywa kisichombusu.

 

Mungu amemchagua Yesu Kristo kuwa ni mtiwa mafuta wake na wote watampigia magoti kwa jina la Mungu.

Wafilipi 2:10 inasema: Ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;

 

Kile kinachatakiwa kijulikane na Mungu ni kuonekana kwa wateule wanaofanya kazi kwa jina lake. (Warumi 1:19-20). Katika Ufalme unaokuja wa Mungu watu hawataliitia jina la Mungu kwa uwongo kama walivyofanya kwenye kipindi kilichopita huko nyuma (Mwanzo 4:26). Yule liyechaguliwa kuwa kama ni Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melkizedeki atatangazwa kuwa ni Mfalme wa Wafalme na atatawala kwa jina la Mungu wa Pekee na wa Kweli aliyemtuma (Yohana 17:3); na hakutakuwa na ulimi wowote utakaolitaja jina la Mungu bure tena.

q