Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[256]

Sheria na Amri ya Nne [256]

(Editor 1.1.19981007-20000118)

Amri ya Nne ya Mungu inahusu Sabato au pumziko. Hii inajumlisha na Sabato ya kila Siku ya Saba ya Juma, Siku Takatifu, Sabato ya kila Mwaka wa Saba ya Mapumziko ya Ardhi na Utaratibu wa Yubile. Hizi zote zimefungamanishwa kutokana na Kalenda ya Mwandamo wa Mwezi na Mwelekeo wa Nyota na ni za muhimu kuadhimishwa kwa manufaa ya wote wenye mwili (Mk.2:27). Zinasimama pamoja au zinaanguka pamoja (Kol.2:16-17).

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

E-mail: secretary@ccg.org

(Copyright © 1998, 1999, 2000  James Dailley)

Masomo haya yanaeza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

This paper is available from the World Wide Web page:

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org and http://www.ccg.org


Sheria na Amri ya Nne [256]


Sheria zilizo elelekezwa

Kuna zike za kila juma, au za Siku ya Saba au Mwezi Mpya, za kila mwaka au Siku Takatifu, za mapumziko ya ardhi kwa kila miaka saba na Sabato za marejesho ya Yubile, zote zimeamriwa na zote inabidi ziadhimishwe.

Kumbukumbu la torati 5:12-15 inasema:

12 Ishike siku ya Sabato uitakase, kama BWAA, Mungu wako, alivyokuamuru. 13 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 14 lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng’ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako yeyote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vilevile kama wewe. 15 Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa BWANA, Mungu wako, alikutoa huko na mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wako, alikuamuru uishike Sabato.

Kutoka 20:8-11 inasema:

8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

Neno ‘Sabato’

Katika Kamusi ya Kiebrania iitwayo Strong Hebrew’s Dictionary (SHD 7676), neno sabbat linamaana ya kukuma au kupumzika. Ni siku iliyotengwa kwa ibada (Law.23:3) na siku ya mapumziko na kuburudika (Kut.23:12) ni ishara ya Ubwana wa Mungu kwa viumbe au uumbaji wake na ni baraka ya kwanza kuandikwa na ilitakaswa au kutengwa na uumbaji wa Adamu (Mwa.2:2-3). Ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu (Mk.2:27) na maadhimisho yake inafungamanishwa na imani. Iliadhimishwa na Abraham (Mwa.26:5) ambaye alipewa kweli ya Mungu (Mwa.24:27) na aliye waongoza wengine katika njia (Mwa.24:48). Kwa kuadhimisha kwao, Israeli walikiri kuwa wao ni watu wake waliokombolewa watakaoshika sheria zake.

Kwa kupumzika huku tunadhihirisha imani yetu kwa Mungu. Adhimisho la Sabato lilinenwa kuwa ni baraka. (Isa.56:2-4; 58:13; 66:23; Eze.44:24; 45:17; 46:1,3-4,12). Israeli walikemewa kwa kupuuzia kuitunza (Isa.1:13; Yer.17:21-27; Eze.20:12-24; Amosi 8:5). Urefu wa Yuda kuwa utumwani Babeli ulilinganishwa na jinsi walivyoutia unajisi mwaka wa Sabato au mapumziko ya ardhi (2Nya.36:21).

Sabato kama Ishara au Muhuri

Sabato ni amri ya nne kati ya amri kumi za Mungu na inapatika katika vitabu vyote viwili yaani Kutoka 20:8-11 na Kumbukumbu la torati 5:12-15. Siku ya Sabato ni takatifu kwa Bwana, Mungu (Yehova Elohim), kwa mujibu wa amri ya nne.

Katika kutoka 20:8-11 tunasoma:

8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

Hii inaonyesha kwamba kila mmoja hata mnyama wa kufugwa, na apumzike (Kum.5:14).

Kwa siku sita twaweza kufanya kazi (Kum.5:13) kulima na kutunza au kuangalia uumbaji wake (Mwa.2:15) na hatutakiwi tuendekeze uvivu (2The.3:6-11). Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako (Muh.9:10). Kwa kuwa chochote apandacho mtu ndicho atakacho vuna (Gal.6:7).

Siku ya saba ya juma ni Sabato. Ilihesabiwa kuwa ni Sabato tangia uumbaji wa Adamu. Inajulikana kwa mataifa yote kuwa ni Sabato na inangukia siku ya Jumamosi kwa kalenda zetu za siku hizi. Siku hii ta saba imo katika mzunguko endelevu na haiwezi kuwekwa siku nyingine bila kutilia maanani ni lini inaangukia kwa mujibu wa kalenda ya mzunguko wa jua au mwezi.

Kalenda Mpya ya Ulimyengu na mabadiliko yake yaliyoko, yanakiuka kiini cha sheria. Kalenda ya Ulimwengu ina miezi kumi miwili, kalenda bwawa yaani isiyo na mabadiliko yenye mihula minne yenye robo zinazofanana. Ni kalenda bwawa kwa sababu inabaki vivyohivyo kila mwaka.

Kalenda yetu ya leo sio kalenda bwawa, ila ni ya kila mwaka. Hubadilika kila mwaka. Inafanya hivyo kwa sababu ya urefu wake wa mzunguko wa siku 365 hauwezi vilevile kugawanyika kwa idadi ya siku za wiki. Na hauna ule mwezi wenye siku 29.5 ujulikanao kama mwezi wenye muelekeo na nyota.

Mafuatano ya ukumbushio wa siku ile moja ni kwamba kwamfano mwaka huanza na kuishia katika siku ileile ya wiki. Hivyo basi mwaka unaofuata lazima uanzie katika siku inayofuata ya wiki. Ndio maana inalazimu kila mwaka kuwepo kalenda nyingine.

Kitaalamu, Kalenda yetu ya Kigregoriani imetokana na mzunguko wa majaribio mbalimbali wa kalenda kumi na nne. Kalenda ambayo kwa mwaka unaoanzia Jumapili hutofautiana na ule ambao mwaka unaoanzia Jumatatu, kadhalika kwa siku nyingine zote saba. Tangia kuanzishwa kwa utaratibu wa mwaka mrefu wenye Februari yenye siku 29 kuliweza geuza uwepo wa kalenda hizi zote saba, na kufanya jumla yake.

Kama tukiiondoa siku ile isiwepo katika kalenda, basi kwa hakika mwaka mpya ungekuwa unaanzia katika siku ileile ya wiki kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma. Hivyo basi tungekuwa na kalenda isiyo badilika.

Tunaweza kuiondoa siku nje ya kalenda bila kupotosha kutoka na mzunguko wa jua wenye wastani wa siku 365.24 kwa kuichukulia tu kila siku kuwa ina masaa ishirini na manne kipindi cha kusubiria kabla ya kuanzisha kalenda tena. Siku hizi fifi katika kalenda, huitwa pia “siku tupu” au “siku zisizo za kawaida,” haviwezi kuwa siku za wiki. Inaonekana kuwa ni busara zitumiwe kama sikukuu na sehemu ya Kalenda ya Dunia. Pendekezo hili na mengine huondoa mafuatano ya juma la siku saba katika uumbaji wa Adamu. Mzunguko huu wa siku saba hauingii, iwe kwenye utaratibu wa mwezi muandamo au kwa mwaka wa unaofuata utaratibu wa kila mwaka wa jua.

Walawi 23:32 hutuonyesha kuwa siku hasahasa huishia na huanzia majira ya jioni na sio usiku wa manane au asubuhi.

Walawi 23:32, inasema:

32 Itakuwa kwenu Sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtazitesa nafsi zenu; siku ya kenda ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hata jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu.

Siku ya saba huanzia mwishoni mwa siku ya sita ya juma, ambayo ni Ijumaa kama tulivyozoea kuiita, wakati giza linaanza au jioni ya mabadilishano ya zamu za mabaharia kwa utaratibu wa mambo ya vyombo vya majini (EETN). Angalia somo lisemalo Kuanza kwa Mwezi na kwa Siku (No. 203).

Hii imethibitishwa na Paulo katika Matendo 27:27-34 na Mishnah, ambayo ni utunzi wa uandhishi wa karne ya pili ulioandika matukio ya nyuma hadi ya karne ya pili KK. Angalia mgawanyo wa pili, usemao Moed, Sabato 1:3, 15:3.

Hakukuwepo kununua wala kuuza wala kazi iliyokuwa inahitaji kufidiwa haikufanyika siku ya Sabato. Hii haimaanishi kuwa hakukuwa na shughuli kabisa. Nehemia ni mfano kwa aina ya kazi zilizofanyika siku ya Sabato.

Nehemia 10:28-31 inasema:

28 Na watu waliosalia, makuhani, walawi, mabawabu, waimbaji, Wamethini, na hao wote waliojitenga katika watu wa nchi kwa torati ya Mungu; wake zao, na wana wao, na binti zao, kila mwenye maarifa na akili; 29 wakaambatana na ndugu zao, wakuu zao nao wakaingia katika laana na kiapo, ya kuwa wataiendea torati ya Mungu, iliyotolewa kwa mkono wa Musa, mtumishi wa Mungu, na kuziangalia, na kuzitenda, amri zote za BWANA, Bwana wetu, na hukumu zake na sheria zake; 30 wala tusiwaoze watu wan chi binti zetu, wala kuwatwalia wana wetu binti zao; 31 tena watu wan chi wakitembeza biashara,  au chakula chochote, siku ya Sabato, tusinunue kwao siku ya Sabato, au siku takatifu; tena kwamba tuuache mwaka wa saba, na madai ya kila deni.

Utararatibu wa Kisabato inabidi ueleweke ili kukufanya uweze kushirikisha wengine kushika taratibu zake, ambao ni waakipekee kwa watu wa Mungu.

Mkate usiotiwa Chachu ni ishara ya sheria za Bwana (Kum.6:8) na jinsi Alivyowakomboa Israeli (Kum.6:30) ambayo kupitia dhabihu ya Kristo, inahusisha wote walio ndani ya Kristo (Rum.9:6, 11:25-26). Ishara hizi ziliwalinda Israeli wasivyutwe kuabudu sanamu (Kum.11:16) ni ishara na muhuri wa wateule wa Bwana (Ufu.7:3).

Ni ishara, SHD 226, neno owth au ot ni alama inayotofautisha au ishara ya kukumbushia kazi ya mtu. Sabato zimeorodheshwa kama ishara ya watu wa Mungu. Ni ishara kati yetu na Mungu atutakasaye.

Kutoka 31:12-14 inasema:

12 BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 13 Kisha nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwakuwa ni ishara kati mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi. 14 Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwakuwa kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.

Ni kwa nadra na kimakosa imedhaniwa kuwa Sabato ambazo ziliongelewa hapa ni uwingi wa umoja wa Sabato za kila wiki. Hiyo si sahihi. Sabato zimepelekea hadi kufikia hatima ya kuabudu siku za Miandamo ya Mwezi Mpya, Siku Takatifu na utaratibu mzima wa Yubile pamoja na maelekezo yake ya kiuchumi. Tendo la kuuawa vilevile lipo kiroho na linaendeza nia ya kuwalinda wana wa maagano na ushawishi wa ibada za sanamu.

Sabato ishara iliyopuuziwa katika imani ya Kanisa La Mungu; vilevile ni ishara ya wana wa maagano ambao bado hawajaitwa kujiunga na Kanisa. Kama ingekuwa ni ishara teule, basi walio katika imani ya Kiyahudi na Wasabato wenyekuamini juu ya miungu miwili na wenye kuamini mafundisho ya Utatu Mtakatifu wangekuwa miongoni mwa watakaokuwepo katika ufufuo wa kwanza. Lakini hawatakuwemo.

Ishara ya pili ni Pasaka na Mikate isiyotiwa Chachu.

Kutoka 13:9-10 inasema:

9 Nayo itakuwa ishara kwako katika mkono wako, na kwa ukumbusho kati ya macho yako, ili kwamba sheria ya BWANA ipate kuwa kinywani mwako; kwani BWANA alikutoa utoke Misri kwa mkono wenye uwezo. 10 Kwa hiyo utaitunza amri hii kwa wakati wake mwaka baada ya mwaka.

Upatanisho ni ishara nyingine ya wana wa agano. Asiyeitunza siku ya Upatanisho alihukumiwa kwa kukatiliwa mbali na watu wake, kwa maneno mengine, ni mbali na mwili wa agano wa Israeli, ambao ni Kanisa (Law.23:29; Rum.9:6-8).

Walawi 23:26-32 inasema:

26 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 27 Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtazitesa nafsi zenu; nanyi mtazisongeza sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto. 28 Nanyi msifanye kaziyoyote siku hiyo; kwa kuwa ni siku ya upatanisho, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za BWANA, Mungu wenu. 29 Kwa kuwa mtu awaye yote asiyejitesa mwenyewe katika siku iyo hiyo, atakatiliwa mbali na watu wake. 30 Na mtu yeyote afanyaye kazi ya namana yo yote siku hiyo, mtu huyo nitamwangamiza atoke katika watu wake. 31 Msifanye kazi ya nama yo yote; ni amri ya milele katika vizazi vyenu, katika makao yenu yote. 32 Itakuwa kwenu Sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtazitesa nafsi zenu; siku ya kenda ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hata jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu.  

Siku hii ya Upatanisho pia ilitumika kwa kutangaza Yubile, kwakuwa Yubile ni miongoni mwa vitu vya msingi katika utaratibu wa Mungu katika kuweka taratibu za shughuli za wanadamu duniani. Ni sabato kuu, ni Sabato ya Sabato zotetakatifu sana ambayo huwekwa mkazo wa utakatifu wake (tazama SHD 7677). Mlinganisho wa kiroho wa Yubile utalinganishwa mbele baadae.

Walawi 25:8-12 inasema:

8 Newe utajihesabia Sabato saba za niaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda. 9 Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu, yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; kayika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote. 10 Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupigwa mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote waiketio itakuwa ni Yubile* kwenu; nanyi kila mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake. 11 Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni Yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenywewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa. 12 Kwa kuwa ni Yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani.

Sukui ya Upatanisho kwa hakika haimo kwenye kundi la siku za kutoa sadaka ambazo hutegemea ukarimu na jinsi mtu alivyobarikiwa. Kwahiyo pia ni Siku ya kupigwa Baragumu. Hii mi kwasababu hakuna kati ya siku hizi zinahusiana na shughuli za mwanadamu wala bidii zake. Siku Takatifu ya Upatanisho iko hasa kwa ajili ya hesabu ya watu kwa aina ya makusanyo yanayotolewa.

Kutoka 30:11-16 inasema:

11 BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 12 Utakapo wahesabu wana wa Israeli, kama itakavyotokea hesabu yao, ndipo watakapo mpa BWANA kila mtu ukombozi kwa ajili ya roho yake, hapo utakapowahesabu; ili kwamba yasiwe maradhi kati yao, hapo utakapo utakapowahesabu. 13 Nacho watakachotoa ni haki, kila mtu apitaye kwa wale watakao hesabiwa atatoa nusu shekeli kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu;, (shekeli ni gera ishirini); nusu shekeli kwa sadaka ya BWANA. 14 Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa tangu huyo ambaye umri wake ni miaka ishirini, au zaidi, atatoa hiyo sadaka ya BWANA. 15 Matajiri hawataleta zaidi, wala maskini hawataleta kilichopungua, katika hiyo nusu shekeli, watakapotoa hiyo sadaka ya BWANA, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu. 16 Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania; ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mele ya BWANA, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.

Kodi au makusanyo yaliyofanywa siku ya Upatanisho yalikuwa ni kwaajili ya kuheasabu Israeli. Ni uzani sawa uliowekwa kwa kila mtu, na haukutakiwa utofautiane kulingana na hali aliyonayo mtu. Hesabu hii ilifanywa na Mungu hata kabla ya kuwekwa misingi ya dunia (Ufu.17:8) na uzani wa maachilio ulilipwa mara moja na kwa wote na Yesu Kristo (Rum.6:10). Kuwekwa huru huku kunamaanisha kuwa wokovu umeshalipiwa sio kulingana na mazingira ya kimwili ya kila mmoja, bali kwa dhabihu ya Kristo ilitolewa mara moja tu na kwa wote (Ebr.7:27, 9:26; 10:10; 1Pet.3:18). Ukusanyaji matoleo siku ya Upatanisho unaendana sambamba na tendo la dhabihu ambayo Yesu Kristo aliitoa.

Na ni kwa ajili hii ni kwamba kuna makusanyo kufanyika mara tatu tu kama yalivyoelezewa katika Kutoka 23:14-18, 34:24; Kumbukumbu la torati 16:16; 1Wafalme.9:25 na yanapaswa yachukuliwe kabla ya asubuhi ya siku ya kwanza ya kila sikukuu.

Kutoka 23:14-18 inasema:

14 Mara tatu kila mwaka utaniwekea sikuu. 15 Utaiweka sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu; utakula mikate isiyochachwa kwa muda wa siku saba kama nilivyokuagiza, kwa wakati uliowekwa, mwezi wa Abib (kwa maana ndio mwezi uliotoka Misri); wala hapana mtu atakayeonekana mbele yangu na mikono mitupu; 16 tena, sikukuu ya mavuno, hayo malimbuko ya kazi zako za kupanda mashambani; tena sikukuu ya kukusanya, mwisho wa mwaka, hapo utakapokusanya hayo uliyoyataabikia shambani. 17 Mara tatu katika mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele ya Bwana MUNGU. 18 Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate usiotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi.

Ishara au nadhiri zilitumika kwa mara ya kwanza katika Mwanzo 9:12. upindi wa mvua ulikuwa ukumbusho wa kudumu wa Mungu kwa ahadi yake kuwa hataigharikisha tena dunia kwa maji mara nyingine. Mungu hutumia ishara pia katika kuwatambulisha wale walio na uhusiano maalumu na yeye.

Mwanzoni kabisa na ishara ya kwanza ya wana wa maagano ilikuwa ni tohara (Mwa.17:10-14). Tendo hili la kimwili lilikuwa ni alama. Kwa sasa hufanyika kiroho na inajumlisha na wanawake kwa njia ya ubatizo (tazama karatasi toba na ubatizo (No.52). huu ulikuwa ndio kusudi tokea mwanzo (Kum.10:15-17) lakini pia inahitaji ushiriki wa Mungu.

Kumbukumbu la torati 30:6 inasema:

6 BWANA, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate kuwa hai.

Kubatizwa na kumpokea Roho Mtakatifu, ni ishra za kwanza za mteule, kupitia damu ya Yesu Kristo katika mwili mmoja (Mat.28:19; Mdo.1:5, 11:16; Rum.6:3; 1Kor.12:13; Ebr.9:11-28). Ishara hizi za sheria, yaani Sabato na Pasaka ziliwekwa kwa makusudi ili kuwalinda Israeli na ushawishi wa ibada ya sanamu(Kum.11:6). Ishara hizi mbili hufanya kazi kama mihuri katika mikono na katika paji za nyuso za wateule wa Mungu.

Kwa njia ya Roho Mtakatifu zinatengeneza msingi wa muhuri tusomao katika Ufunuo 7:3 wa siku za mwisho. Ishara ya wateule ni ile iliyoko katika amri ya kwanza ya Mungu. Kristo alisema …Msujudie Bwana Mungu wako,umwabudu yeye peke yake (au umtumikie) (Mat.4:10; Lk.4:8). Huduma yetu ni kuabudu katika katika usemi wa Kibiblia na tamko hili huonyesha kuwa kuna Mungu mmoja tu, Mungu Baba, anayestahili kuabudiwa, Hahoshua, Mmpakwa mafuta wake hastahili kuabudiwa.

Sabato ni ishara mojawapo ya Kanisa la Mungu. Ishara ya mwanzoo ni Uungu. Muundo wa Kibiblia katika Uungu ni kwamba kuna Mungu Mmoja (Kum.6:4; 1Kor.8:4) ambaye tunamjua (Hos.8:2, 13:4). Tunatakiwa tujue yote mawili, yeye (Gal.4:8-9) na mapenzi yake (Mdo.22:14).

Tunaambiwa umuhimu wa kuwatenganisha Mungu na Kristo wake (Yoh.17:3) na ni kwa aibu yetu ya milele ikiwa hatuta au hatuwezi (1Kor.15:34). Kufahamu kuwa Yehova Shabaot, Bwana wa majeshi, ni Mungu wa pekee, ni msinghi muhimu katika imani.

Ubatizo ni ishara ya pili na kumpokea Roho Mtakatifu ni muhuri wa ndani. Ishara ya nje ni Sabato na Ushirika wa Meza ya Bwana/Pasaka, ambayo ni ya sheria za Mungu. Ikifuatiwa na Miandamo ya Mwezi Mpya na Siku Takatifu. Sabato hupigwa vita na wanadamu kwasababu ya ushwishi wa ibada ya sanamu.

Ezekieli 20:15-20 inasema:

15 Tena naliwainulia mkono wangu jangwani, ya kwamba sitawaingiza katika nchi ile niliyokuwa nimewapa, ijaayo maziwa na asali, ambayo ni utukufu wa nchi zote; 16 kwa sababu walizikataa hukumu zangu, wala hawakuenda katika amri zangu, wakazitia unajisi Sabato zangu, kwa maana mioyo yao iliandama vinyago vyao. 17 Walakini jicho langu likawahurumia nisiwaangamize kabisa, wala sikuwakomesha kabisha jangwani. 18 Kisha nikawaambia watoto wao jangwani, Msiende katika amri za baba zenu, wala msizishike hukumu zao, wala msijitie unajisi kwa vinyago vyao. 19 Mimi ni BWANA, Mungu wenu; endeni katika amri zangu, mazishike hukumu zangu, na kuzitenda; 20 zitakaseni Sabato zangu; nazo zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 

Tendo la kuzinajisi Sabato chanzo chake ni ushawishi wa ibada ya sanamu. Sabato zinajumlisha siku zile zote zilizotengwa na Mungu kwaajili ya ibada kwa mujibu wa Kalenda yake, ikiegemea katika maadhimisho sahihi ya Mwezi Mpya. Mungu huliadhibu taifa kwa kushindwa kwake kumtii na kuzishika amri zake.

Ezekieli 20:21-24 inasema:

21 Lakini watoto hao waliniasi; hawakuenda katika amri zangu wala hawakuzishika hukumu yangu kuzitenda, ambazo mwanadamu ataishi kwazo kama akizitenda, walizitia unajisi Sabato zangu; ndipo nakasema, kwamba nitamwaga ghadhabu yangu juu yao, ili kuitimiza hasira yangu juu yao jangwani. 22 Lakini naliuzuia mkono wangu, nikatenda kwa ajili ya jina langu, lisitiwe unajisi mbele ya macho ya mataifa, ambao mbele ya macho yao niliwatoa. 23 Tena niliwainulia mkono wangu jangwani, kwamba nitawatawanya kati ya mataifa, na kuwatapanya katika nchi mbalimbali 24 kwa sababu hawakuzitekeleza hukumu zangu, bali walizikataa amri zangu, nao walizitia unajisi Sabato zangu na macho yao yaliandama vinyago vya baba zao.

Sabato ni kitu kisicho tenganishwa na amri ya kwanza ya sheria. Taifa hupata hukumu kwa kushindwa kwake kushika kanuni zote za sheria ya Mungu (Zek.14:16-19).

Sabato ni ishara ya uaminifu wetu na ukombozi wetu kwa mapumziko na Mungu. Kuiacha Sabato ni kuachana na tumaini letu na Mungu. Hii ndio sababu kwamba kwasiku hizi tunapitia mateso kwa ajili ya kuishika Sabato za Bwana, Mungu wetu.

Kila anayeitia unajisi atauawa (Kut.31:14; Hes.32:36). Ni ishara kati ya Mungu na wana wa Israeli milele (Kut.31:17).tafsiri hii ya neno milele ni kutoka katika Kamusi ya Kiebrania inayoitwa kwa kifupi SHD 05769, Olam, neno linalobeba maana ya ‘zama zisizo kikomo”sawa na kusema cha siku zote, chenye kudumu muda mrefu, ukamilifu wa dahari au milele, nk.

Sisi wapya au wafuasi wa maagano yaliyofanywa upya tufuatao njia, ni Israeli wa kiroho (Rum.9:4).

Maandlizi ya Sabato yanapaswa yakamilike katika siku za nyuma yake (Kut.16:5). Chakula kinapaswa kikusanywe na kuandaliwa kwa mfano wa mana. Kila mtu apaswa kubakia katika sehemu yake Kut.16:29-30). Wakitakiwa kupumzika na kustarehe kwa majira ya kupanda nay a kuvuna katika siku ya Sabato (Kut.34:21). Matendo ya Bwana ya kuchuma masuke siku ya Sabato yali lalamikiwa na wale walioidhania Sabato kuwa ni mzigo kwa kuongeza mapokeo yao ya bure.

Usemi wa Bwana kuwa yeye ni Bwana wa Sabato waukuwa na maana kuwa Sabato haikufaa iendelee kutunzwa, ila ulikuwa unaonyesha kulaumu kuwa ilikuwa inaadhimishwa kwa namana isiyostahili. Ni makosa kuchuma chakula au kuandaa chakula katika siku ya Sabato kutokana na aya hii na vilevile katika sheria za Agano (Mat.12:1-12).

Mathayo 12:1-12 inasema:

Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya Sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala. 2 Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya Sabato. 3 Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wenziwe? 4 Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao? 5 Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya Sabato makuhani hekaluni huinajisi Sabato na wasipate hatia? 6 Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu. 7 Lakini kama mgelijua maana yake maneno haya, Nataka rehema wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia. 8 Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye BWANA wa Sabato. 9 Akaondoka huko, akaingia katika sinagogi lao. 10 Na tazama, yumo mtu mwenye mkono uliopooza; wakamwuuliza, wakisema, Ni halali kuponya mtu siku ya Sabato? Wapate kumshitaki. 11 Akawaambia, Ni mtu yupi miongoni mwenu mwenye kondoo mmoja, na yule kondoo ametumbukia shimoni siku ya Sabato, asiyemshika akamwopoa? 12 Je! Mtu si bora kuliko kondoo mmoja mara ngapi? Basi ni halali kutenda mema siku ya Sabato.

Aya ya tatu hapo juu inaturudisha kwenye 1Samweli 21:6 ambapo Daudi alikuwa mikate ya wonyesho iliyokatazwa (Kut.25:30; Law.24:5-8). Na vilevile, makuhani Hekaluni waliinajisi au kubadili matumizi Sabato na wasilaumiwe (Mat.12:5; Hes.28:9-10; pia soma Neh.13:7; Eze.24:21; Yoh.7:22-23).

Kazi zile tuzifanyazo siku ya Sabato zinazohusiana na ibada kwa Mungu kama wateule hatubebi hukumu. Kwakweli kulikuweko na wingi wa dhabihu zilizokuwa zinabebwa siku ya Sabato kuliko siku nyingine yoyote. Aina fulani ya mahangaiko tunayoshughulika nayo yaweza kutuhukumu sio kwa sababu ya kushughulika kwetu.

Kristo vilevile aliamuru kuponywa wagojwa. Hii inatakiwa ifanyike siku ya Sabato. Ni halali kuponya na kuwalisha wagonjwa na kuwaganga waliovunjika siku ya Sabato (Lk.6:8-10; 13:14-16; 14:3; Mat.12:10-13).

Yohana 7:23 inasema:

23 Basi ikiwa mtu hupashwa tohara siku ya Sabato, ili torati ya Musa isije ikavunjika, mboma mnanikasirikia mimi kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya Sabato?

Lika 14:5 inauonyesha kuwa ni muhimu kushughulika na mambo ya dharura siku ya Sabato.

Hii ni kwakweli ilikuwa inaongelea wazo la kuponya watu siku ya Sabato. Uangalifu sahihi na maandalizi kwa wagonjwa na wanaoteseka siku ya Sabato ni suala muhimu sana. Lakini ikiwa mtu anakula na na kufanya shughuli hizi kisirisiri kwa kudhani kuwa yuko peke yake na hakuna anayemuona katika siku ya Sabato ni aibu na kupoteza maana yake. Inatakiwa watu wajiandae kwaajili ya Sabato ilikwamba waweze kuwafaidia wapendwa wao.

Marko 3:1-5 inasema:

Akaingia tena katika sinagogi siku ya Sabato, na palikuweko huko mtu mwenye mkono uliopooza; 2 wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya Sabato, wapate kumshitaki. 3 Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati. 4 Awauliza, Ni halali siku ya Sabato kutenda mema , au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua?  Wakanyamaza. 5 Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioya yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake akawa mzima tena.

Fundisho lile la ng’ombe kutumbukia shimoni linasemea mambo ya dharura, lakini tunatikiwa kupanga mambo mapema. Punda haitakiwi wabebeshwe mizigo (Neh.13:15) na malango ya mji yanatakiwa yafungwe, yasifunguliwe (Neh.13:19). Hii inamaana kuwa tunatakiwa tuzizibe kila aina ya fursa ya kufanya kazi. Mizigo inatakiwa isibebwe (Yer.17:21) na kuni zisiokotwe (Hes.15:32-35). Miganda isiletwe ndani na divai isishinikizwe au kukamuliwa (Neh.13:15). Katika maandalizi siku hizi zote, kazi ni budi isimamishwe.

Vishada (RSV) au kipande cha nguo kilichoshonwa (KJV) cha rangi ya buluu kilishonwa kwenye pembe au pindo za nguo zao ili ziwakumbushe sheria za Mungu.

Hesabu 15:37-41 inasema:

37 Kasha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 38 Nena na wana wa Israeli, na kuwaagiza ya kwamba wajifanyie vishada katika ncha ya nguo zao, katika vizazi vyao, tena ya kuwa watie katika kila kishada nyuzi za rangi ya samawi; 39 nacho kitakuwa kwenu ni kishada, ili mpate kukiangalia, na kuyakumbuka maagizo yote ya BWANA, na kuyafanya;tena kwamba msiende kutanga-tanga kuandama mioyo yenu wenyewe, na macho yenu wenyewe, ambayo mlikuwa mkiyaandama kwa uasherati hapo kwanza; 40 ili mpate kukumbuka na kuyafanya maagizo yangu yote, na kuwa watakatifu kwa Mungu wenu. 41 Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Hii ni kwako binafsi kati yako na Yehova, Elohim wako. Haisababishi mtu kupata hukumu asipoifanya kama ilivyo kwa sheria nyingine zinapovunjwa. Ni ya muhimu ingawa lakini haifai itumike kama onyesho (Mat.23:5).

Chakula na bidhaa zozote hairuhusiwi iwe kununua (Neh.10:31) au kuuzwa (Neh.13:15).   Mambo yote mawili, kununua na kuuza ni shughuli zilizokatazwa kabisa. Ukombozi ni kitu ambacho utaratibu wa Sabato unalenga na maisha yaweze kuokolewa (Mk.34Lk69) na kuokoa ni kitu kinachotakiwa kufanyika pale inapowezekana (Mat.12:11).

Tutasoma na kujifunza kushika taratibu zake kamilifu za Sabato, sio tu kwa sababu tunaogopa kuhukumiwa, bali ni kwa sababu tunampenda Mungu wetu wa Pekee wa Kweli.

1Yohana 5:3 inasema:

3 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake, wala amri zake si nzito.

Sabato hizi sio mzigo kuzishika, bali inatakiwa kuzishika katika roho na uchaji (Isa.113). Hazitakiwi kuchafuliwa wala kutiwa unajisi (Isa.56:2, 4-7).

Isaya 56:2 inasema:

2 Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye haya; azishikaye Sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wowote.

Isaya 56:4-7 inasema:

4 Kwa maana BWANA awaambia hivi matowashi, wanoazishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu; 5 Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lilio jema kuliko kuwa na wana na binti nitawapa jina lidumulo milele, lisilo katiliwa mbali. 6 Na wageni walioandamana na BWANA wamuhudumu, na kulipenda jina la BWANA, kuwa watumishi wake; kila aishikaye Sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; 7 Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu, zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu, kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.

Sabato ni kwa furaha na vicheko na sio kwa maombolezo (Isa.58:13-14). Itatunzwa na wote wakati watakapokuja kumuabudu Bwana, kutoka Mwezi Mpya hadi mwingine na kutoka Sabato hadi Sabato (Isa.66:23).

Hakuna aina yoyote ya mzigo unaoruhusiwa kubebwa siku ya Sabato, kama ilivyokuwa kuingizwa au kubebwa katika mji wa Yerusalemu (Yer.17:21). Ifurahie sabato na ulete furaha katika nyumba ya Mungu. Usibebe mzigo nje ya nyumba yako siku ya Sabato (Yer.17:22) kuonyesha kwamba kufanya kazi ya kuajiriwa siku ya Sabato pia kumekatazwa. Inatakiwa itukuzwe na itunzwe na kutengwa na na siku nyingine.

Kristo alikuwa mkuu kuliko Hekalu kama sisi tulivyo wakuu kuliko Hekalu la kawaida, kama sisi tulivyo Hekalu (2Kor.6:16) na Hekalu lilijengwa kwa ajili yetu (Mk.2:27). Kwahiyo tunapaswa sote kuishika Sabato ya kila juma kama maandalizi ya nyumbani ambako tunaenda kuwa na Mungu. Hii ni kwa kila mwenye mwili, kama walivyopewa Israeli kama jaribio (kut.16:18).

Sabato ni ya muhimu ili kuurithi ufalme wa Israeli kama hakuna mzigo wa kuletwa ndani kupitia malango ya mji. Wafalme na wana wa ufalme wataketi katika kiti cha enzi cha Daudi. Lakini kama maonyo yake yakipuuziwa, hivyo mji uta utangamizwa kwa moto (Yer.17:27). Mataifa watazidhihaki Sabato (Omb.1:7, RSV iasema maanguko) katika siku za taabu yake. Kwahiyo Sabato ni ishara na ni chanzo cha mjeledi wa mateso kwa wale wote walio katika nyumba ya Mungu. Mfalme na kuhani watachukua machungu ya hasira yake kwaajili ya kunajisi kwao Sabato (Omb.2:6).

Sabato ni kwa vicheko na furaha, lakini kwa adhabu, vicheko vya Sabato vimeondolewa mbali (Hos.2:11).Utaratibu mzuri budi unatakiwa kufanyika siku ya Sabato. Ni vema kusubirisha jambo moja baada ya jingie kukamilisha ili lichukue pahala pake, kwa sababu hii itachukuliwa kwa mtazamo wa uaminifu, dhabihu na utoaji (Amosi 8:5). Kumbuka kutenda mema kila wakati na kuwatianguvu waliolegea kila mahali (Lk.13:10-16).

Luka 23:54 inaonyesha kwamba unatakiwa kufanya maandalizi kwa ajili ya Sabato. Fikiri kabla, hudumianeni na kutendeana mema. Tuonyeshe kuwa tunapendana kama Kristo anavyotupenda. Na tukue katika imani kama tunavyopaswa kuwa (Lk.5:5-14).

Ni kama ilivyokuwa ni ruhusa kufanya tohara siku ya Sabato, vivyohivyo inaruhusiwa kufanya tohara ya mioyo yetu kwa kujitoa kwa uweza wa Roho. Tuhukumiane kwa hukumu ya haki na kutenda matendo mema siku ya Sabato (Yoh.7:21-24).

Isaya 56:2 inasema:

2 Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye haya; azishikaye Sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wowote.

Baraka zitawapata wale wote wanaozishika taratibu za Sabato na kwa wale wanaohubiri na kuwatia moyo watu kuzinajisi Sabato, tunasoma katika Yeremia 10:21 hivi:

21 Kwa sababu wachungaji wamekuwa kama wanyama, wala hawakuuliza kwa BWANA, basi hawakufanikiwa na makusudi yau yote yametawanyika.

Wachungaji wa Israeli ya kiroho ambao hawajifunzi na kujisoma kwa bidii na kulitii neon la Mungu, watahukumiwa na kondoo wao watatawanyika! Hukumu hii inaweza kumaanisha kuwa ni kifo kwa kila mchungaji anayehubiri kuzitia unajisi Sheria hizi (Isa.66:16-24).

Kipindi baada ya Masihi, tunatakiwa kubatizwa tukiwa watu wazima kwaajili ya kumpokea Roho na kurudia tena maagano. Ulazima wa kushika Sabato (SGD 4520) unabaki palepale.

Waebrania 4:9-11 inaema:

9 Basi, imesalia raha ya Sabato kwa watu wa Mungu. 10 Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. 11 Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa ,fano huohuo wa kuasi.

Sabato ya kustarehe ya siku ya saba ya juma inabakia palepale! Sisi tuliobatizwa Israeli wa kiroho ambao tumerudia tena maagano kwa Mungu wetu, tutaendelea kuitunza na hatutafanya kazi katika siku hizi.

Kutoka 31:12-18 inasema:

12 BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 13 Kisha nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwakuwa ni ishara kati mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi. 14 Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwakuwa kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake. 15 Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, takatifu kwa BWANA; kila mtu atakayefanya kazi yo yote katika siku ya Sabato, hakika yake atauawa. 16 Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele. 17 Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika. 18 Hapo BWANA alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sunai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu.

Katika siku zijazo, katika majira yake, Mungu atawachukua kutoka katika mataifa, watu mmoja mmoja ili kuwa makuhani na walawi kulingana na utaratibu wa Melkizedeki. Wao pamoja kila mmoja wao watakuja kumuabudu yeye katika siku ya Sabato.

Isaya 66:18-23 inasema:

18Nami nayajua matendo yao na mawazo yao;wakati unakuja nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote;nao watakuja nao watauona utukufu wangu. 19 Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puti, na Ludi wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari yangu, wala kuuona utukufu wangu nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa. 20 Nao watawaleta ndugu zenu wote katika mataifa yote, kuwa sadaka kwa BWANA, juu ya farasi na katika magari, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema BWANA; kama vile wana wa Israeli waletavyo nyumbani kwa BWANA katika chombo safi. 21 Na baadhi ya hao nitawatwaa kuwa makuhani na walawi, asema BWANA.. 22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokuwa mbele zangu, asema BWANA, ndipo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa, 23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA

Jinsi ya Kuliweka kwenye Matendo

Sabato ya kila juma ni lazima kuishika (soma Kutoka 20:8-11; Kum.5:12-15; Hes.4:9-11) kama amri ya daima ya Bwana na miongoni mwa zile amri kumi za Mungu. Ni amri isiyotakiwa kuvunjwa milele kwa watu wote. Sabato ni takatifu. Kila aitiaye unajisi Sabato hukumu yake ni kifo na kukatiliwa mbali na watu wake (Kut.31:14-15). Sabato ya siku ya saba ya juma, hubakia kwa waishikao waliofanya upya maagano yao (Ebr4:9). Siku hii ya saba huanzia katika mwisha wa kiku ya sita ya juma, yaani Ijumaa jioni wakati wa mabadilishano ya zamu ya jiona ya mabaharia. Ni kutoka jua linapozama hadi kuzama kwa jua tena siku ya pili (Law.23:32; Mdo.27:27-33). Ni agano la milele kati ya wana wa Israeli na ishar ya milele kati yao na Mungu, ili wajue kuwa yeye ndiye Muubaji wao (Kut.31:15-16). Wakristo wote walio katika kweli ni Israeli wa kiroho na wamataifa wote hatimaye wanapaswa kuja kujiunga na taifa hili la Israeli (Rum.9:6; 11:16-25). Hukumu kwaajili ya kuinajisi Sabato ni kifo sawa na kumfanyia jeuri Roho Mtakatifu na kutokuwa na sehemu katika ufufuo wa pili (Ufu.20:5).

Sabato yapaswa ifurahiwe na kupewa heshima kama Siku Takatifu ya Bwana. Sio siku ya kuendekeza uvivu na starehe lakini ni ya kusanyiko takatifu (isa.58:13-14). Hakutakiwi kufanya kazi wala kubeba mizigo siku hiyo (Yer.17:21-22) na ndani yake hatutakiwi kununua (Neh.10:31) wala kununua kitu chochote (Neh.13:15).

Miandamo ya Mwezi Mpya

Isaya 66:22-23 inasema:

22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokuwa mbele zangu, asema BWANA, ndipo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa, 23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA.

Wanadamu wameamriwa kuabudu katika matukio yote mawili, Sabato ya Siku ya Saba na Miandamo ya Mwezi Mpya (tazama pia Eze.46:6, 9:10).

Ezekieli 46:1-3 inasema:

Bwana MUNGU ASEMA HIVI; Lango la ua wa ndani, lielekealo upande wa mashariki litafungwa siku sita za kazi; lakini siku ya Sabato litafunguliwa, na siku ya mwezi mpya litafunghuliwa. 2 Naye mkuu ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango lile, upande wa nje, naye atasimama karibu na mwimo wa lango, nao makuhani wataitengeneza sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, naye ataabudu penye kizingiti cha lango; kasha, atatoka lakini lango lile halitafungwa hata wakati wa jioni. 3 Watu wan chi nao wataabudu mbele ya mlango wa lile lango mbele za BWANA , siku ya Sabato, na siku ya mwezi mpya.

Dhabihu za Mwezi Mpya kwakweli ni kuu kuliko zile za Sabato (Eze.46:4, 6). Hakuna tofauti iliyofanywa kati ya Mwezi Mpya na Sabato za kila juma. Zote mbili ni takatifu na hakuna biashara inayoruhusiwa kufanyika katika siku hiyo.

Amosi 8:5 inasema:

5 mkisema, Mwezi mpya utaondoka lini, tupate kuuza nafaka? Na Sabato nayo tupate kuandika ngano? Mkipunguza efa na kuongeza shekeli, mkidanganya watu kwa mizani ya udanganyifu.

Ishara ya dhabihu kwa ajili ya Mwezi Mpya inahusiana na Kanisa na baraza la Israeli. Bila ya kutunza Miandamo ya Mwezi, haitawezekana kabisa kuelewa Kalenda ya Mungu (soma karatasi isemayo Kalenda ya Mungu No.156). Kalenda ya Kiyahudi iliyopo sasa sio Kalenda sahihi na inahitaji irekebishwe, Sikukuu na Miezi Mipya haziwezi huadhimishwa sawasawa hivyo basi marekebisho yamechelewa. Kwa njia ya kurejesha kanuni ya Miandamo ya mwezi tu, ndipo Kalenda hii na Sikukuu zitaadhimishwa kiusahihi na kueleweka.

Mwezi Mpya ni mojawapo katika kumbukumbu za Bwana zilizoorodheshwa katika kitabu cha Hesabu 10:10.

Hesabu 10:10 inasema:

Tena katika siku ya furaha yenu, na katika sikukuu zenu zilizo amriwa, na katika kuandama miezi kwenu, mtapiga hizo tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa, na juu ya dhabihu za sadaka zenu za amani; nazo zitakuwa kwenu ni ukumbusho mbele za Mungu wenu, mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Bwana Mungu wako ni Yehova Elohim wako. Dhabihu ilitimizwa na Kristo. Sabato, Miandamo ya Mwezi na mpangilio wa Sikukuu hazikuondolewa.

Sikukuu ya Mwezi Mpya ziliadhimishwa sawa na Sabato kuu au Sabato Takatifu. Dhabihu zilitolewa kama tulivyoona hapo juu kama kumbukumbu.

Hesabu 28:11-15 inasema:

11 Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsongezea BWANA sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng’ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana kondoo waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba; 12 pamoja na sehemu ya kumi tatu za efa ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta, kwa kila ng’ombe ;na sehemu ya kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa huyo kondoo mume mmoja; 13 na sehemu ya kumi moja ya unga mwembamba na mafuta kuwa sadaka ya unga kwa kila mwana kondoo; kuwa sadaka ya kuteketezwa ya harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto, 14 Tena sadaka zote za vinywaji zitakuwa nusu ya hini ya divai kwa ng’ombe, na sehemu ya tatu ya hini kwa kondoo mume, na robo ya hini ni kwa mwana kondoo, hii ndio sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi katika miezi yote ya mwaka. 15 Tena mbuzi mmoja kuwa sadaka ya nadhiri kwa BWANA itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.

Tunajua kutokana na maandiko hapo juu kuwa Mwezi Mpya ulikuwepo katika miezi yote ya mwaka. Sharti kama hilohilo kufanywa kwa Mwezi Mpya kama inavyofanyika katika Sikukuu nyingine na Sabato.

1Nya.23:31 inasema:

31 na kumtolea BWANA sadaka zote za kuteketezwa, katika siku za Sabato, na mwezi mpya na sikukuu zilizoagizwa, kwa hesabu, kadiri ya agizo lake, daima mbele za BWANA

Mwezi Mpya zinafungamana kati ya Sabato na Sikukuu.

2 Nyakati.31:3 inasema:

3 tena akaweka sehemu ya mfalme ya mali zake kwa sadaka ya kuteketezwa, yaani, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na sadaka za kuteketezwa za Sabato na mwezi mpya na sikukuu, kama ilivyoandikwa katika torati ya Musa.

Ezra 3:5 vilevile inasema kuwa Miandamo ya Mwezi ilifanywa upya. Yote mawili, marejesho makuu yatahusisha marejesho ya Mwezi Mpya.

Ezra 3:5 inasema: 

5 Na baadae sadaka ya kuteketezwa ya daima, na za mwandamo wa mwezi, na za sikukuu za BWANA, zilizoamriwa na kuwekwa wakfu, na za kila mtu aliye mtolea BWANA sadaka kwa hiari yake.

Muandamo wa Mwezi ndio mwanzo au ni siku ya kwanza ya mwezi (Hes.10:10; 28:11). Kalenda ya Mwandamo wa Mwezi,ni alama ya Watu Watakatifu. Katika nukuu zake za Kutoka 12:2, Melkita anasema kuwa “mataifa” wanatambuliwa kwa jua lakini Israeli kwa mwezi (Zab.104:19). Sabato na Mwezi Mpya zote kunatakiwa kupumzika na kazi kama tusomavy Amosi 8:5 yapaswa iwe siku ya kufurahia. Vicheko vivyokusudiwa kusikika Siku Takatifu, Mwezi Mpya na Sabato viliondolewa.

Hosea 2:11inasema:

11 Tena nitaikomesha furaha yake yote, na sikukuu zake, na siku zake za mwandamo wa mwezi, na Sabato zake na makutaniko yake yote yaliyo amriwa.

Hii ni kwa sababu ya kutokuwa waaminifu kwao na ibada ya sanamu. Mungu huwaangamiza watu wake kwa sababu hawakuzishika sheria zake. Hatimaye ni kwamba aliuharibu utajiri wa taifa.

Hosea 2:12 inasema:

12 Nami nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake, ambayo alisema, Hii ndio ujira wangu niliopewa na wapenzi wangu; nami nitaifanya kuwa misitu, na wanyama porini wataila

Mwanzo 1:14 inaonyesha kuwa Mungu aliweka mwanga katika mbingu ili kufanya tofauti kati ya mchana na usiku na kama ishara ya majira. Mwezi Mpya hutupa utaratibu na muda wa sikukuu na hasahasa hutanguliwa na Sabato, ambayo husimamia tando la kukamilisha siku saba, wakati Miezi huanzia kutoka siku ya nne. Nuru hutenga nuru na giza (Mwa.1:18). Mwezi huashiria nuru ya nuru ya ulimwengu katika giza ambalo huitawala. jua lilitumia kufananisha na Kristo.

Malaki 4:2-4 inasema:

2 Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini. 3 Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika siku ile niifanyayo, asema BWANA wa majeshi. 4 Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi wangu niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam amri na hukumu.

Kumcha Bwana ni kukumbuka sheria za Mungu. Sabato na Mwezi Mpya ziliadhimishwa kwa namna moja moja bila kusahau jinsi ipasavyo kufanya na mishughuliko yetu. Jinsi tupasavyo kufanya katika shughuli za biashara kuhusu kuto nunua wala kuuza, na zilikatazwa kwa siku zote mbili Mwezi Mpya na Sabato.

Amosi 8:4-6 inasema:

4 Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nalikuwa sina habari; kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyizia sanamu, kusudi wakatiliwe mbali. 5 Amemtupa ndama yako, Ee Samaria; hasira yangu imewaka juu yao; siku ngapi zitapita kabla ya hao kupata hali isiyokuwa ya hatis? 6 Maana katika Israeli kimetokea hata na kitu hiki; fundi ndiye aliyekifanya, nacho si mungu kamwe; naam, ndama ya Samaria itavunjika vipande vipande.

Jumla ya miezi iko kumina miwili pamoja na wa kumi na tatu au mwezi usio wa kawaida unaoongezewa mara saba katika kila mzunguko wa miaka kumi na tisa, ya mwaka na ni wa muhimu kwa mujibu wa Kutoka 12:1. mafuatano ya kalenda kama ilivyoanzishwa na Mungu katika uumbaji inaamuluwa na mfumo wa mbinguni. Mwenendo na nafasi ya mfumo wa mbinguni ndio kitu cha kweli kutuamulia kwa kalenda. Hii yaweza kuonekana katika maendeleo ya Biblia na kiini cha sheria zake.

Zaburi 104:19 inasema:

Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati,

Jua latambua kuchwa kwake.

Mwezi ni kitu chenye kutoa maamuzi na sio jua. Jua hufanya kazi zake usiku tu na ni mhimili kutoka mwanzo wa mwaka kwa mujibu wa majira ya jua kupita Ikweta au majira ya mabadiliko ya mwaka katika Mwanzo34:22, kwa mujibu wa SHD 8622, neno {tek-oo-faw}  au {tekquphah}, lina maana ya:

Katika Israeli na watu wote katika nchi za Kaskazini, kipindi cha baridi cha jua kuwa katika ncha za kaskazini ya mistari ya latitude huwa mwezi Desemba wakati jua linafika katika latitude za juu za kusini ya mbali. Kipindi hiki tunakuwa na masaa machache sana ya mchana na mchana mfupi sana hasahasa karibu katikatarehe ya 21/22 Desemba. Majira ya hari huwa mwezi Juni wakati jua linapita latitude za Kaskazini sana mwa dunia. Majira haya tunakuwa na usiku mrefu sana, hasahasa huwa ni tarehe 21/22 Juni

Majira ya baridi ambayo usiku na mchana huwa sawa ni mwezi March wakati jua linapita katika msitari wa Ikweta likitokea katika kizio cha Kaskazini ya Dunia. Majira ya mchana na ya usiku huwa sawa wakati huu. Hutokea hasa kwenye tarehe za 20/21 Machi. Kipindi cha tatu cha usiku na mchana kuwa sawa, ni mwezi Septemba wakati jua linipopita tena katika mstari wa Ikweta linapotokea kizio cha Kasikazini kwenda Kusini ya Dunia. Mchna na usiku huwa karibu na urefu sawa. Hutokea hasa kwenye tarehe za 21/22 Septemba.

Mwaka wa Kitropiki ina siku 365.24219 na ule mwezi wa pili huwa na siku 29.53059. Miaka ya kumi na tisa ya kitropiki au yenye jua kali inafungwa na hesabu kamili ya miezi ya kisidoni au ya mwezi wa pili mrefu. Urefu halisi wa mwaka unaweza kutofautiana kwa dakika kadhaa ambako husababishwa na mvuto wa nguvu za asili za mvutano kutoka katika sayari nyingine. Ni sawa na kusema, muda wa kati ya miezi miwili mipya waweza kutofautiana kwa masaa kadhaa kwa sababu ya idadi ya mambo kukiwemo mabadiliko ya nguvu za asili za mvutano kati ya jua na mwelekeo wa mhimili wa mwezi.

Mwaka wa kumi na tisa unaweka hesabu ya ukamilifu wa mzunguko mmoja. Kipindi hiki huamuliwa na miandamo yenyewe ya miezi, kadiri inavyo zunguka kupitia majira mbali mbali. Kuna jumla ya miaka kumi na tisa kukamilisha mzunguko huu.

Kuliweka katika matendo

Miandamo ya Mwezi yapaswa kuadhimisha kwa mujibu wa sheria (Hes.10:10, 28:11-15; 1Nya.23:31; 2Nya.2:4, 8:13, 31:3). Biashara inabidi zisimame kipindi hiki kama ilivyo kwa siku za Sabato (Amosi 8:5). Israeli walishika Miandamo ya Mwezi (Isa.1:13-14; Ezra 3:5; Neh.10:33; Zab.81:3; Hos.2:11) kama lilivyofanya Kanisa kwa karne na karne . kanisa lilishika Miandamo ya Mwezi na Sabato na Siku Takatifu (Kol.2:16). Mwezi Mpya utakuwa unaadhimishwa katika marejesho kipindi cha majilio ya Masihi (Isa.66:23; Eze.45:17, 46:1, 3, 6) kama Sabato, na ni za lazima kwetu sasa. Mwezi Mpya iliamriwa kuadhimisha hata kabla ya Siku Takatifu ambazo zilianzishwa kama kwa wakati wake. (Zab.81:3). Hii ni kwa mujibu wa mwingiliano wa mzunguko wa mwezi na nyota na sio kwa mujibu wa maadhimisho (Zab. 104:19).

Siku Takatifu Na Sikukuu

Siku Takatifu za kila mwaka zinapatikana katika Walawi 23:1-44, Hesabu 28:16-29, 35 na katika Kumbukumbu la torati 16:1-16. Siku hizi Takatifu za kila mwaka ni za lazima kuziadhimisha kwa kuweka kutaniko takatifu (Law.23:4). Ni za kukumbukwa (Law.23:43) na nikioo cha mpango wa wokovu wa Bwana.

Siku hizi Takatifu ni:

Pasaka (Law. 23:7; Hes.28:18);

Siku ya Mikata isiyotiwa Chachu (Law.23:8; Hes.28:25);

Pentekoste (Law.23:21;  Hes.28:26);

Baragumu (Law.23:23; Hes.29:1);

Upatanisho (Law.23:26; Hes.29:7)

Vibanda (Law.23:35; Hes.29:12);

Siku Iliyokuu ya Mwisho (Law.23:36; Hes.29:35).

Kuna jumla ya sikukuu tatu kuadhimishwa kila mwaka (Kut.23:14). Majira ya maadhimisho ya sikukuu hizi yamepangiliwa katika umakini mkubwa (Ezra 3:5; Neh.10:33) Neno hili pangiliwa linatokana na mow’ed (SHD4150) lina maana ya “wakati ulio wekwa” na hauwezi “kubadilishwa” au kuahirishwa.

Ya kwanza ni Sikukuu ya Mikate isiyotiwa Chachu ambayo ina Siku mbili Takatifu, Pasaka katika siku ya kumi na tano na vilevile ni siku ya mwisho ya Mikate isiyotiwa Chachu katika siku ya ishirini na moja ya mwezi wa kwanza wa Nisan (Abib).

Ya pili ni Sikukuu ya Mavuno au Majuma au Siku Takatifu ya Pentekoste (Kut.23:16) ambayo ni siku hamsini kufuatia Sadaka ya Mganda wa Kutikisa katika siku ya kwanza ya juma, Jumapili ya Kirumi, katika Mikate isiyotiwa Chachu.

Ya tatu ni Sikukuu ya Vibanda au Makusanyo (Kut.23:16) katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba ambapo ni Siku Takatifu sawa na kama mojawapo ya Siku Iliiyokuu ya Mwisho kama siku ya tisa ya Sikukuu hii.

Utaratibu wa utoaji zaka unahusishwa na sikukuu na inaendana na utaratibu wa Ybile.

Kumbukumbu la torati 14:22-29 inasema:

22 Wana wa Israeli wakaenda ndani ya bahari katika nchi kavu; nayo maji yalikuwa ukuta kwao mkono wa kuume na mkono wa kushoto. 23 Na wale Wamisri wakawafuatia, wakaingia ndani kati ya bahari, farasi zote za Farao, na magari yake, na wapanda farasi wake. 24 Ikawa katika zamu ya alfajiri, BWANA akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto nay a wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri. 25 Akayaondoa magurudumu ya magari yao, hata wakaenda kwa uzito; na Wamisri wakasema, Na tukimbie mbele ya Israeli; kwa kuwa BWANA anawapigania, kinyume cha Wamisri. 26 BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya Bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao. 27 Musa akaunyoosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake, na BWANA akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari. 28 Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; halikusalia hata mtu mmoja. 29 Lakini wana wa Israeli wakaenda katika nchi kavu katikati ya bahari; na hayo maji yalikuwa ni makuta upande wao wa kuume, na upande wao wa kushoto.

Zaka ya pili hutumika kwa ajili ya ushiriki wa kwenye Sikukuu. Sikukuu yaweza kuwa isiandaliwe katika maeneo ya nyumbani au katika malango (mjini) yako, isipokuwa pale ambapo umbali ni mkubwa. Pasaka imeandaliwa (Kum.16:5-7).

Kumbukumbu la torati 12:21 inasema:

21 Na mahali atakapo chagua BWANA, Mungu wako, apaweke jina lake, pakiwa mbali nawe mno, ndipo utakapochinja katika kundi lako la ng’ombe alilokupa BWANA, kama nilivyokuagiza, nawa utakula ndani ya malango yako, kwa kufuata yote yanayotamani roho yako.

Wale ambao hawakujiandaa kuila Pasaka, au wanaosafiri, itawabidi kuila Pasaka katika mwezi unaofuata (Hes.9:6-12; 2Nya.30:24).

Hesabu 9:1-23 inasema:

Kisha BWANA akanena na Musa katika bara ya Sinai, mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya kutoka kwao katika nchi ya Misri, akamwambia, 2 Tena, wana wa Israeli na washike sikukuu ya Pasaka kwa wakati wake ulioagizwa. 3 Siku ya kimi na nne ya mwezi huu, wakati wa jioni, mtaishika kwa wakati wake ulioagizwa; kwa amri zake zote, na kama huku zake zote zilivyo, ndivyo mtakavyoishika. 4 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli kwamba waishike sikukuu hiyo ya Pasaka. 5 Nao wakaishika Pasaka katika mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika bara ya Sinai; vilevile kama hayo yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli. 6 Basi walikuwako watu waume kadha wa kadha waliokuwa na unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu, hata wasiweze kuishika Pasaka siku hiyo; nao wakaenda mbele ya Musa na Haruni, siku hiyo; 7 hao watu wakamwambia, Sisi tu hali ya unajisi kwa ajili ya maiti ya mtu; nasi tumezuiwa kwa nini hata tusipate kumtolea BWANA kwa wakati wake ulioagizwa, kati ya wana wa Israeli? 8 Musa akamwambia, Ngojeni hapo; hata nipate sikiza BWANA atakalo agiza juu yenu. 9 BWANA akanena na Musa, akamwambia, 10 Nena na wana wa Israeli, na kuwaanbia, Mtu wa kwenu, au wa vizazi vyenu, yeyote atakayekuwa na unajisi kwa ajili ya maiti, au akiwako mbali katika safari, na haya yote, ataishika Pasaka ya BWANA; 11 mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu; 12 wasisaze kitu chochote hata asubuhi, waka wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika. 13 Lakini mtu aliye safi, wala hakuwa katika safari, naye amekosa kuishika Pasaka, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake; kwa sababu hakumtolea BWANA matoleo kwa wakati wake ulioamriwa, mtu huyo atachukua dhambi yake. 14 Na kama mgeni akiketi kati yenu ugenini, naye ataka kuishika Pasaka kwa BWANA; kama hiyo sheria ya Pasaka ilivyo, na kama amri, ndivyo atakavyofanya; mtakuwa na sheria moja, kwa huyo aliye mgeni, na aliyezaliwa katika nchi.15 Na siku hiyo maskani itasimamishwa, lile wingu litaifunika maskani, yaani, hema ya kukutania; wakati wa jioni likawa juu ya maskani, mfano wa moto, hata asubuhi. 16 Ndivyo ilivyokuwa siku zote; lile wingu liliifunika kwa mfano wa moto usiku. 17 Na lika lilipoinuliwa lile wingu juu ya ile Hema, ndipo wana wa Israeli waliposafiri; na mahali lilipokaa lile wingu, ndipo wana wa Israeli walipopiga kambi yao. 18 Kwa amri yaBWANA wana wa Israeli walisafiri, na kwa amri ya BWANA walipiga kambi; wakati lile wingu lilipokaa juu ya maskani walikaa katika kambi yao. 19 Na lile wingu lilipokawia juu ya maskani siku nyingi, ndipo wana wa Israeli walipolinda malinzi ya BWANA wala hawakusafiri. 20 Na pengine lile wingu lilikaa juu ya maskani siku chache; ndipo kwa amri ya BWANA walikaa katika kambi yao, tena kwa amri ya BWANA walisafiri. 21 Na pengine lile wingu lilikaa tangu jioni hata asubuhi; na lile wingu lilipoinuliwa asubuhi walisafiri, au kama lilikaa usiku na mchana pia, lilopoinuliwa lile wingu, ndipo waliposafiri.

Ni muhimu kwa kila mmoja kuishika Pasaka, hata kwa wageni wanaoishi katika Israeli wanapaswa pia washerehekee Pasaka (Kut.12:48; Hes.9:14).

Kutoka 12:29-51 inasema:

29 Hata ikawa, usiku wa manane BWANA akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama. 30 Farao akaondoka usiku, yeye na watumishi wake wote, na Wamisri wote; pakawa na kilio kikuu katika Misri; maana hapakuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu. 31 Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni, tokeni katika watu wangu, ninyi na wana wa Israeli; enendeni, kamtumikieni BWANA kama mlivyosema. 32 Twaeni kondoo zenu na ng’ombe zenu kama mlivyosema, enendeni zenu, mkanibariki mimi pia. 33 Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, Tumekwisha kufa wote. 34 Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabegani. 35 Wana wa Israeli wakafanya kama neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi. 36 BWANA akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walicho kitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara. 37 Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu sita mia elfu watu waume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto. 38 Na kundi kubwa la watu waliochangamana nao wakakwea pamoja nao; na kondoo na ng’ombe, wanyama wengi sana. 39 Nao wakaoka mikate isiyochachwa na ule unga waliouchukua walipotoka Misri, maana, haukutiwa chachu, kwa sababu walitolewa watoke Misri, wasiweze kukawia, nao walikuwa hawajajifanyia tayari chakula. 40 Basi wana wa Israeli kukaa kwao, maana, muda waliokaa ndani ya Misri, ulikuwa ni miaka mia nne na thelathini. 41 Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ileile, ya kwamba majeshi yote ya BWANA yalitoka nchi ya Misri. 42 Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za BWANA kwasababu ya kuwatoa katika nchi ya Misri; huu ndio usiku wa BWANA, ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israeli wote katika vizazi vyao. 43 BWANA akawaambia Musa na Haruni, Amri ya Pasaka ni hii; mtu mgeni asimle; 44 lakini mtumishi wa mtu awaye yote aliye nunuliwa kwa fedha, akisha kumtahiri, ndipo hapo ataila Pasaka. 45 Akaaye kwenu hali ya ugeni, na mtumishi aliye ajiriwa, wasimle Pasaka. 46 Na aliye ndani ya nyumba moja; usiichukue nje ya nyumba nyama yake yoyote; wala usivunje mfupa wake uwao wote. 47 Na wafanye jambo hili mkutano wa Isrtaeli wote. 48 Na mgeni atakapoketi pamoja nawe, na kupenda kumfanyia BWANA Pasaka, waume wake wote na watahiriwe, ndipo hapo akaribie na kufanya pasaka; naye atakuwa mfano mmoja na mtu aliyezaliwa katika nchi; lakini mtu yeyote asiye tahiriwa asimle. 49 Sheria ni hiyo moja kwa mtu aliyezaliwa kwenu, na kwa mgeni akaaye kati yenu ugenini. 50 Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli wote; kama BWANA alivyowaagiza Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya. 51 Ilikuwa siku ileile moja, BWANA akawatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri kwa majeshi yao.

Wokuvu wao hujumlisha wokovu wa mataifa, kwa maana ya wote wenye mwili, ambao watakuwa kwenye kutaniko. Kama umebatizwa na kupokea Roho Mtakatifu, basi umesha tahiriwa na uko safi.

Sikukuu yapaswa isherehekewe mahali ambapo Mungu amepachagua (kupitia ukuhani) (Kum.16:5-7) na inatakiwa isherehekewe na mkate usiotiwa chachu (Kut.12:8, 15-20, 12:3, 6; 23:15; Law.23:6; Hes.9:11; 28:17; Kum.16:3, 4; Mk.14:12; Lk.22:7; Mdo.12:3; 1Kor.5: 8). Hukumu ya kupuuzia kuadhimisha sikukuu ni kukutiliwa mbali na watu wako au na kutaniko la Bwana, (Hes.9:13) isipokuwa kwa asiye safi au aliyesafiri. Kuna sheria mbili kufanywa na mgeni au na msafiri (Hes.9:14) na hairuhusi kuadhimishwa nyumbani.

Kumbukumbu la torati 16:5-7 inasema:

5 Usimchinje pasaka ndani ya malango yako yote rkupayo BWANA, Mungu wako; 6 ila mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, ndipo mtakapo mchinja pasaka jioni, katika mwachweo ya jua, kwa wakati kama uliotoka Misri. 7 Nawe umwoke na kumla atakapochagua BWANA, Mumgu wako, kasha asubuhi yake uende hemani mwako.

Sheria ya Kumbukumbu 16:5 ilikuwa ndio sababu Kristo alituma wanafunzi kutafuta na kuandaa chumba kama inavyosema Mathayo 26.

Mathayo 26:17-19 inasema:

17 Hata siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi wake wakamwendea Yesu, wakamwambia, Ni wapi utakapo tukuandalie uile pasaka? 18 Akasema, Enendeni mjini kwa mtu Fulani, mkamwambie, Mwalimu asema, Majira yangu ni karibu, kwako nitafanya Pasaka pamoja na wanafunzi wangu. 19 Wanafunzi wakafanya kama Yesu alivyowaagiza, wakaiandaa Pasaka.

Katika Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa, ishara ya Yona ililazimu itimilike kikamilifu katika maeneo yake yote. Sehemu ya kwanza ni kwamba Kristo alikuwa kaburini kwa muda wa siku tatu za mchana na siku tatu za usiku zisizidi wala zisipungue. Kristo pia alibidi afufuke kabla ya asubuhi ya siku ya kwanza ya juma, siku inayofuatia Sabato ya wiki, kwa sababu ni sadaka ya kutikiswa, ambao ulikuwa ni malimbuko ya mavuno (Kut.29:24-27; pia ona Law.7:30, 34, 8:27, 29, 9:21; 10:14, 15; 14:12, 24; 23:11-20; Hes.5:25, 6:20; 18:11, 18).

Kutoka 29:24-27 inasema:

24 Nawe utavitia hivi vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe; utavitikisa-tikisaviwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA. 25 Kisha uvitwae vile vitu mikononi mwao, na kuviteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa, view harufu nzuri mbele za BWANA, ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto. 26 Kisha twaa kidari cha huyo kondoo wa kuwekwa kwake Haruni  kwa kazi takatifu, na kukitikisa-tikisa kiwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; nacho kitakuwa ni sehemu yako. 27 Nawe kitakase kile kidari cha ile sadaka ya kutikiswa, na lile paja la sadaka ya kuinuliwa, lililotikiswa, na lilio inuliwa juu, vya yule kondoo na kuwekwa kwa kazi takatifu, huyo aliyekuwa kwa ajili ya Haruni, na huyo aliyekuwa kwa ajili ya wanawe;

Mganda wa Kutikiswa, kwa kawaida ulikuwa unatolewa saa 3 asubuhi. Alikuwa anasuburia kupaa juu, na ndio maana Kristo alimwambia Mariamu alipokuja kumuona kuwa “usinishike”.

Yohana 20:1, 15-17 inasema:

1 Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalena alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini. 15 Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtauta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa. 16 Yesu akamwambia, Mariamu, yeye akageuka, ahamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (yaani, mwalimu wangu). 17 Yesu akamwambia, Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.   

Mara tu baada ya kukubalika kwake kama dhabihu na baadae kurudi ndipo aliporuhusu mwenyewe kuguswa (Yoh.20:27).

Siku ya kwanza ya juma, au Jumapili ya Sadaka ya Mganda wa Ktikiswa sio Siku Takatifu ila inapasa itunzwe kama inavyoanza kufanyiwa hesabu kuelekea Pentekoste.

Si Siku Takatifu ya Baragumu au ya Upatanisho iliyo sehemu ya sikukuu inayoshirikishwa na utaratibu wa utoaji wa sadaka.

Kuna Sikukuu tatu kwa mwaka.

Kutoka 23:14 “Mara tatu kila mwaka utaniwekea sikuu.”

Ziko katika

Kumbukumbu la torati 16:16 “Mara tatu kwa mwaka na watolee wanaume wako wote mbele za BWANA, Mungu, wako mahali atakapochagua; katika idi ya mikate isiyotiwa chachu, na katika idi ya majuma, na katika idi ya vibanda; wala wasitokee mbele za BWANA mikono mitupu.

Wale wanaohudhuria Sikukuu wasiende mbele za BWANA, Yehova mikono-mitupu:

Kumbukumbu la torati 16:17 inasema:

17 Kila mtu na atoe kama awezavyo, kwa kadiri yabaraka ya BWANA, Mungu wako, aliyokupa.

Kuna nyakati tatu kwa mwaka za kutoa sadaka. Hii inabidi ifanyike mwanzoni kabla ya asubuhi ya kila siku ya kila mojawapo ya Sikukuu hizi.

Kutoka 23:18 inasema:

18 Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate usiotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi.

Sadaka hizi zilizoamriwa haitakiwi zidaiwe kwa nguvu toka kwa Wakristo wajapo kwenye kila Siku Takatifu hizi, au kwenye makutaniko ya kila juma. Sadaka ya moyo wa hiyari ni siri kati ya mtu binafsi na Mungu na yaweza kutolewa wakati wowote, lakini yapasa itolewe bila aina yoyote ya shinikizo au shuruti.

Baragumu inaitwa Sabato ya Ukumbusho na Makusanyo Matakatifu (Law.23:24). Upatanisho huitwa Sabato ya Sabato na Kutaniko Takatifu (Law.23:27-32). Zote mbili huitwa siku [Takatifu] na sio sikukuu.

Hesabu 10:10 huelezea mazingira ambayo baragumu zilikuwa zinapolizwa. Inasema kuwa siku zote za Mwezi Mpya na Siku zote Takatifu na Sabato wakati sadaka za kuteketezwa na za amani zikitolewa.

Siku Takatifu na Sikukuu za Kibiblia zinapatikana katika Walawi 23 na kule tunakuta maelekezo yote kuliko maelendelezo ya kitabu cha Kutoka. Kutoka 23 inaendeleza ilivyo katika Kutoka 20 na Walawi 23 ikisisitiza ya kitabu cha Kutoka. Hesabu 15, 28 na 19 inasisitiza yote mawili pamoja na Mwezi Mpya. Marudio mengi sana na msisitizo huonekana katika Kumbukumbu la torati 5 na 14. Uweza wa Kristo unategemeana na uwezo wa kushika sheria katika Roho Mtakatifu na hivyo, kwa neema. Kristo alishika Sabato zote, Miandamo ya Mwezi na Sikukuu (Kol.2:16) sawa na kanisa kwa kipindi cha karibu miaka elfu mbili. Mataifa wakati wa Milenia, vilevile watazishika Sabato, Mwezi Mpya na Sikukuu (Isa.66:23; Zek.14:16-19).

Uhusiano kati ya sikukuu hizi na dhabihu yaonekana katika Kumbukumbu la torati 12:8-14 zilihalifiwa pamoja na mahusiano kati ya dhabihu na Sabato za kila wiki. Haziwezi kuhusiana na sikukuu na sheria ya dhabihu bila ya tendea kazi wazo hilohilo katika mitazamo mingine yote ya sheria, ikiwemo Sabato. Mifumo yote ya tawala za Mungu iliweka huru kutoka na taratibu za dhabihu ikijumlisha taratibu za Sabato na Siku Takatifu. Pasaka yenyewe ilianzishwa kabla hata sheria hazijatolewa pale Sinai. Kristo ni dhabihu ya Pasaka na hakuna dhabihu ya mnyama ambayo inaweza kutolewa leo ili ifunike dhambi zetu.

Mlolongo wote wa kuwaingiza wateule katika Ukristo unategemeana na mafuatano yanayojitokeza hadi ufufuko wa wote. Siku takatifu haziwezi kukomeshwa hadi Siku iliyokuu ya Mwisho ikamilishe sehemu ya mpango huu. Kila sikukuu huwakilisha sehemu ya mpango wa Mungu ambao hadi sasa umekuwa katika fumbo. Sheria zilikuwa ni kivuli cha mambo yajayo (Ebr.10:1). Kivuli huonyesha ukweli; hakiwezi kutenganishwa.

Kivuli kilifungamanishwa kirasmi na dhabihu (Ebr.10:1-10), na sio kwa sikukuu. Biblia inasema kuwa mapungufu katika husababishwa na wale walio katika mwili wanaojitoa nafsi zao kutumikia makosa ya Balaam na kuangamia katika uasi wa Kora (Yuda 1:11-12). Kwa maneno mengine, hufundisha kwa malipo na hugeuza sikukuu na ufahamu wa sheria na ushuhuda. Hakuna nuru (Isa.8:20 Biblia ya KJV) au mapambazuko (RSV) ndani yao. Wamekufa mara mbili na kukatiliwa mbali. Watu hawa, bila ya Roho, wanaosababisha matengano katika siku hizi za mwisho (Yuda 1:19) ufahamu wa sheria huleta na hufanya mzingo akilini na mioyo ya kila mmoja wao.

Suala hapa sio Sabato, au Mwezi Mpya au Sikukuu, wala sio Sheria katika kushika maagano. Ni ukweli kuwa Mungu Baba ni Mungu Mmoja na Wapekee (Yoh.17:3; 1Yoh.5:20) na kwamba ni yeye tu pekeyake huishi milele (1Tim.6:16).

Mtu anaweza kuishika Sabato na bado akawa unaamini na kutumikia mafundisho mapotovu ya uwongo. Kama hutaishikilia kweli utaondolewa katika kundi la wateule kuingiwa na nguvu za upotevu na kuuamini uongo (2The.2:11). Marshall’s Interlinear imetafsiri aya hii kuwa operesheni ya upotovu ili wauamini uongo. Hawawezi kujisaidia tena wenyewe. Hawawezi kuelewa hatakama wangependa kuyaona makosa yao. Mpango na kusudi la Mungu, vimefunuliwa kwa mfumo na mafuatano ya sikukuu, na vimeanzishwa kama sheria katika Biblia.

Ukristo wa mfumo wa kimambo leo hauna habari kuhusu kuadhimisha sikukuu hizi na kwa bahati mbaya, bila kufuata maelekezo na ufahamu kutoka katika mpango wa kibiblia. Makanisa haya mamboleo hudhrau maelekezo ambayo Biblia imeamuru kwaajili ya kulinda jamii kupitia utaratibu wa familia. Serikali zetu kuu haziwezi kuchukua mahali pa familia na kulinda mfumo wa Yubile ya ardhi. (Mik.4:3-4).

Sheria zinazosimamia sikukuu zimeandikwa katika mipangano minne katika vitabu vya Torati ya Musa kuanzia kitabu cha Kutoka hadi Kumbukumbu la torati. mpangilio wa kwanza unapatikana katika kitabu cha Kutoka zaidi ya sura nyingi. Kutoka 20 inahusika na amri za Mungu ambazo zimerudiwa katika Kumbukumbu 5. Kutoka 21 inashughulika na maswali ya ndoa na mambo ya nyumbani na majukumu ya familia, ambayo inaendeleza utaratibu wa amri za Mungu katika kila aina ya jamii. Kutoka 22 inashughulika na ongezeko la haki ya mali ya mtu na kanuni yake chini ya amri hizi. Kutoka 23 inashughulika na juu ya ushahidi wa uwongo na jinsi ya kulinda heshima ya na maendelezo ya amri ya.kumi. Kutoka 23:10, kasha inachukua amri ya nne na kuieneza ili kuonyesha utendaji wake katika utaratibu wa jamii. Sio tu kuwa inahusiana na wiki, mahusiano yake na Yubile na utaratibu mzima wa kisabato. Kutoka 12 ilishughulika na Pasaka.

Hizi ndizo zilikuwa sikukuu za Bwana na aliziita Sikukuu zangu (Law.23:2). Zinanenwa kuwa ni Sikukuu za Bwana katika Walawi 23 na 2Nyakati 2:4. Usemi wa sikukuu zunu ulitumika pia katika Hesabu 15:3 na 29:39. Usemi sikukuu zao umetumika katika Isaya 1:14 na 5:12 katika sura tofauti na hapo chini. Sikukuu hizi sio za kidunia au sio za wana wa ulimwengu huu au hazikuanzishwa kwa utaratibu wa kidunia. Haziwezi kubadilishwa kwa sababu yoyote ile au kuachwa hadi pale mpango wa wokovu, ambao kwayo uliwakilisha, ubadilishwe au uachwe.

Walawi 23:1-44 inasema:

Kasha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2 Nena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Sikukuu za BWANA, ambazo mtazipigia mbiu kuwa ni makusanyiko matakatifu; hizi ni sikukuu zangu. 3 Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu, msifanye kazi ya namna yoyote; ni Sabato kwa BWANA katika makao yenu yote. 4 Sikukuu za BWANA ni hizi, ni makusanyiko matakatifu, ambayo mtayapigia mbiu kwa nyakati zake. 5 Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi wakati wa jioni ni Pasaka ya BWANA. 6 Na siku ya kumi na tano ya mwezi uleule ni sikukuu kwa BWANA ya mikate isiyotiwa chachu; mtaila mikate isiyo chachwa muda wa siku saba. 7 Siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yoyote ya utumishi. 8 Lakini mtasongeza sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto siku saba; siku ya saba ni kusanyiko takatifu; msifanye kazi yoyote ya utumishi. 9 Kasha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 10 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapo mletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu; 11 naye atautikisa mganda mbele za BWANA ili kwamba ukubaliwe mbele yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa. 12 Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana kondoo wakiume mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA. 13 Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu ya kumi mbili za efa ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya kinywaji itakuwa divai, robo ya hini . 14 Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapo kuwamkwisha kuleta sadaka kwa Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote. 15 Nanyi mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya Sabato, tangu siku hiyo mliyouleta mganda wa sadaka ya kutikiswa; zitatimia Sabato saba; 16 hata siku ya pili ya hiyo Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea BWANA sadaka ya unga mpya. 17 Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu ya kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa BWANA. 18 Nanyi, pamoja na hiyo mikate, mtatongeza wana kondoo saba, walio wakamilifu, wa mwaka wa kwanza, na ng’ombe mume mmoja, na kondoo waume wawili; watakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA, pamoja na sadaka yao ya unga, na sadaka zao za kinywaji, sadaka ya harufu ya kupendeza iliyo songezwa kwa BWANA kwa njia ya moto. 19 Namyi mtasongeza mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wana kondoo wawili waume wa mwaka wa kwanza kuwa dhabihu ya sadaka za amani. 20 Kisha kuhani atawatikisa pamoja na hiyo mikate ya malimbuko kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA, pamoja na wale kondoo wawili; watakuwa watakatifu kwa BWANA, wawe na huyo kuhani. 21 Nanyi, mtapiga mbiu siku iyohiyo; kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; msifanye kazi yoyote ya utumishi; ni amri ya milele katika makao yenu yote, katika vizazi vyenu. 22 Nanyi hapo mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, usivune kabisa kabisa pembe za shamba lako, wala msiyakusanye masazo ya mavuno yako; utayaacha kwa ajili ya huyo maskini, na mgeni; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 23 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 24 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mwezi wa saba siku ya kwanza ya mwezi, kutakuwa na kustarehe kabisa kwenu, ni ukumbusho wa kuzipiga baragumu, ni kusanyiko takatifu. 25 Msifanye kazi yoyote ya utumishi; nanyi mtasongeza sadaka kwa BWANA  kwa njia ya moto. 26 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 27 Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtazitesa nafsi zenu; nanyi mtazisongeza sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto. 28 Nanyi msifanye kaziyoyote siku hiyo; kwa kuwa ni siku ya upatanisho, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za BWANA, Mungu wenu. 29 Kwa kuwa mtu awaye yote asiyejitesa mwenyewe katika siku iyo hiyo, atakatiliwa mbali na watu wake. 30 Na mtu yeyote afanyaye kazi ya namana yo yote siku hiyo, mtu huyo nitamwangamiza atoke katika watu wake. 31 Msifanye kazi ya nama yo yote; ni amri ya milele katika vizazi vyenu, katika makao yenu yote. 32 Itakuwa kwenu Sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtazitesa nafsi zenu; siku ya kenda ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hata jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu.  33 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 34 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu  ya vibanda muda wa siku saba kwa BWANA. 35 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu, msifanye kazi yoyote ya utumishi. 36 Mtamsongezea BWANA sadaka kwa moto; siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamsongezea BWANA sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yoyote ya utumishi. 37 Sikukuu za BWANA ni hizi, ambazo mtazipia mbiu ya kuwa ni makusaniko matakatifu, ili mumsongezee BWANA sadaka kwa moto, sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya unga, na dhabihu, na sadaka ya kinywaji, kila sadaka kwa siku yake; 38 zaidi ya hizo Sabato za BWANA, na zaidi ya matoleo yenu, na zaidi ya hizo nadhiri zenu zote, na zaidi ya sadaka zenu za hiari, ambazo mwampa BWANA. 39 Lakini siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, hapo mtakapokuwa mmekwisha kuyachuma mavuno ya nchi, mtaweka sikukuu ya BWANA muda wa siku saba; siku ya kwanza kutakuwa na kustarehe kabisa, na siku ya nane kutakuwa na kustarehe kabisa. 40 Nanyi siku ya kwanza mtajipatia matunda ya miti mizuri, na makuti ya mitende, na matawi ya miti minene, na mierebi ya vijitoni, nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu muda wa siku saba. 41 Nanyi mtaishika kuwa sikukuu kwa Bwana muda wa siku saba katika mwaka; ni amri ya milele katika vizazi vyenu; mtaishika katika mwezi wa saba. 42 Mtaketi katika vibanda kwa muda wa siku saba; wazalia wote wa Israeli wataketi katika vibanda; 43 Ili vizazi vyenu vipate kujua ya kuwa niliwaketisha wana wa Israeli katika vibanda, hapo nilipowawaleta kutoka nchi ya Misri; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 44 Naye Musa akawaambia wana wa Israeli hizo sikukuu za BWANA.

Masihi kwakweli alikuwa ni sehemu ya kwanza na muhimu ya mavuno ya Mungu, kama kielelezo cha Pasaka na Sadaka ya Mganda au ya Kutikiswa, lakini alikuwepo tangu mwanzo kama Elohim wa Israeli, akijinyenyekesha kwa Elohimu wake ambaye ni Eloah. Ni kwa uwezo huu alimpa sheria Musa ambaye alisema naye uso kwa uso.

Musa hakuongea na Mungu (Baba kama Eloah au Theon). Yohana anasema waziwazi kuwa hakuna mtu aliye wahi kumuona Mungu (ton Theon) wakati wowote (Yoh.1:18). Alikuwa ni huyu Elohim aliyetajwa kama Malaika Aliyeko au Malaika wa Shauri Kuu (Isa.9:6 LXX).

Mungu alitoa sikukuu kwa Kristo, na Kristo akaziagiza na kutoa miongozo yake kwa waleule wake na hatimaye kwa mataifa yote kwa utaratibu wa milenia. Hesabu 28 & 29 imebeba orodha kamili tu. Hii inajumlisha dhabihu au sadaka za kila siku, kila wiki, kila mwezi na kila mwaka. Dhabihu zilikuwa zinatolewa kulingana na vile jinsi tulivyo, ambayo ni dhambi za kurithi, na dhabihu zilikuwa zinatokewa kama malipo kwa maovu yote tuliyoyafanya.

Kristo ni yeye yule jana, leo kesho na hata milele (Ebr.13:8). Mungu hana kigeugeu (Mal.3:6; Yak.1:17). Wala habadiliki, kwahiyo, siku anazoshikilia kuwa takatifu kwa wanadamu kama walivyopewa na sheria hazibadiliki.

Sabato, Mwezi Mpya, Siku Takatifu na Sikukuu, zinapuuziwa kwa makusudi tu. Hii ni ahadi ambayo Mungu mwenyewe aliiweka kupitia manabii. Mungu alisema na nabii Amosi akiilinganisha Israeli katika siku hizi za mwisho na kapu la matunda wakati wa hari (Amosi 8:1). Kushindwa kumtii Mungu ni mwanzo wa mashaka. Hukumu ya kutotii Mungu ni kwamba Sabato na sikukuu zao kugeuka kuwa maombolezo.

Hii itafuatiwa na njaa ya kuto lisikia neon la Yehova (Amosi 8:11-14) kwasababu ya kukosa kuelewa asili ya Mungu wa Pekee wa Kweli (Yoh.17:3; 1Yoh.5:20) watu wanaangamia (Hos.8:5-9). Hata mapepo yanajua kuwa Mungu ni mmoja kwa kutetemeka (Yak.2:19). Mambo makuu katika sheria za Mungu yaliandishwa kwaajili ya Israeli. Walihesabia kama mambo mageni kwaajili ya uvunjaji wao wa amri ya kwanza na ongezeko la dhambi katika ibada (Hos.8:11-14).

Sura yote ya Yohana 6 ni mafuatano ya mifano inayotuongoza katika maandalizi na Pasaka. Kuna maana maalumu katika kila sentensi moja ya Yohana 6 na jinsi inavyomuandaa kila mtu kwa wito wao, mahala pao katika makabila kama sehemu ya wale 144,000 na umati chini ya mitume kumi na wawili katika kuyahukumu makabila.

Yohana 6:53-54 inasema:

53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua diku ya mwisho.

Kuna hatua tatu kufanya kwa ajili ya uzima wa milele. Mambo haya huwa kwa kawaida hayafanywi katika Ushirika wa Meza ya Bwana. Mambo mawili ya kwanza yanatoka katika Yohana 17:3.

Hatua ya kwanza   “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Hatua ya pili la uzima wa milele ni kumwamini Yesu Kristo katika ufahamu wa Mungu wa pekee wa kweli (1kor.15:34).

Hatua ya tatu la uzima wa milele ni kushiriki katika Pasaka na kushiriki kula mwili na damu ya Yesu Kristo kama (Yoh.6:53-54) isemavyo hapo juu.

Kuna hatua tatu, unayotakiwa kufanya ili kuuingia uzima wa milele. Hatua hizo zote tatu zinategemeana na utii. Utii ni kwa Mungu wa pekee wa Kweli kwa kuzishika amri zake (Kum.4:2,  6:17,  8:6,  10:13, 28:9; Zab.119:115; Mt.19:17). Kushindwa kuzishika sheria huleta hukumu.

Warumi 2:27 inasema:

Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikaye torati, je! Hatakuhukumu wewe, uliye na kutahiriwa, ukaihalifu torati?

Utunzaji wa sheria ni kanuni muhimu kwa kumruhusu Roho Mtakatatifu. Pasipo na Roho Mtakatifu huwezi kuuingia Ufalme wa Mungu na kuwa na uzima wa milele. Kwa hiyo ni kwa kupitia hatua hizi za imani. Kwahiyo unalazimika kushiriki utii. Utii kwa hizi sikukuu kunajiri utunzaji wa sheria na taratibu ambazo Kristo aliziweka kushiriki katika Pasaka. Kama hutashiriki tafrija hii, wewe huna ushirika na na Kristo (Yoh. 13:8).

Adhimisho la kwanza la Meza ya Bwana ni tendo la kuosha miguu. Kuosha miguu kulifanywa kama ni tendo la ukarimu kwa mwanyeji mgeni anapowasili. Kwa kawaida watu huwa wameshaoga kabla yake, lakini kwa ajili ya kutembea mitaani basi uoshaji miguu huwafanya wajisikie kuburudika. Ilikuwa ni kazi ya kufanywa na kijakazi aliye duni sana. Mgeni alweza kupewa taulo na balasi la maji. Tendo hili la kuosha miguu kwa kawaida hufanywa wakati ule mgeni anapowasili, au kabla ya kuanza kula, wakati wageni wamekaa mezani. Kukataa kufanya kazi hii kuliashiria ukweli kuwa hakuna mtu aliye tayari kujinyenyekesha kufanya kazi dhaifu, kuwatumikia wengine.

Yohana 13:6-8 inasema:

 6 Hivyo yuaja kwa Simon Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? 7 Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye. 8 Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.

Pengine sisi sote twaweza kuyafahamu maneno haya kutoka moyoni. Petro hakutaka amwoshe miguu yake kama Mfalme Masihi alivyotaka. Hakujua kuwa Kuhani Mkuu alitembea kwanza na vazi au nguo ya hariri ili kuombea watu msamaha na kutoa dhabihu. Ilibidi ziwepo aina mbili za majilio ya Kimasihi. Wakwanza ni ule wa unyenyekevu akivalia vazi la hariri na wa pili ni ule atakao vikwa mamlaka ya Kifalme. Alitaka kumweka Yesu Kristo katika kiti cha enzi cha Kaisari na kutawala dunia hii kama kidhalimu sawa kama Kaisari alivyokuwa anafanya, lakini toka Yerusalemu.

Petro akasema, “Wewe hutanitawadha miguu kamwe”!. Tunapaswa kuruhusu miguu yetu ioshwe, ni kiashirio kuwa maisha yetu yameoshwa na kutakaswa na Kristo katika mtazamo endelevu, kama tunataka kuwa na sehemu simony katika Ufalme wake na kwa kweli katika kila anachofanya. Kama tukifanya, tutaurithi Ufalme kama alivyofanya. Petro aliujua umuhimu wa tendo hili lakini sio ishara yake.

Yohana 13:9-11 inasema:

9 Simoni Petro akamwambia, Bwana, si muguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia. 10 Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote. 11 Kwa maana alimjua yeye atakaye msaliti; ndiyo maana alisema si nyote mliosafi.

Tunahitaji kuosha miguu yetu tu kama tulivyoingia mara moja tu katika maji ya ubatizo na hivyo kufanya kuwa tumetakasika mara moja na kwa milele. Ni katika wakati wa ameza ya Bwana tu tunahitajika kuosha miguu.

Kusema kweli katika roho ni kwamba, kila mwaka tunakusanya dhambi, wakati mwingine bila hujielewa, kadiri tuendeleavyo kupita mapito ya maisha, nahivyo tunahitaji kufanya upya yale maagano ya ubatizo. Tunatakiwa tuoshwe. Tunaonyesha kukubaliana nayo kwavile tunapofanya tendo la kuoshana miguu. Katika Yohana 13:12-17 tunaona tena jinsi wazo lile lilivyo.

Yohana 13:12-17 inasema:

12 Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niyowatendea? 13 Nyinyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwasema vema, maana ndivyo nilivyo.14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. 15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. 16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka. 17 Mkiyajua hayo heri ninyi mkiyatenda.

Maneno haya yapo hapa ili tufahamu kwamba kipo kielelezo ambacho wao na sisi tunapaswa kuelewa.

Nia ya Bwana na Mwalimu kuwaosha miguu wanafunzi wake, ninyi pia inawapasa kuoshana miguu kama mshiriki wa Kristo. Inatupasa kufanya hivyo kila mwaka katika kila siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. Hii sio Siku Takatifu, lakini inatakiwa ifanyike katika usiku ule aliosalitiwa, pamoja na kuula mkate na kunywa divai ili kuupata uzima wa milele.

Yohana 6:53-56 inasema:

53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua diku ya mwisho. 55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.

1Wakorintho 11:23-28 inasema:

23 kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa ninyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliyetolewa alitwaa mkate, 24 naya akiisha kushukuru, akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. 25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho wangu. 26 Maana kila mwulapo na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. 27 Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. 28 Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.

Usiku ule ulikuwa ni siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza na tunatakiwa kujipambanua na kuishiriki mwili. Tunapaswa kujihoji sisi wenyewe, na kupuuzia hili kunasababisha hukumu. Mkate wenye Chachu hautakiwi kuliwa wakati wa ibada hii (Kut.23:18). Kutoka 34:25 vilevile inaonyesha kuwa ingawa siku za Sikukuu ya mikate isiyotiwa Chachu hazijaanza, na mkate unaoliwa katika ibada hii ni lazima uwe ni ule usiotiwa chachu.

Kutoka 34:25 inasema:

25 Usisongeze damu ya sadaka yangu pamoja na mkate uliotiwa chachu; wala hiyo sadaka idi ya Pasaka haitasazwa hata asubuhi.

Mkate usiotiwa chachuulikuwa unatolewa kila siku kama sehemu ya utaratibu wa utoaji wa dhabihu. Masihi alikuwa ni dhabihu iliyokubalika na sasa, sisi washika maagano ni dhabihu.

Hii hutangulia na Pasaka na siku za Mikate isiyotiwa Chachu. Kutoka katika Mganda wa kutikiswa tunaanza kipindi cha kuelekea Pentekoste. Hapa tuna kipindi cha majuma saba kamili na Sikukuu na Siku Takatifu katika siku ya hamsini. Neno pentekoste lina maana ya “hesabu ya siku hamsini”. Yote mawili, Mganda wa Kutikiswa na Pentekoste zilikuwa na ibada zake katika saa tatu (au 3:00) asubuhi. Pentekoste ni mavuno ya malimbuko na kiroho inategemewa kuwa ni mavuno ya watu.

Hii inachukuliwa katika kipindi cha mzunguko wa Sabato saba za mapumziko ya ardhi, na ukamilifu wake wa mzunguko ule wa mara saba ya miaka ya Sabato, ambayo inaelekea katika mwaka wa Yubile. Utimilifu huu wa majuma saba kamili au Sabato kamili hadi Pentekoste na mzunguko wa miaka saba mara miaka saba hadi Yubile ni wa dhahiri. 

Jinsi ya Kutia Kwenye Matendo

Siku hizi Takatifu za kila mwaka zinapatikana katika Mambo ya Walawi 23:1-44, Kumbukumbu la torati 28 & 29. Siku Takatifu za kila mwaka ni kioo cha mpango wa wokovu wa Bwana. Ni muhimu kuziadhimisha na zinachukua umuhimu fulani kama ishara kati ya Mungu na watu wake. Siku takatifu zinaadhimishwa kama zilivyo Sabato. Kuna jumla ya Sikukuu za kila mwaka tatu na zimeandikwa katika Kutoka 23:14. Sadaka hutolewa kabla ya asubuhi ya siku ya kwanza ya kila mojawapo ya Sikukuu kama isemavyo Kutoka 23:18, Kumbukumbu la torati 16:16-17; 2Nyakati 8:13.

Ushirika wa Meza ya Bwana haimo miongoni mwa Siku Takatifu na inaitangulia Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Inatakiwa iadhimishwe kwa umuhimu wa kuurithi uzima wa milele katika ufufuo wa kwanza (Yoh.6:53-54). Pentekeste yapaswa iadhimishwe kama Sikukuu (ya majuma), (Kut.34:22; Kum.16:10, 16).  Sikukuu ya Vibanda ni muhimu kuiadhimisha ilikwamba watu woye waweze kusikiliza na kujifunza (Walawi 23:34;Kum.16:13, 16, 31:12). Bragumu na Upatanisho zimeitwa Siku [Takatifu] na sio Sikukuu (Law.23:24,27).

Miaka Saba Ya Mapimziko Ya Ardhi

Hii inajumlisha:

1.  Miaka saba kuachilia huru watumwa (Kut.21:2-6, Kum.15:12-18).

2.  Maachilio au kusamehe madeni (Kum.15:1-6), na

3.  Sabato ya mapumziko ya ardhi (Kut.23:10-11; Law.25:1-7, 19-24).

Baraza hili la kutunga sheria huhusisha maeneo yote ya masuala ya kimazingira, kiuchumi na kimaadili.

Katika mzunguko huu wa miaka saba, huitwa mzingo wa miaka saba au shemittah, tubapaswa kusoma Sheria za Mungu katika Sikukuu ya Vibanda.

Kumbukumbu la torati 31:10-13 inasema:

10 Musa, akaamuru, akasema, Mwisho wa kila mwaka wa saba, wakati wa maachilio, wakati ulioamriwa wa sikukuu ya vibanda, 11 Israeli wote wafikapo ili kuonekana mbele za BWANA, mungu wako, mahali pale atakapopachagua, uisome torati hii mbele ya Israeli wote masikioni mwao. 12 Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako, wapate kusikia na kujifunza, na kumcha BWANA, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii; na watoto wao wasiojua, wapate kusikia na kujifunza kumcha BWANA, Mungu wenu, siku zote mtakazo kaa katika nchi mnayoivukia Yordani ili kuimiliki. 

Utaratibu wowote wa Mungu wa sheria hulinda makabila, familia na kila mtu binafsi. Utaratibu wa Yubile na utoaji wake wa zaka, sabato zake, makatazo kwa madeni ya viwanja, ni mambo yaliyopuuziwa na kudharauliwa.

Tunasoma sheria ili kwamba watu wasiozielewa waweze kujifunza.

Ardhi yote ni mali ya Mungu na sisi tumepewa kama dhamana tu.

Walawi 25:23 inasema:

23 Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa; kwani nchi ni yangu mimi; maana ninyi ni wageni na wasafiri wangu.

Hii haimaanishi kuwa inaihusu ardhi ile tu iliyoitwa “Ardhi Takatifu”. Kila kitu ni mali ya Mungu na utaratibu wa Yubile umewekwa kwa faida ya wanadamu wote unachukua mahali pa wadamu wote, mahali pote tulipopewa katika mipaka ya familia (Kum.28:32).

Hatupaswi kudai kuwa ardhi au mito ni mali yetu.

Ezekieli 29:9 inasema:

9 Nayo nci ya Misri itakuwa na jangwa; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA; kwa sababu amesema, Mto huu ni wangu nami nimeufanya.

Ardi yote ni mali ya Mungu na kama hatuipi ardhi ifurahie Sabato zake katika kila mwaka wa saba, ndipo Mungu atakapoipatia kwa gharama itakayo tupata.

Walawi 26:34-35 inasema:

34 Hapo ndipo nchi itakapo zifurahia Sabato zake, wakati itakapokuwa hali ya ukiwa, nanyi mtakapokuwa katika nchi ya adui zenu; ndipo nchi itakapopumzika, na kuzifurahia Sabato zake. 35 Wakati wote itakapokuwa na ukiwa, itapumzika; ni hayo mapumziko ambayo haikuwa nmayo katika Sabato zenu, hapo mlipoiketi nchi hiyo.

Nchi au ardhi, itapewa mapumziko ambayo sisi tulipuuzia kuip, kwa jinsi tutakavyo chukuliwa mbali au kutekwa na kufanyika maganjo kama watu. Huu ni sehemu kati ya  mfumo mkamilifu wa Sabato kama ilivyo kwa Sabato ya siku ya saba ya wiki, hauwezi kubadilishwa wala kupuuziwa. Je, ninini maana vipimo hizi vikali?

Walawi 26:14 inasema:

14 Walakini msiponisikiza, wala hamtaki kuyafanya maagizo hayo yote;

Mwenendo wa kila mmoja wetu sawa na matumizi yetu mabaya ya ardhi na mazingira yanaweza kutusababishia .tutapikwe mbali na nchi.

Walawi 18:25-30 inasema:

25 hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa, 26 Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msijifanye machukizo hayo mojawapo, yeye aliyemzalia, wala mgeni aketiye kati yenu; 27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wamefanya haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi); 28 ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu. 29 Kwani awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazofanya zitakatiliwa mbali na watu wao. 30 Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi zichukizazo mojawapo, zilizo tangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Uvunjaji wa maagano, ambayo hujumlisha kwa kiasi kikubwa sana na Amri Kumi za Mungu, husababisha hukumu.

Walawi 26:43 inasema:

43 Nchi nayo itaachwa na wao, nayo itazifurahia Sabato zake, itakapokuwa ukiwa pasipokuwa na wao; nao wataikubali adhabu ya uovu wao; kwa sababu, naam, ni kwa sababu wamezikataa hukumu zangu, na roho zao zimezichukia amri amri zangu.

Uvunjaji wa maagano makamilifu ambayo baba zetu wote waliyaweka na Mungu pale Sinai, (Kut.24:3) husababisha hukumu. Tunamthibitishia tene kurudi kwetu kwake  kwa jiansi  ya Roho kwa njia ya ubatizo na kutamani kuyatunza kwasababu tunampenda Mungu Mmoja na Wapekee.

Flavius Josephus alinukuu katika kitabu kiitwacho Mapokeo ya Wayahudi, Kitabu cha XIV Sura ya X aya vi inaposema:

“Kaisari Caius, liwali kipindi cha pili, ameamuru kuwa nchi yote ya Yuda isipokuwa Yafa, watozwe kodi kila mwaka kwa ajili ya Yerusalemu, isipokuwa Mwaka wa saba wanaouita mwaka wa Sabato, kwa sababu kwa huo hawavuni matunda katika miti yao na wala hawapandi mbegu katika nchi yao; na kwamba walipe kodi yao Sidoni katika mwaka unaofuata wa (kipindi kile cha maadhimisho ya Sabato) sehemu ya nne ya kilicho vunywa au kupandwa”. (inaendana na 3: 12:3; 12:9; 5; 13; 8:1; 15:1:2)

Tunaambiwa kuwa sheria hizi za kale kutoka Walawi 26:34 (sawa na 2Nyakati 3621), ziliishilia katika hali ya kuto tunzwa na kwamba hali ya Yuda kupelekwa utmwani ulifidia kuifanya nchi ipumzike na kustarehe jambo ambalo lilipuuziwa. Mungu atafanya njia kuifanya ardhi ipumzike kama sisi tukikataa kufanya hivyo.

2 Nyakati 36:20-21inasema:

20 Na wale waliookoka na upanga akawachukua mpaka Babeli; wakamtumikia yeye na wanawe hata kulipoingia milki ya Uajemi; 21 ili kulitimiza neno la BWANA kwa kinywa cha Yeremia, hata nchi itakapofurahia Sabato zake; kwa maana siku zote ilipokaa ukiwa ilishika Sabato, kuitimiza miaka sabini.

Yeremia 29:19 nayo inasema:

19 Kwa sababu hawakusikiliza maneno yangu, asema BWANA, ambayo naliwatuma watumishi wangu, hao manabii, niliamka mapema, na kuwatuma; lakini hamkutaka kusikiliza, asema BWANA.

Kama ilivyokuwa imeahidiwa, walirudishwa katika nchi ya ahadi baada ya nchi kuwa imepata haki yake ya Sabato zilizokuwa zimepuuziwa. Ahadi nyingi za Mungu zimetegemeana na utayari wetu katika jinsi ile tutakavyo zitunza sheria zake kikamilifu na katika wakati uliowekwa. Hatuwezi kubadili chochote kuendana na mawazo yetu ya kwamba sisi tunafahamu vizuri, au kulingana na mapokeo yetu.

Tumeona kwa huyu Josephus kuwa Wayahudi waliamriwa kutunza sabato za kila mwaka wa saba kwa utaratibu Fulani. Hazikuwa zimetunzwa vizuri kwa miaka sahihi. Ingawa Wayahudi walikuwa wanalishika Sabato za kila juma, hawakuwa wameshika sheria.

Wagalatia 6:13 inasema:

13 Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kuona fahari katika miili yenu.  

Mungu hufanya mambo yake kwa watati wake.

Kutoka 12:41

41 Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ileile, ya kwamba majeshi yote ya BWANA yalitoka nchi ya Misri.

Ilikuwa ni vema tufanye kile ambacho Mungu anatamani kufanyika katika ratiba yake na kuacha kuendekeza mifumo yetu ambayo inahalifu Sheria zake, ambako ndiko sehemu ya faida yetu.

Sheria za kijamii za uchumi ambazo zinafanyiwa kazi hapa zaonyesha kuwa kila mtu apokee kiapande au sehemu ya raslimali iliyopo katika familia, iliyokabidhiwa kama dhamana ya siku zote. Imetolewa bure. Ni kipawa cha bure.

Nayo ardhi isiuzwe milele (Law.25:23) lakini itarudishwa kwenye familia husika katika mwaka wa Yubile. Ardhi  iligawanywa kwa kura, baada ya hesabu za kimazingira kumalika na kutathminiwa.

Yoshua 18:1-9 

Kasha mkutano mzima wa wana wa Israeli walikutana pamoja hapo Shilo, wakasimamisha hema ya kukutania huko; nayo nchi ilikuwa imeshindwa mbele zao. 2 Zilisalia katika wana wa Israeli kabila saba, ambazo hazijagawanywa bado urithi wao. 3 Yoshua akawauliza wana wa Israeli, akasema, Je! Hata lini mtakuwa walegevukatika kuingia kwenu na kuimiliki hiyo nchi, ambayo yeye BWANA, Mungu wa baba zenu, amewapa? 4 Haya, jichagulieni watu watatu kwa ajili ya kila kabila; nami nitawatuma, nao watainuka waende kati ya hiyo nchi, na kuiandika kama urithi wao ulivyo; kisha watanijilia mimi. 5 Watu hao watakapoifanya nchi iwe mafungu saba; Yuda atakaa katika mpaka wake huko upande wa kusini, na nyumba ya Yusufu watakaa katika mpaka wao upande wa kaskazini. 6 Nanyi mtaiandika nchi iwe mafungu saba, kasha hayo maandiko yake mtaniletea mimi hapa, nami nitawapigia kura hapa mbele za BWANA, Mungu wetu. 7 Kwa maana Walawi hawana fungu kati yenu; Kwa kuwa huo ukuhani wa BWANA ndio urithi wao; tena Gadi na Reubeni na hiyo nusu ya kabila ya Manase, wamekwishapata urithi wao ng’ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki, ambao walipewa na Musa mtumishi wa BWANA. 8 Basi watu hao wakainuka wakaenda; kisha Yoshua akawaagiza wale waliokwenda kuiandika nchi, akawaambia, Enandeni, mkapite katikati ya nchi na kuiandika habari zake, kasha mnijie tena hapa, nami nitawapigia kura kwa ajili yenu hapo mbele za BWANA huko Shilo. 9 Basi watu hao wakaenda, wakapita katikati ya nchi, waandika habari zake katika chuo, na kuigawanya kwa miji yake, hata iwe mafungu saba, kasha wakamrejea Youshua maragoni huko Shlo.

Maelekezo ya jinsi ya kugawa ardhi kwa kura yaliendelea hadi katika:

Yoshua 19:51 ambapo inasema:

51 Hizi ndizo nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa ya kabila za wana wa Israeli, walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huklo Shilo mbele ya BWANA,  hapo mlangoni mwa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.

Miji ya makimbilio ilijumlishwa katika zoezi hili la urithi wa makabila.